Nimothoraksi ni kuanguka kwa sehemu ndogo au mapafu yoye kutokana na mkusanyiko wa hewa kati ya mapafu na ukuta wa kifua.
Ugonjwa huu unaweza kutokea kwa watoto waliozaliwa majuzi ambao wamezaliwa kabla ya wakati, ambao wana ugonjwa wa mapafu kama vile ugonjwa wa shida ya kupumua au ugonjwa wa kupumua meconium, au ambao hutibiwa kwa shinikizo la hewa linaloendelea (CPAP) au mashine ya kupumulia.
Mapafu yanaweza kuanguka, kupumua kunaweza kuwa kugumu, na shinikizo la damu linaweza kupungua.
Utambuzi kwa kawaida hushukiwa kulingana na matatizo ya kupumua au viwango vya chini vya oksijeni na huthibitishwa kwa eksrei ya kifua.
Watoto waliozaliwa majuzi ambao wana shida ya kupumua hupewa oksijeni, na wakati mwingine hewa huondolewa kwenye uwazi wa kifua kwa kutumia sindano na sirinji au mrija wa plastiki wa kutoa majimaji ambao huachwa mahali pake.
(Angalia pia Muhtasari wa Matatizo ya Jumla kwa Watoto Wachanga na Nimothoraksi kwa watu wazima.)
Nimothoraksi ni aina ya ugonjwa wa uvujaji wa hewa. Hewa inapovuja kutoka kwenye mapafu na kuingia kwenye nafasi inayozunguka mapafu, haiwezi kutoka na inaweza kujilimbikiza. Ujilimbikizaji huu wa hewa husababisha shinikizo kwenye mapafu, kwa hivyo hayawezi kupanuka kama kawaida mtoto aliyezaliwa majuzi anapopumua.
Nimothoraksi kubwa inaweza kusababisha ugumu mkubwa wa kupumua pamoja na matatizo ya moyo. Ikiwa hewa ya kutosha itajilimbikiza katika nafasi kati ya mapafu na ukuta wa kifua, mishipa inayopeleka damu kwenye moyo hubanwa. Matokeo yake, damu kidogo hujaza vyumba vya moyo, utoaji wa damu kutoka moyoni hupungua, na shinikizo la damu la mtoto maliyezaliwa majuzi hupungua. Hii huitwa nimothoraksi ya mkazo.
Nimothoraksi mara nyingi hutokea kwa watoto waliozaliwa majuzi wenye mapafu yenye mkazo, kama vile watoto waliozaliwa kabla ya wakati au walio na ugonjwa wa shida ya kupumua au ugonjwa wa kupumua meconium.
Nmothoraksi inaweza pia kutokea kama tatizo linalotokana na matumizi ya mashine ya shinikizo la njia ya hewa linaloendelea (CPAP) au kifaa cha kupumulia. CPAP ni mbinu inayowaruhusu watoto wachanga kupumua wenyewe huku wakipokea hewa au oksijeni yenye shinikizo kidogo, na mashine ya kupumulia ni mashine inayosaidia hewa kuingia na kutoka kwenye mapafu. Kwa sababu matibabu haya yote mawili husukuma hewa kwenye mapafu chini ya shinikizo (badala ya hewa kufyonzwa kama wakati wa kupumua kwa kawaida), yanaweza kudhuru mapafu na kusababisha uvujaji wa hewa, hasa mapafu yanapokuwa tayari yamekaza.
Nimothoraksi inaweza kutokea mara kwa mara kwa watoto waliozaliwa majuzi ambao hawana ugonjwa wa mapafu uliopo na ambao hawahitaji msaada wa kupumua. Kwa watoto hawa waliozaliwa majuzi, nimothoraksi mara nyingi hupatikana kwa bahati mbaya, na watoto hawa huenda wasihitaji matibabu yoyote. Hata hivyo, wakati mwingine nimothoraksi ya ghafla inaweza kuhatarisha maisha, na baadhi ya watoto waliozaliwa majuzi ambao wana nimothoraksi ya ghafla hupata ugonjwa mwingine wa mapafu unaoitwa shinikizo la juu la damu linaloendelea la mapafu. Madaktari huwafuatilia kwa karibu watoto wote wachanga wenye nimothoraksi.
