Maambukizi hutokea katika umri wowote, lakini ni sababu kubwa ya wasiwasi kwa watoto wachanga kwa sababu watoto hao, hasa waliozaliwa kabla ya wakati (njiti), wana mfumo wa kinga ambao bado haujakomaa na wako katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa. Ingawa baadhi ya kingamwili kingi hupita kutoka kwa mama kwenda kwa kijusi kupitia kondo la nyuma (plasenta), viwango vya kingamwili kwenye damu ya kijusi vinaweza visiwe vya kutosha kupambana na maambukizi.
Kijusi na mtoto mchanga anaweza kupata maambukizi kupitia njia zifuatazo:
Akiwa bado tumboni
Wakati wa kuzaliwa
Baada ya kuzaliwa
Maambukizi yanayopatikana kwenye mfuko wa uzazi (katika maambukizi ya utero)
Maambukizi kwa kijusi, ambayo yanaweza kutokea wakati wowote kabla ya kuzaliwa, hutokana na maambukizi aliyo nayo mama. Maambukizi ya mama hupita kwa kijusi kupitia kondo la nyuma (plasenta). Maambukizi hayo yanaweza kumsababishia mama dalili au yasisababishe dalili zozote. Wakati mwingine maambukizi hugunduliwa wakati wa ujauzito, lakini nyakati nyingine hayagunduliwi.
Maambukizi ya kawaida yanayopita kupitia kondo la nyuma ni pamoja na rubela, toksoplasmosisi, virusi vya saitomegalo (cytomegalovirus), virusi vya Zika, na kaswende. Virusi vya UKIMWI (VVU) na homa ya ini B ni maambukizi yanayoweza kupita kupitia kondo la nyuma ingawa hutokea kwa uchache zaidi. Pia kuna maambukizi mengine mengi adimu yanayoweza kumpata kijusi kabla ya kuzaliwa.
Athari kwa kijusi hutegemea aina ya kimelea kinachosababisha maambukizi na kipindi ambacho mama alipata maambukizi hayo wakati wa ujauzito. Matatizo yanayoweza kutokea ni pamoja na kuharibika kwa mimba, ukuaji wa kusuasua tumboni, kuzaliwa kabla ya wakati (njiti), mtoto kuzaliwa mfu, na ulemavu wa kuzaliwa.
Maambukizi yanayopatikana wakati wa kujifungua (maambukizi wakati wa kujifungua)
Kuna njia 2 kuu ambazo mtoto anaweza kupata maambukizi wakati wa uchungu wa uzazi na wakati wa kujifungua:
Ikiwa maambukizi yatatoka kwenye uke wa mama na kuingia kwenye mji wa mimba (uterasi) kabla mtoto hajazaliwa lakini baada ya chupa ya uzazi kupasuka, hasa ikiwa kuna ucheleweshaji kati ya kupasuka kwa chupa na wakati wa kujifungua
Ikiwa mtoto atagusana na damu au majimaji yaliyoambukizwa kutoka kwenye uke wa mama wakati wa uchungu wa uzazi au kujifungua
Maambukizi yanayoweza kutokea wakati wa kuzaliwa ni pamoja na VVU, virusi vya herpes simplex, homa ya ini B, bakteria za streptococcus, Escherichia koli (E. koli), listeriosis, kisonono (gonococcal infections), na klamidia.
Maambukizi yanayopatikana baada ya kujifungua (maambukizi baada ya kujifungua)
Maambukizi ya baada ya kuzaliwa hutokea wakati mtoto mchanga anapogusana moja kwa moja na tishu au majimaji ya mwili yaliyoambukizwa ya mama yake, kupitia kunyonyesha, au kupitia kugusana na wataalamu wa afya, familia, au wageni walioambukizwa wakiwa hospitalini (tazama Maambukizi Yanayopatikana Hospitalini kwa Watoto Wachanga)) au nyumbani.
Aina za maambukizi kwa watoto waliozaliwa karibuni
Maambukizi kwa watoto wachanga kwa kawaida husababishwa na bakteria au virusi, na kwa uchache husababishwa na fangasi au vimelea.
Bakteria zinazosababisha maambukizi kwa watoto wachanga mara nyingi ni pamoja na streptococci ya kundi B, E. koli, Listeria monocytogenes, gonococci, na chlamydiae.
Virusi ni pamoja na virusi vya herpes simplex (HSV), virusi vya UKIMWI (VVU), saitomegalovirusi (CMV), na virusi vya homa ya ini B (HBV).
Baadhi ya maambukizi yanayoweza kuwapata watu wa rika zote husababisha matatizo makubwa zaidi yanapotokea kwa kijusi au mtoto mchanga. Baadhi ya maambukizi hatari zaidi kwa watoto wachanga ni pamoja na haya yafuatayo:
Saitomegalovirusi (CMV)
Virusi vya Homa ya Ini B (HBV)
Tazama Candidiasis (Maambukizi ya Fangasi) kwa maambukizi yanayosababishwa na fangasi wa Candida.
Utambuzi wa Maambukizi kwa Watoto Waliozaliwa Karibuni
Uchunguzi wa daktari
Vipimo vya damu au majimaji ya mwili
Madaktari hushuku maambukizi kulingana na dalili za mtoto mchanga au kasoro (kama ulemavu wa kuzaliwa) na kupitia matokeo ya uchunguzi wa kimwili wa daktari.
Madaktari pia hupima sampuli za damu ya mtoto, majimaji ya uti wa mgongo, mkojo, mate, au tishu ili kubaini ikiwa kuna maambukizi na ni kimelea gani kinasababisha. Mama wa mtoto mchanga anaweza pia kuhitaji kupimwa.
Matibabu ya Maambukizi kwa Watoto Waliozaliwa Karibuni
Antibiotiki au dawa za kuzuia virusi (antivirals)
Maambukizi haya hutibiwa kulingana na kimelea kilichosababisha maambukizi.
Baadhi ya maambukizi ya bakteria hutibiwa kwa antibiotiki.
Baadhi ya maambukizi ya virusi yanaweza kutibiwa kwa dawa za kuzuia virusi.