Matumizi ya Dawa na Kitu Wakati wa Kunyonyesha

NaRavindu Gunatilake, MD, Valley Perinatal Services;
Avinash S. Patil, MD, University of Arizona College of Medicine
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023 | Imebadilishwa Jul 2024
v36961352_sw

Wakati wanwake wanaonyonyesha wanapotakiwa kutumia dawa, wanajiuliza endapo wanapaswa kuacha kunyonyesha. Jibu linategemea yafuatayo:

  • Kiasi gani cha dawa kinachoingia kwenye maziwa

  • Endapo dawa imenyonywa na mtoto

  • Jinsi gani dawa hiyo inamwathiri mtoto

  • Ni kiasi gani cha maziwa ambacho mtoto anatumia, hali ambayo inategemea umri wa mtoto na kiwango cha vyakula vingine na vimiminika kwenye mlo wa mtoto

Baadhi ya dawa, kama vile, epinephrine, heparin, na insulin, haziingii kwenye maziwa ya mama kwa hivyo ni salama kutumia. Dawa nyingi zinaingia kwenye maziwa ya mama lakini kwa kawaida ni kwa kiwango kidogo. Hata hivyo, hata katika kiwango kidogo, baadhi ya dawa zinaweza kumdhuru mtoto.

Baadhi ya dawa zinapita kwenye maziwa ya mama, lakini kwa kawaida mtoto anafonya kidogo sana kiasi kwamba haziwezi kumwathiri mtoto. Mifano ni dawa za kuua baktaria za gentamicin, kanamycin, streptomycin, na tetracycline.

Pale inapowezekana, dawa zinapaswa kutumiwa haraka baada ya kunyonyesha au kabla ya kipindi kirefu zaidi cha mtoto kulala.

Dawa Ambazo ni Salam Kiasi Wakati wa Kunyonyesha

Dawa zinazochukuliwa kuwa ni salama zinajumusiha dawa nyingi ambazo haziagizwi na madaktari (dawa za kununua dukani). Isipokuwa kwa dawa za antihistamines (kwa kawaida zinatumika kwenye tiba ya kikohozi na mafua, dawa za mzio, dawa za kichefuchefu cha kujongea, na dawa za kusaidia kupata usingizi) na ikiwa zitatumiwa kwa kiwango kikubwa kwa muda mrefu, aspirini na salicylates nyinginezo. Acetaminophen na ibuprofen, zikitumiwa katika dozi ya kawaida zinaonekana kuwa salama.

Dawa zinazotumika kwenye ngozi, macho, au pua au zile ambazo zinavutwa kwa pumzi kwa kawaida ni salama.

Dawa nyingi za kupunguza shinikizo la damu hazisababishi tatizo kubwa kwa watoto wanaonyonyeshwa. Wanawake wanaweza kutumia vizuizi vya beta kwakati wa kunyonyesha, lakini mtoto anapaswa kuangaliwa mara kwa mara kuona kama kuna madhara, kma vile mapigo ya moyo ya polepole na shinikizo la damu la chini.

Kafeini na theophylline hazina madhara kwa mtoto anayenyonya lakini zinaweza kuwafanywa wawe na harara. Moyo wa mtoto na viwango vya kupumua vinaweza kuongezeka.

Hata kama baadhi ya dawa zinaripotiwa kuwa salama kwa watoto wanaonyonyeshwa, wanawake wanaonyonyesha wanapaswa kupata ushauri wa mtaalamu wa afya kabla ya kutumia dawa yoyote, hata dawa inayotolewa bila agizo la daktari, au dawa inatokana na mimea. Lebo zote za dawa zinapaswa kukaguliwa ili kuona endapo zina onyo dhidi ya kutumia wakati wa kunyonyesha.

Je, Ulijua...

  • Hata kama baadhi ya dawa zinaripotiwa kuwa salama kwa watoto wanaonyonyeshwa, wanawake wanaonyonyesha wanapaswa kupata ushauri wa mtaalamu wa afya kabla ya kutumia dawa yoyote, hata dawa inayotolewa bila agizo la daktari, au dawa inatokana na mimea.

