Kwa kawaida, uchungu na kujifungua hutokea bila matatizo yoyote. Matatizo makubwa ni nadra sana, na madaktari kwa kawaida wanaweza kuyagundua na kuyatibu. Ziara za mara kwa mara kwa daktari au mkunga aliyethibitishwa wakati wa ujauzito ni muhimu ili kuwa na ujauzito wenye afya na kugundua matatizo yakitokea. Baadhi ya matatizo hujitokeza ghafla na bila kutarajiwa, hivyo wanawake wajawazito wanapaswa kumpigia simu daktari au mkunga wao ikiwa kitu kinaonekana kuwa kibaya (kama vile kutokwa na damu, au kupungua kwa miondoko ya kijusi).
Mifano ya matatizo (changamoto) yanayoweza kujitokeza au kudhihirika tu baada ya mwanamke mjamzito kuanza uchungu au wakati wa kujifungua ni pamoja na:
Maambukizo kwenye uterasi (maambukizo yanayosababisha uvimbe wa tishu zinazozunguka kijusi)
Kukwama kwa bega (bega la kijusi kukwama kwenye mfupa wa fupanyonga ya mwanamke, na mtoto kunaswa kwenye njia ya uzazi)
Kuchomoza kwa kiunga mwana (kiunga mwana kutoka nje ya njia ya uzazi kabla ya mtoto)
Uterasi kupasuka (nadra)
Amniotic fluid embolism (kiowevu kinachokizunguka kijusi ndani ya uterasi kuingia kwenye mfumo wa damu wa mwanamke, jambo ambalo wakati mwingine husababisha athari inayotishia maisha)
Kutokwa na damu baada ya kujifungua (kutokwa na damu kupita kiasi kwenye uterasi wakati wa kujifungua)
Akreta ya kondo la nyuma (tatizo la kondo la nyuma ambalo linaweza kugunduliwa wakati wa ujauzito au baada ya mtoto kuzaliwa)
Changamoto zinapojitokeza, njia mbadala badala ya uchungu wa asili na kujifungua kwa njia ya kawaida zinaweza kuhitajika. Zinajumuisha
Koleo au kifaa cha kuvuta (inayoitwa upasuaji wa kumtoa mtoto) ili kumtoa mtoto
Wakati wa Uchungu wa uzazi na Kuzaa
Wastani wa muda wa ujauzito ni wiki 40, ukihesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho. Tarehe ya kujifungua huwekwa katika wiki ya 40, lakini haya ni makadirio tu. Wanawake wengi hawajifungui sawia na tarehe yao ya kutarajia, lakini baadhi hufanya hivyo.
Uchungu unaweza kuanza
Mapema mno (uchungu wa uzazi kabla ya wakati): Kabla ya wiki ya 37 ya ujauzito
Kuchelewa (baada ya muda): Baada ya wiki ya 42 ya ujauzito
Ikiwa mtoto atazaliwa mapema mno au kuchelewa mno, kuna hatari ya matatizo ya kiafya.
Uchungu unaweza kuwa wa mapema au kuchelewa kwa sababu mwanamke au kijusi ana tatizo la kimatibabu au kijusi kipo katika mkao usio wa kawaida.
Kuamua urefu wa ujauzito kunaweza kuwa kugumu kwa sababu tarehe sahihi ya kutungwa kwa mimba mara nyingi haiwezi kujulikana. Mapema katika ujauzito, kipimo cha picha kinachotumia mawimbi ya sauti kinaweza kusaidia kuamua umri wa ujauzito. Katika kipindi cha katikati hadi mwishoni mwa ujauzito, vipimo vya picha vinavyotumia mawimbi ya sauti si vya kuaminika sana katika kuamua urefu wa ujauzito.