Matumizi ya Kitu Wakati wa Ujauzito

NaRavindu Gunatilake, MD, Valley Perinatal Services;
Avinash S. Patil, MD, University of Arizona College of Medicine
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023 | Imebadilishwa Apr 2025
v86118072_sw

Baadhi ya dutu, ikiwemo kafeini, aspartame, pombe, na tumbaku, vinaweza kuwa na madhara kwa wanawake wajawazito na vijusi. Dawa haramu ni pamoja na amphetamines, bath salts, kokeini, hallucinogens, bangi, na dawa za afuni (mfano, heroin au matumizi mabaya ya dawa za afuni).

Matumizi ya dawa haramu (hasa dawa za afyuni) wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha matatizo wakati wa ujauzito na matatizo makubwa kwa kijusi kinachoendelea kukua na kwa mtoto mchanga. Hii inaweza kusababisha kasoro za kuzaliwa, ukuaji duni wa kijusi, au kuzaliwa kabla ya wakati. Kwa wanawake wajawazito, kudungwa dawa haramu kwa sindano huongeza hatari ya maambukizi yanayoweza kuathiri au kuenezwa kwenye kijusi. Maambukizi haya yanajumuisha homa ya ini na maambukizi ya VVU (ikiwa ni pamoja na UKIMWI).

Matumizi ya Kafeini Wakati wa Ujauzito

Kafeini, ambayo imo kwenye kahawa, chai, baadhi ya soda au vinywaji vingine, chokoleti na baadhi ya dawa ni kichocheo ambacho kinapita kwa urahisi kwenye plasenta kwenda kwenye kijusi.

Haiko wazi endapo kutumia kafeini wakati wa ujauzito kunadhuru kijusi. Utafiti unaonekana kupendekeza kwamba kutumie kafeini kwa viwango vidogo (kwa mfano, kikombe kimoja cha kahawa kwa siku) wakati wa ujauzito kunaweza kuwa na hatari kidogo au isiwepo kwa kijusi.

Baadhi ya tafiti zainapendekeza kwamba kunywa zaidi ya vikombe 7 vya kahawa kwa siku kunaweza kuongeza hatari ya kuzaa mtoto mfu, kuzaliwa kabla ya wakati, mtoto kuzaliwa akiwa na uzito wa chini, au kuharibika mimba.

Baadhi ya wataalamu wanapendekeza kupunguza matumizi ya kawaha na kunywa vinywaji visivyo na kafeini pale inapowezekana.

Matumizi ya Aspartame Wakati wa Ujauzito

Aspartame, sukari bandia, inaonekana kuwa salama wakati wa ujauzito ikiwa inatumiwa kwa viwango vidogo, kama vile kiasi kinachotumika katika sehemu za kawaida za vyakula na vinywaji vilivyo na sukari bandia.

Hata hivyo, mtu yeyote (pamoja na wanawake wajawazito) aliye na fenilketonuria, ugonjwa usio wa kawaida wa mmeng'enyo wa tindikali ya amino, hapaswi kutumia aspartame.

Kuvuta Sigara (Tumbaku) Wakati wa Ujauzito

Uvutaji sigara unaweka hatari kwa wanawake wajawazito na vijusi. Wanawake wanaojaribu kushika ujauzito au ambao ni wajawazito wanapaswa kuacha kuvuta sigara. Wataalamu wa huduma ya afya wanaweza kutoa nyenzo kuhusu mpango wa kuacha kuvuta sigara.

Madhara yasiyobadilika ya kuvuta sigara kwenye kijusi wakati wa ujauzito ni

Kadiri mwanamke anavyovuta sigara wakati wa ujauzito, ndivyo uwezakano wa mtoto kuongezeka uzito unakuwa mdogo.

Kasoro za kuzaliwa za moyo, ubongo na uso zipo sana kwa watoto wa wanawale waliokuwa wanavuta sigara.

Pia hatari ya haya yafuatayo inaweza kuongezeka:

Aidha, watoto wa wanawake wanaovuta sigara, wana upungufu mdogo lakini unaweza kuonekana katika ukuaji wa kimwili na maendeleo ya kiakili na tabia. Athari hizi zinafikiriwa kuwa zimesababishwa na kaboni monoksidi na nikotini. Kaboni monoksidi inaweza kupunguza usambazaji wa oksjeni kwenye tishu za mwili. Nikotini inachochea kutolewa kwa homoni zinazobana mishipa unayosambaza damu kwenye mji wa mimba na kondo la nyuma, kwa hivyo oksojeni na virutubishi vihache vinafikia kijusi.

Kwa sababu ya athari mbaya za kuvuta sigara wakati wa ujauzito, wanawake wajawazito, wanapaswa kufanya kila jitihada za kutovuta sigara wakati wa ujauzito, ikiwa ni pamoja na kujadili mikakati pamoja na daktari wao.

Wanawake wajawazito wanapaswa kuepuka kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu mwingine kwa sababu unaweza kumdhuru kijusi.

