Kujifungua Kwa Njia ya Upasuaji

(Sehemu-C)

NaJulie S. Moldenhauer, MD, Children's Hospital of Philadelphia
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Mar 2024
v8578575_sw

Kujifungua kwa njia ya upasuaji ni kujifungua mtoto kwa kuchana tumbo la mwanamke na mji wa mimba.

Nchini marekani, zaidi ya asilimia 30 ni ujifunguaji kwa njia ya upasuaji.

Madaktari wanatumia kujifungua kwa njia ya upasuaji wanapoona kuwa ni salama kuliko njia ya kawaida kwa mwanamke huyo, kwa mtoto, au wote wawili, kama vile pale ambapo:

  • Uchungu unaongezeka taratibu sana

  • Kijusi kipo katika mkao usio wa kawaida, kama vile utaratibu wa mtoto kuwa kinyume (kutanguliza matako)

  • Mapigo ya moyo ya kijusi si ya kawaida, ikiashiaria shida ya kujusi.

  • Kuvuja damu ukeni kupita kiasi, ikionyesha kwamba kondo la nyumalinaweza kujitenga na mji wa mimba mapema sana (mgawanyiko wa kondo la nyuma)

  • Kondo la nyuma linafunika shingo ya kizazi (placenta previa)

  • Mwanamke huyo amejifungua kwa njia ya upasuaji zaidi ya mara moja huko nyuma (kwa kawaida)

Huko nyuma, baada ya mwanamke kujifungua kwa njia ya upasuaji mara moja, madaktari walipendekeza kujifungua kwa njia ya upasuaji kwa mimba zote zinazofuata. Madaktari walikuwa na wasiwasi kwamba jeraha la mchano kwenye mji wa mimba linaweza kufuguka (kuchanika kwa mji wa mimba) wakati wa uchungu. Hata hivyo, madaktari sasa wanagundua kwamba hatari ya kuchanika ni ndogo baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji endapo upasuaji ulifanywa kwenye sehemu ya chini ya mji wa mimba na kwa mlalo. Kwa hivyo, wanawake wamewahi kujifungua kwa njia ya upasuaji mara moja huko nyuma na alichanwa kwa mlalo sehemu ya chini ya mji wa mimba, wanaweza kuchagua kujifungua kwa njia ya kawaida, inaitwa jaribio la uchungu baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji (TOLAC). Hata hivyo, ikiwa wanawake walijifungua kwa njia ya upasuaji kwa zaidi ya mara moja, madaktari wengi wanapendekeza kujifungua kwa njia ya upasuaji kwa mimba zote zinazofuata. Wanawake wanapaswa kujadili hatari pamoja na daktari wake kabla ya kuamua ama kujaribu TOLAC. Vituo vingi vinatumia orodha kaguzi kuhakikisha kwamba wanawake na watoto wake ni wataradhia wazu wa TOLAC salama na yenye mafanikio.

Ikiwa mwanamke anachagua kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji mara moja hapo awali, anapaswa kupanga kujifungua mtoto wake kwenye kituo chenye vifaa kuweza kufanya haraka huduma ya kujifungua kwa njia ya upasuaji

  • Kijifunguwa kwa kwaida hufanikiwa kwa karibu asilimia 60 hadi 80 kwa wanawake ambao hapo awali walijifungua kwa njia ya upasuaji kwa kuchanwa kwa mlalo.

  • Kuna hatari kidogo sana kwamba mji wa mimba utapasuka.

Je, Ulijua...

  • Ikiwa mwanamke amewahi kufanyiwa upasuaji wa kujifungua kwa kuchanwa kimlalo, anaweza kuzungumza na daktari wake kuhusu uwezekano wa kujifungua kwa njia ya kawaida kwenye ujauzito wake unaofuata.

Daktari wa wajawazito, mtaalamu wa nusukaputi, uauguzi na wakati mwingine daktari wa watoto wanahusika katika kujifungua kwa njia ya upasuaji. Kutumia nusukaputi, dawa zinazotolewa kwa njia ya mishipa, dawa za kuua baktaria na kuongezewa damu husaidia kufanya kujifungua kwa njia ya upasuaji kuwa salama.

Kwa kujifungua kwa njia ya upasuaji, mkato unaweza kufanywa sehemu ya juu au ya chini ya mji wa mimba.

  • Mkato wa chini: Aina hii ya mkato ni ya kawaida sana. Sehemu ya chini ya mji wa mimba ni nyembamba sana na ina mishipa michache ya damu, kwa hivyo kwa kawaida damu kidogo huwa inapotea. Pia, kovu lililopona huwa imara, kwa hivyo kuna uwezekano mdogo kufunguka kwenye mimba zinazofuata. Mkato wa chini kwa kawaida huwa ni wa mlalo. Mkato wa wima unafanywa endapo tu kuna hatari fulani, kama vile hali ya kutokuwa kawaida kwenye kondo la nyuma au kwenye ukubwa au mkao wa kijusi.

  • Mkato wa juu (wa zamani): Kwa kawaida, mkato huu unatumika pale ambapo kondo la nyuma linafunika shingo ya kizazi (tatizo linaloitwa placenta previa), kijusi kinapolala kimlalo kwenye njia ya uzazi, kijusi kinapokuwa njiti, au kijusi kinapokuwa na kasoro ya kuzaliwa.

Wanawake wanahimizwa kutembea muda mfupi baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji ili kupunguza hatari ya kuganda damu kwenye miguu au nyonga, kisha kusafiri kwenda kwenye mapafu na kuziba ateri hapo (kuziba kwa mishipa ya mapafu).

Kujifungua kwa njia ya upasuaji husababisha maumivu kwa ujumla baada ya hapo, kukaa hospitalini kwa muda mrefu na muda mrefu wa kupona kuliko kujifungua kwa njia ya kawaida.

Taarifa Zaidi

Nyenzo zifuatazo za lugha ya Kiingereza zinaweza kuwa muhimu. Tafadhali kumbuka kuwa MWONGOZO hauwajibiki kwa maudhui ya nyenzo hizi.

  1. Muunganiko wa Kuzaa Mtoto: Tovuti hii inatoa vidokezo vya kupata mtoto mwenye afya njema na kuzaliwa salama. Umuhimu wa huduma ya matibabu kabla, wakati, na baada ya kujifungua unasisitizwa.