Magonjwa meningine ya uvujaji wa hewa
Dalili zingine za uvujaji wa hewa ni pamoja na zifuatazo:
Pneumomediastinum
Interstitial emphysema ya mapafu (hewa katika tishu za mapafu kati ya vifuko vya hewa)
Pneumopericardium (hewa kwenye kifuko kinachozunguka moyo)
Pneumoperitoneum (hewa kwenye uvungu wa tumbo)
Emphysema ya ngozi (hewa chini ya ngozi)
Hewa inayovuja kutoka kwenye mapafu hadi kwenye tishu katikati ya kifua huitwa pneumomediastinum. Tofauti na nimothoraksi, hali hii kwa kawaida haiathiri kupumua na haihitaji matibabu. Pneumomediastinum kwa kawaida hugunduliwa tu wakati ambapo mtoto mchanga anafanyiwa eksrei ya kifua kwa tatizo lisilohusiana.
Pneumopericardium na pneumoperitoneum ni dharura za kimatibabu.
Interstitial emphysema ya mapafu inaweza kuhitaji mabadiliko katika mkao, au mbinu maalum za uingizaji hewa.
Emphysema ya ngozi ni nadra na mara nyingi ni tatizo la dalili zingine za uvujaji wa hewa. Mara nyingi hutoweka yenyewe na mara chache huhitaji matibabu ya ziada.
Dalili za Pneumothoraxia katika mtoto mchanga
Nimothoraksi kwa mtoto aliyezaliwa majuzi wakati mwingine haisababishi dalili zozote. Hata hivyo, kwa kawaida husababisha kupumua kwa kasi na kwa shida. Watoto waliozaliwa majuzi pia wanaweza kuguna wanapopumua na wanaweza kuwa na rangi ya bluu kwenye ngozi na/au midomo yao (cyanosis). Kwa watoto waliozaliwa karibuni wenye ngozi nyeusi, ngozi inaweza kuonekana kama bluu, kijivu, au nyeupe, na mabadiliko haya yanaweza kuonekana kwa urahisi zaidi kwenye utando wa kamasi ulio ndani ya mdomo, pua na kope.
Kifua kwenye upande ulioathiriwa ni kikubwa kuliko upande usioathiriwa.
Utambuzi wa ugonjwa wa Pneumothoraxia katika mtoto mchanga
Transillumination
Eksirei ya kifua
Madaktari hushuku nimothoraksi kwa watoto waliozaliwa majuzi ambao hupata shida ya kupumua inayozidi kuwa mbaya. Wakati wa kuwachunguza watoto hawa waliozaliwa majuzi, madaktari wanaweza kugundua sauti ndogo za hewa inazoingia na kutoka kwenye mapafu upande wa nimothoraksi.
Wakati mwingine madaktari huweka taa ya fiberoptic kwenye upande ulioathiriwa wa kifua cha mtoto aliyezaliwa majuzi wakiwa katika chumba chenye giza (transillumination). Mwanga huo huangaza kupitia ukuta mwembamba wa kifua cha mtoto aliyezaliwa majuzi na unaweza kuonyesha mifuko ya hewa katika nafasi inayozunguka mapafu. Transillumination mara nyingi haisaidii kwa watoto wakubwa.
Eksrei ya kifua inathibitisha utambuzi wa nimothoraksi kwa mtoto aliyezaliwa majuzi.
Matibabu ya Pneumothoraxia katika mtoto mchanga
Oksijeni
Wakati mwingine kuondolewa kwa hewa kutoka kwenye kifua
Hakuna matibabu yanayohitajika kwa watoto waliozaliwa majuzi ambao hawana dalili na ambao wana nimothoraksi ndogo.
Watoto waliozaliwa kwa wakati ambao wana dalili ndogo wanaweza kuwekwa kwenye hema dogo ambapo oksijeni husukumwa (kifuniko cha oksijeni) au kupokea oksijeni kupitia mirija miwili inayowekwa puani ili wapumue hewa yenye oksijeni zaidi kuliko hewa iliyo chumbani. Kiasi cha oksijeni wanachopewa kwa kawaida kinatosha kudumisha viwango vya kutosha vya oksijeni katika damu.
Ikiwa kupumua kwa mtoto aliyezaliwa majuzi kuna shida au ikiwa kiwango cha oksijeni katika damu kinapungua, na hasa ikiwa mzunguko wa damu umeharibika, hewa lazima iondolewe haraka kutoka kwenye uwazi wa kifua. Hewa huondolewa kwenye uwazi wa kifua kwa kutumia sindano na sirinji au kwa kuweka mrija wa plastiki kwenye uwazi wa kifua ili kuendelea kufyonza na kutoa hewa kutoka humo. Mrija huondolewa baada ya madaktari kuhakikisha hakuna hewa zaidi itakayojilimbikiza, kwa kawaida baada ya siku kadhaa.
Pneumomediastinum haihitaji matibabu na hutoweka yenyewe.