Matumizi ya Pombe Wakati wa Ujauzito

Kunywa pombe wakati wa ujauzito na chanzo kinachoongoza kinachojulikana cha kasoro za kuzaliwa. Kwa sababu kiasi au ruwaza ya kunywa pombe inayohitajika kusababisha maradhi ya athari za pombe za kabla ya kuzaliwa haijulikani, wanawake wajawazito wanashauriwa kutotumia pombe kabisa.

Je, Ulijua...

  • Sababu inayoongoza inayojulikana ya kasoro za kuzaliwa ni kunywa pombe wakati wa ujauzito.

Hatari ya kuharibika mimba karibu inaongezeka mara mbili kwa wanawake wanaokunywa pombe kwa namna yoyote wakati wa ujauzito, hasa wanapokunywa kwa wingi. Hatari huenda inategemea kiasi cha pombe kinachotumiwa, lakini hakuna kiasi kinachojulikana kuwa salama kabisa.

Maradhi ya athari za pombe za kabla ya kuzaliwa ni moja ya matokeo hatari zaidi ya kunywa pombe wakati wa ujauzito. Kunywa pombe hata vinywaji 3 kwa siku, kunaweza kusababisha ugonjwa huu. Unatokea kwa karibu watoto wanaozaliwa 2 kati ya 1,000. Ugonjwa huu unajumuisha yafuatayo:

Amfetamini Wakati wa Ujauzito

Matumizi ya amphetamines wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha kasoro za kuzaliwa, hasa za moyo, na pengine ukuaji duni kabla ya kuzaliwa.

Chumvi ya Kuoga (Visisimuaji vya Sintetiki) Wakati wa Ujauzito

Chumvi za kuoga hurejelea kundi la dawa za kusisimuwa kutoka kwenye dutu mbalimbali zinazofnana na amphetamine. Dawa hizi zinazidi kutumika sana wakati wa ujauzito.

Dawa hizi zinaweza kusababisha mishipa ya damu kwenye kijusi kusinya, hivyo kupunguza kiwango cha oksijeni kinachofika kwenye kijusi.

Pia, dawa hizi zinaongeza hatari ya:

Kokeini Wakati wa Ujauzito

Kokeini inayotumiwa wakati wa ujauzito inaweza kusababisha mishipa ya damu ambayo inapeleka damu kwenye mji wa mimba kusinyaa. Kisha, oksijeni kidogo na virutubishi vidogo vinafika kwenye kijusi.

Endapo wanawake wajawazito watatumia kokeini mara kwa mara, hatari ya haya yafuatayo inaongezeka:

Hata hivyo, haijulikani endapo kokeini ndicho chanzo cha matatizo hayo. Kwa mfano, chanzo kinaweza kuwa sababu vihatarishi vingine ambavyo vipo sana kwa wanawake wanatumia kokeini. Vihatarishi hivyo vinajumuisha kuvuta sigara, kutumia dawa zingine haramu, uangalizi wa kabla ya kujifungua usiojitosheleza, na umasikini.

Dawa Zenye Kuleta Jonzi Wakati wa Ujauzito

Hallucinogens, kutegemeana na dawa, inaweza kuongeza hatari ya haya yafuatayo:

Hallucinogens inajumuisha methylenedioxymethamphetamine (MDMA, au Ecstasy), rohypnol, ketamine, methamphetamine, na LSD (lysergic acid diethylamide).

Bangi Wakati wa Ujauzito

Dutu kubwa ya bangi, tetrahydrocannabinol, inaweza kuvuka kondo la nyuma na hivyo kuathiri kijusi. Hakuna kiasi cha bangi kinachochukuliwa kuwa salama wakati wa ujauzito, ingawa tafiti hazijaonyesha ongezeko la kasoro za kuzaliwa. Hata hivyo, tafiti za hivi karibuni zinaashiria kuwa matumizi ya bangi wakati wa ujauzito yanaweza kuhusishwa na uzito mdogo wa mtoto kuzaliwa na matatizo ya utotoni, ikiwemo masuala ya umakini, kujifunza, tabia, na mabadiliko katika ukuaji na utendaji kazi wa ubongo.

Dawa za Afyuni Wakati wa Ujauzito

Dawa za afyuni zinatumika kupunguza maumivu, lakini pia zinasababisha hali ya kujihisi kuwa na siha isivyo na uhalisia, na ikiwa ni nyingi zaidi, zinaweza kusababisha utegemezi au uraibu.

Dawa za afyuni, kama vile heroini, methadone, na morphine, zinapita kwenye kondo la nyuma kwa urahisi. Matokeo yake, kijusi kinaweza kuwa na uraibu wa hizo dawa na anaweza kuwa na dalili za kuacha kutumia saa 6 hadi siku 8 baada ya kuzaliwa. Hata hivyo, matumizi ya dawa za afyuni, ni nadra sana kusababisha kasoro za kuzaliwa.

Kutumia dawa za afyuni wakati wa ujauzito kunaongeza hatari ya matatizo wakati wa ujauzito, kama vile

Watoto wa watumiaji heroini wana uwezekano mkubwa wa kuzaliwa wakiwa na mwili mdogo.