Protozoa ni aina ya vimelea. Wanaunda kundi tofauti la viumbe vidogo, vyenye seli moja. Baadhi ya protozoa huhitaji mwenyeji binadamu au mnyama ili kuishi. Wengine huitwa "amiba zinazoishi kwa kujitegemea" kwa sababu ingawa ni vimelea, zinaishi kwenye udongo au maji na hazihitaji kuishi katika mwili wa binadamu au mnyama (angalia Utangulizi kwa Amiba Zinazoishi kwa Kujitegemea).
Wadudu wanaobeba na kusambaza vimelea vinavyosababisha magonjwa kwa watu huitwa vekta. Kwa mfano, mbu wa kike walioambukizwa ni wabebaji wa vimelea vinavyosababishamalaria, na mbung'o walioambukizwa ndio wabebaji wa vimelea vinavyosababishaUgonjwa wa usingizi wa kiafrika.
Protozoa inaweza kusababisha maambukizi katika viungo mbalimbali vya mwili wa mwanadamu zinamoishi, lakini protozoa za nje ya utumbo huitwa hivyo kwa sababu husababisha maambukizi katika maeneo ya nje ya utumbo pekee kama vile damu, ini, mapafu, ubongo, ngozi, na tishu zilizo chini ya ngozi. Maambukizi haya husababisha dalili na matatizo mbalimbali.
Maambukizi ya protozoa nje ya utumbo ni pamoja na yafuatayo:
(Angalia pia Muhtasari wa Maambukizi ya Vimelea.)