Kasoro za kuzaliwa nazo, pia zinajulikana kama hali zisizo za kawaida wakati wa kuzaliwa, ni kasoro za kimwili zinazotokea kabla ya mtoto kuzaliwa. "Matatizo ya kuzaliwa nayo" humaanisha "kuwepo tangu kuzaliwa."
Kasoro za kuzaliwa nazo katika mifupa, viungo, na misuli (zinazojulikana kama kasoro za mfumo wa mifupa na misuli) ni za kawaida miongoni mwa watoto. Huenda zikahusisha sehemu maalum ya mwili pekee, kama vile mguu (tatizo la mguu uliojipinda). Au zinaweza kuwa sehemu ya ugonjwa wa kijenetiki wenye kasoro nyingi, ambapo kasoro za kuzaliwa huathiri si mifupa, viungo, na misuli tu bali pia sehemu nyingine nyingi za mwili.
Arthrogryposis multiplex congenita inarejelea kundi la matatizo adimu ya kuzaliwa nayo yanayosababishwa na mwendo mdogo wa viungo mtoto akiwa kwenye mfuko wa uzazi. Mwendo mdogo husababisha viungo vingi kupinda na “kuganda” katika mkao mmoja.
Kasoro za nyonga na viungo zinajumuisha displasia ya ukuaji wa nyonga na kuteguka kwa goti.
Kasoro za viungo ni nyingi. Wakati mwingine kiungo kinakosekana au hakijakua kikamilifu. Sehemu au mkono mzima au mguu mzima unaweza kukosekana. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na vidole vichache au vingi kupita kiasi vya mikono au miguu. Tatizo la mguu uliojipinda (talipes equinovarus) ni kasoro ambayo mguu na kifundo cha mguu hupinda nje ya umbo au mkao wa kawaida. Kasoro nyingine za mguu ni pamoja na kupinda ndani kwa nusu ya mguu, kupinda ndani kwa nusu ya mbele ya mguu, kupinda juu kupita kiasi kwa mguu na kwa kifundo cha mguu, na kasoro ya sehemu ya chini ya miguu kuwa bapa.
Katika miguu inayopinda inje, magoti inayopinda kwenda nje. Katika miguu inayopinda ndani, magoti yanaonekana kupinda ndani. Kasoro nyingine zinazoathiri miguu ni pamoja na kupindika kwa sehemu ya juu ya mfupa wa paja (femoral torsion) na kupindika kwa muundi wa mguu (tibial torsion).
Kasoro za misuli zinaweza kuwepo wakati wa kuzaliwa. Watoto wanaweza kuzaliwa bila misuli binafsi au makundi ya misuli, au misuli inaweza kuwa haijakua kikamilifu. Kasoro katika misuli zinaweza kutokea peke yake au kama sehemu ya ugonjwa.
Kasoro za shingo na mgongo zinaweza kusababishwa na majeraha ya tishu laini au mifupa. Kasoro mbili zinazotokea mara nyingi zaidi ni
Kasoro za uti wa mgongo zinajumuisha skoliosisi, ambayo mara chache huonekana wakati wa kuzaliwa, na kasoro mahususi za uti wa mgongo, ambazo zinaweza kutambuliwa wakati wa kuzaliwa. Magonjwa kadhaa tofauti ya kijenetiki hujumuisha skoliosisi kama mojawapo ya kasoro zao. Kadri watoto wanavyokua, mkunjo wa mgongo unaosababishwa na kasoro ya uti wa mgongo unaweza kuongezeka haraka. Madaktari hufuatilia hali ya uti wa mgongo kwa ukaribu.
Kasoro za kuzaliwa zinaweza kuainishwa kama
Mabadiliko ya umbo
Ulemavu
Mabadiliko ya umbo ni mabadiliko katika umbo la sehemu ya mwili. Mabadiliko ya umbo husababishwa na shinikizo lisilo la kawaida kwa mtoto anapokuwa kwenye mfuko wa uzazi (kwa mfano, ganda la nje la sikio hujikunja) au baada ya mtoto kuzaliwa (kwa mfano, baadhi ya mabadiliko ya umbo la fuvu). Baadhi ya mabadiliko huboreka bila matibabu ndani ya siku chache, lakini mengine yanahitaji kutibiwa.
Ulemavu ni hitilafu katika ukuaji wa mtoto ambayo hutokea kwenye mfuko wa uzazi. Vyanzo vya ulemavu ni pamoja na kasoro za kromosomu, kasoro za jeni moja, na mambo ya kimazingira (kama vile teratojeni, ambavyo ni vitu vinavyojulikana kusababisha kasoro za kuzaliwa). Ulemavu unaweza pia kusababishwa na mchanganyiko wa vipengele vya kijenetiki na mazingira. Katika baadhi ya visa, chanzo hakijulikani.