Dawa Ambazo Zinahitaji Uangalizi wa Daktari Wakati wa Kunyonyesha

Baadhi ya dawa zinahitaji usimamizi wa daktari wakati wa kuzitumia. Kuzitumia kwa usalama wakati wa kunyonyesha kunaweza kuhitaji yafuatayo:

  • Kurekebisha dozi

  • Kupuguza urefu wa muda wa kutumia dawa

  • Kukadiria muda wa kutumia dawa kwa kuhusianisha na kunyonyesha

Dawa nyingi za kuzuia wasiwasi, dawa za kupunguza unyongovu, na dawa za kutuliza akili zinahitaji usimamizi wa daktari, ingawa hazina uwezekano wa kusababisha matatizo makubwa kwa mtoto. Hata hivyo, dawa hizi zinabaki mwilini kwa muda mrefu. Katika miezi michache ya mwanzo ya maisha, watoto wachanga wanaweza kuwa na ugumu wa kuondoa dawa hizo na zinaweza kuathiri mfumo wa neva wa mtoto. Kwa mfano, dawa za kupunguza wasiwasi kama diazepam (benzodiazepine) zinaweza kusababisha uchovu, usingizi mwingi, na kupoteza uzito kwa watoto wanaonyonyeshwa. Watoto wanaondoa phenobarbital (dawa ya kuzuia kiharusi na barbiturate) polepole, hivyo dawa hii inaweza kusababisha usingizi kupita kiasi. Kutokana na athari hizi, madaktari hupunguza kipimo cha benzodiazepines na barbiturates na kuwa makini na matumizi yake kwa wanawake wanaonyonyesha.

Warfarin (dawa inayozuia damu isigande) inaweza kutumiwa ikiwa mtoto amefikia muda wake na ni mwenye afya. Warfarin haionekani kuingia kwenye maziwa ya mama. Watu wanaotumia warfarin, ikiwa ni pamoja na wanawake wanaonyonyesha, wanapaswa kufanyiwa vipimo vya damu kila baada ya kipindi ili kuamua endapo damu inaganda kwa kawaida. Warfarin inaweza kusababisha hali ya michubuko au kutokwa damu.

Dawa na Vitu Ambavyo Havipaswi Kutumiwa Wakati wa Kunyonyesha

Baadhi ya dawa na dut nyinginezo hazipaswi kutumiwa na akina mama ambao wananyonyesha. Zinajumuisha

Dawa ambazo zinaweza kuzuia uzalishaji wa maziwa zinajumuisha estrogen, tembe za kupanga uzazi zenye estrogen ya dozi ya juu na progestin, trazodone (dawa ya kupunguza unyongovu), na baadhi ya dawa zinazotumiwa kutibu ugonjwa Parkinson (bromocriptine na levodopa).

Ikiwa wanawake wanaonyonyesha ni lazima watumie dawa ambazo zinaweza kumdhuru mtoto, wanapaswa kusitisha kunyonyesha. Lakini wanaweza kurejea kunyonyesha baada ya kuacha kutumia dawa. Wakati wa kutumia dawa, wanawake wanaweza kudumisha kutoa maziwa kwa kuyavuta, kisha yakatupwa.

Wanawake ambao wananyonyesha wanapaswa kuwasiliana na mtoa huduma wao wa afya kuhusu dawa zote wanazotumia au wanazotaka kuanza kutumia.

Wanawake wanaovuta sigara hawapaswi kunyonyesha ndani ya saa 2 za kuvuta sigara na hawapaswi kuvta sigara mbele ya mtoto wao iwe ananyonya au la. Kuvuta sigara kunapunguza uzalishaji wa maziwa na kunaingiliana na halia ya kawaida ya mtoto kuongezeka uzito.

Pombe ikitumiwa kwa viwango vikubwa inaweza kumfanya mtoto kwenye mwenye usingizi na kusababisha kutoka jasho jingi. Urefu wa mtoto huenda usiongezeke kwa kawaida, na mtoto anaweza kupata uzito ulipitiliza. Kunywa hadi kinywaji 1 cha kawaida kwa siku hakuonekani kumdhuru mtoto anayenyonya, hasa ikiwa mwanamke anasubiri angalau saa 2 baada ya kinywaji kimoja kabla ya kunyonyesha.