Tatizo la Kuzaliwa la Shingo Fupi na Pinde

NaJoan Pellegrino, MD, Upstate Medical University
Imekaguliwa naAlicia R. Pekarsky, MD, State University of New York Upstate Medical University, Upstate Golisano Children's Hospital
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Nov 2024
v36025610_sw

Tatizo la kuzaliwa la shingo fupi na pinde ni kasoro ya kuzaliwa nayo ambapo kichwa hupinda wakati wa kuzaliwa au muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Kasoro za kuzaliwa nazo, pia zinajulikana kama hali zisizo za kawaida wakati wa kuzaliwa, ni kasoro za kimwili zinazotokea kabla ya mtoto kuzaliwa. "Congenital" ina maana "iko wakati wa kuzaliwa." (Angalia pia Utangulizi wa Kasoro za Kuzaliwa kwa Mifupa, Viungo na Misuli.)

Chanzo cha kawaida zaidi cha tatizo la Kuzaliwa la shingo fupi na pinde ni

  • Jeraha lililo kwenye shingo ya mtoto wakati wa kujifungua

Jeraha hilo linaweza kuharibu misuli ya shingo na/au kusababisha mkusanyiko wa damu (hematoma) kwenye misuli ya shingo. Hizi zinaweza kusababisha unene usio wa kawaida wa tishu za shingo (fibrosisi) na kukakamaa kwa misuli ya shingo (kukazika kwa viungo). Ni nadra sana, mifupa ya uti wa mgongo (uti) inaweza kuvunjika au kutoka mahali pake wakati wa kuzaliwa. Mabadiliko fulani ya jeni yanaweza kuchangia.

Vyanzo vingine vya tatizo la kuzaliwa la shingo fupi na pinde vinavyo jitokeza katika siku au wiki za mwanzo wa maisha ni pamoja na kasoro za uti wa mgongo kama vile

  • Ugonjwa wa Klippel-Feil (muunganiko wa uti wa mgongo shingoni, shingo fupi, na nywele zilnizoanzia chini kuliko kawaida)

  • Muunganiko wa Atlanto-oksipitali (ambayo ni muunganiko wa uti wa mgongo wa kwanza hadi sehemu ya chini ya fuvu)

Ugunduzi wa Tatizo la Kuzaliwa la Shingo Fupi na Pinde

  • Tathmini ya daktari

  • Kwa kawaida eksirei

Ili kutambua kasoro, madaktari hufanya uchunguzi wa kimwili. Pia hufanya vipimo vya upigaji picha, kama vile eksirei za mifupa ya shingo na mabega, ili kutafuta matatizo.

Matibabu ya Tatizo la Kuzaliwa la Shingo Fupi na Pinde

  • Inalingana na kisababishaji

  • Kuzungusha kichwa na kunyoosha shingo

  • Wakati mwingine sindano za sumu ya botulinum

Matibabu ya tatizo la kuzaliwa la shingo fupi na pinde inayosababishwa na jeraha la misuli ya shingo ni pamoja na kuzungusha kichwa na kunyoosha shingo. Wakati tatizo la kuzaliwa la shingo fupi na pinde ni ngumu kutibu, madaktari hudunga sindano yenye sumu ya botulinum kwenye misuli ya shingo iliyokakamaa. Sindano hizo hulegeza misuli migumu.

Madaktari wanaweza kufanya upasuaji ili kurekebisha au kutuliza majeraha na kasoro za uti wa mgongo.

Kwa sababu jeni zisizo za kawaida zinaweza kuhusika katika uundaji wa tatizo la Kuzaliwa la shingo fupi na pinde, familia zilizoathiriwa zinaweza kufaidika na ushauri nasaha wa jenetiki.