Mgongo kupinda kando

NaNora E. Renthal, MD, PhD, Harvard Medical School
Imekaguliwa naMichael SD Agus, MD, Harvard Medical School
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Sept 2025
v821292_sw

Skoliosisi ni hali ya kupinda kusiko kwa kawaida kwa uti wa mgongo.

  • Skoliosisi inaweza kuonekana wakati wa kuzaa au inaweza kutokea katika umri wa balehe.

  • Aina ndogo inaweza kusababisha maumivu kidogo tu ya mgongo, lakini aina mbaya zaidi inaweza kusababisha maumivu ya muda mrefu au kuathiri viungo vya ndani.

  • Utambuzi wa ugonjwa unatokana na uchunguzi na eksirei.

  • Si aina zote za skoliosisi zinakuwa mbaya, lakini zile ambazo lazima zitibiwe mapema kadiri iwezekanavyo ili kuzuia ulemavu mbaya.

  • Vifungo na upasuaji unaweza kuhitajika ili kunyoosha uti wa mgongo.

(Angalia pia Muhtasari wa Matatizo ya Mifupa kwa Watoto.)

Skoliosisi inapatikana kwa watu wengi kwa kiasi fulani na inatokea katika asilimia 1 hadi 3 ya watoto wenye umri wa miaka 10 hadi 16. Wavulana na wasichana wanaathiriwa kwa usawa. Hata hivyo, kwa wasishana, skoliosisi inaweza kuendelea mara 10 zaidi na kuhitaji kufungwa au kufanyiwa upasuaji.

Skoliosisi inaweza kutokana na sababu za kurithi au matatizo ya kuzaliwa au inaweza kutokea baadaye katika maisha, mara nyingi zaidi katika umri wa balehe. Kwa kawaida, sababu haiwezi kubainishwa (inaitwa skoliosisi ya idiopathiki).

Skoliosisi ya Idiopathiki
Ficha Maelezo

This photo shows an adolescent girl with severe scoliosis (curvature of the spine).

MEDICAL PHOTO NHS LOTHIAN/SCIENCE PHOTO LIBRARY

Dalili za Mgongo Kupinda Kando

Skoliosisi ndogo inaweza kuonekana wakati wa ucunguzi wa kimwili wa mara kwa mara. Mzazi, mwalimu au daktari anaweza kushuku skoliosisi wakati moja ya mabega ya mtoto linaonekana kuwa refukuliko jingine au wakati ambapo nguo za mtoto hazining'inii moja kwa moja.

Skoliosisi ndogo kwa kawaida haisababishi dalili. Wakati mwingine mgongo unakuwa mchungu au mgumu baada ya mtoto kukaa au kusimama kwa kipindi kirefu cha muda. Maumivu ya kadiri au makali zaidi hatimaye yanaweza kufuatia.

Uti wa mgongo kwa kawaida unavimba kuelekea kulia wakati mkundo upo kwenye sehemu ya juu ya mgongo na upande wa kulia unapokuwa katika sehemu ya chini ya mgongo. Matokeo ni kwamba bega la kulia kwa kawaida linakuwa juu kuliko la kushoto. Nyonga moja inaweza kuwa juu kuliko nyingine. Kifua kinaweza kisiwe kimenyooka. Skoliosisi mara nyingi inatokea kwa watoto wenye kyphosis. Muunganiko unaitwa kifoskoliosisi.

Utambuzi wa Mgongo Kupinda Kando

  • Eksirei

Utambuzi wa ugonjwa wa skoliosisi, daktari anamwambia mtoto kuinama kuelekea mbele na kuutazama uti wa mgongo kutokea nyuma kwa sababu mkunjo usio wa kawaida wa uti wa mgongo unaweza kuonekana kwa uarahisi zaidi kwenye mkao huu.

Skoliosisi: Uti wa Mgongo Uliopinda

Eksirei zinaonyesha pembe sahihi za mwinamo. Kiwango cha mwinamo kinafasiliwa kama pembe kati ya mistari 2 iliyochorwa kwenye eksirei ya uti wa mgongo. Pembe hiyo inaitwa pembe ya Cobb. Mstari mmoja unaenea kutoka juu ya pingili la uti wa mgongo wa juu ulioinama zaidi na mstari mwingine unaenea kutoka chini ya pingili ya uti wa mgongo wa chini ulioinama zaidi.

