Kuanzisha uchungu ni matumizi ya dawa ili kufanya uchungu uanze.
Kwa kawaida, uchungu unapohitaji kuanzishwa, mwanamke anapewa oksitosini, dawa ambayo inafanya mji wa mimba kukaza mara kwa mara zaidi na kwa nguvu zaidi. Oksitosini inayotolewa inafanana na oksitosini ya asili inayozalishwa na tezi ya pituitari. Inatolewa kwa njia ya mishipa kwa pampu ya kuingiza, ili kwamba kiwango cha dawa kinachotolewa kinaweza kudhibitiwa kwa usahihi.
Kabla ya mikazo ya mji wa mimba kuwekewa uchungu, shingo ya kizazi inapaswa iwe nyembamba na tayari kufunguka (kupanuka) ili mtoto aweze kutoka. Mbinu kadhaa zinaweza kutumika ili kusaidia shingo ya kizazi kuwa nyembamba na kupanuka:
Prostaglandini (dutu inayofanana na homoni kama vile misoprostol) inaweza kutolewa kwa njia ya uke.
Neli nyembamba, nyumbufu (katheta) ikiwa na puto limeambatishwa inaweza kuingizwa kwenye shingo ya kizazi. Puto linajazwa pumzi ili kuweka shinikizo dogo kisha kutanua shingo ya kizazi.
Mashina yaliyokaishuwa ya magugu maji (laminaria) inaweza kuingizwa kwenye shingo ya kizazi. Laminaria inanyonya majimaji kisha kutanuka, hivyo kupanua shingo ya kizazi.
Sababu za kuanzisha uchungu zinajumuisha
Shinikizo la juu la damu pamoja na protini kwenye mkojo (shinikizo la damu la juu wakati wa ujauzito)
Dalili kwamba kijusi hakiko sawa (shida ya kijusi)
Wakati mwingine uchungu unaanzishwa kwa sababu zisizohusiana na tatizo la kifaya. Kwa mfano, uchungu unaweza kuanzishwa mwanamke anapokuwa na historia ya kujifungua harakaharaka. Katika hali hizo, kuanzisha uchungu kunamaanisha kwamba mwanamke anaweza kuwasilia hospitalini au kituo cha kujifungua kwa wakati ili kijifungua mtoto.
Uchungu hauanzishwi katika mazingira yafuatayo:
Wanawake waliofanyiwa aina fulani ya upasuaji unaohusisha mji wa mimba au aina fulani za kujifungua kwa njia ya upasuaji.
Wanawake wana herpesi ya sehemu za siri.
Mji wa mimba upo katika mkao usio wa kawaida au ni mkubwa sana.
Kondo la nyuma lipo katika mkao usio sahihi (placenta previa au vasa previa).
Katika muda wote wa kuanzisha uchungu na wakati wa uchungu, mapigo ya moyo ya kijusi yanafuatiliwa kielektroniki.
Ikiwa kuanzisha uchungu hakujafanikiwa, mtoto anazaliwa kwa kufanyiwa upasuaji.
Taarifa Zaidi
Nyenzo zifuatazo za lugha ya Kiingereza zinaweza kuwa muhimu. Tafadhali kumbuka kuwa MWONGOZO hauwajibiki kwa maudhui ya nyenzo hizi.
Muunganiko wa Kuzaa Mtoto: Tovuti hii inatoa vidokezo vya kupata mtoto mwenye afya njema na kuzaliwa salama. Umuhimu wa huduma ya matibabu kabla, wakati, na baada ya kujifungua unasisitizwa.