Pembe ya Cobb

Kwenye mbinu ya Cobb, mistari 2 inachorwa kwenye eksirei ya uti wa mgongo. Mstari mmoja unaenea kutoka juu ya pingili la uti wa mgongo wa juu ulioinama zaidi na mstari mwingine unaenea kutoka chini ya pingili ya uti wa mgongo wa chini ulioinama zaidi. Pembe zinazoundwa na mistari hii ni pembe ya Cobb. (Upande wa mbinuko ndipo mgongo unapinda kutoka nje. Upande wa mbonyeo ni pale ambapo mgongo unapinda kuelekea ndani.)

Ikiwa madaktari wanafikiri skoliosisi inaweza kuwa mbaya, wanaweza kumchunguza mtoto mara kadhaa kwa mwaka. Vifaa maalumu vinaweza kutumika kupima mbonyeo wa mgongo kwa usahihi zaidi.

Matibabu ya Mgongo Kupinda Kando

  • Kifungio na tiba ya viungo

  • Wakati mwingine upasuaji

Skoliosisi inayosababisha dalili, inakuwa mbaya au ni mbaya zaidi huenda ikahitaji kutibiwa. Matibabu yakianza mapema, ndipo kunakuwa na uwezakano mkubwa wa kuzuia ulemavu mbaya kabisa.

Kifungio au kifaa kilichoundwa ili kufunga uti wa mgongo (orthosisi) kinaweza kuvaliwa ili kunyoosha uti wa mgongo. Watoto pia wanafanyiwa tiba ya kimwili ili kuzuia ulemavu zaidi.

Kwa watoto ambao wana skoliosisi ya kadiri au mbaya, pingili ya uti wa mgongo zinaweza kuhitaji kuunganishwa pamoja katika utaratibu wa upasuaji unaoitwa muunganiko wa uti wa mgongo. Fimbo ya chuma inaweza kuingizwa wakati wa upasuaji ili kufanya mgongo unyooke hadi pingili zishikane kabisa.

Skoliosisi na matibabu yake mara nyingi huingiliana na vile mtoto aliye kwenye balehe anavyojitazama. Ushauri nasaha au tiba ya kisaikolojia inaweza kuhitajika.

Ubashiri wa Mgongo Kupinda Kando

Ubaya wa mbinuko, mahali ulipo mbinuko na umri wa mtoto unachangia uwezekano wa skoliosisi kuwa mbaya sana. Kadiri mbinuko unavyokuwa mbaya zaidi, ndivyo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa skoliosisi kuwa mbaya. Hatari ya mbinuko kuwa mbaya ni kubwa zaidi wakati skoliosisi imetambuliwa katika umri mdogo, wakati mifupa bado inakua kwa kiasi kikubwa na mbinuko huwa unakuwa mbaya katika hatua za mapema za mbapo ukuaji unakuwa wa haraka. Vilevile, kadiri dalili zinavyoongezeka, kunakuwa na uwezekano mkubwa kwamba skoliosisi inaweza kuwa mbaya. Mbinuko kwenye sehemu ya juu ya mgongo (thoracic) unaweza kuwa na hali mbaya zaidi kuliko mbinuko kwenye sehemu ya chini ya mgongo (lumbar).

Skoliosisi iliyo katika hali mbaya hatimaye inaweza kusababisha matatizo ya kudumu, kama vile ulemavu unaoonekana au maumivu ya muda mrefu. Skoliosisi mbaya inaweza kuathiri hata viungo vya ndani. Kwa mfano, ubaya wa mbinuko unaweza kuleta ulemavu au kuharibu mapafu.

Kwa watoto wengi wenye skoliosisi, mbinuko haui mbaya badala yae unabaki kuwa mdogo. Hata hivyo, unapaswa kufuatiliwa na daktari mara kwa mara.