Uchungu wa uzazi

NaJulie S. Moldenhauer, MD, Children's Hospital of Philadelphia
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024 | Imebadilishwa Apr 2024
v810504_sw

Uchungu wa uzazi ni mfululizo wa mikazo wa mapigo na unaoendelea wa mji wa mimba ambayo inahamisha taratibu mji wa mimba hadi kwenda kwenye sehemu ya chini ya mji wa mimba (shingo ya kizazi) na mfereji wa uzazi (uke).

(Angalia pia Muhtasari wa Uchungu wa Uzazi na Kujifungua.)

Uchungu wa uzazi hutokea katika hatua kuu tatu:

  • Hatua ya kwanza: Hatua hii (ambayo ina awamu mbili: tuli na amilifu) kwa kawaida ni hatua ndefu zaidi. Uchungu wa uzazi unaanza rasmi wakati ambapo kuna mikazo mikubwa na ya mara kwa mara ya mji wa mimba ambayo inasababisha shingo ya kizazi kufunguka taratibu (kupanuka) na kunywea na kurudi nyuma hadi inatanuka kabisa na mtoto anaweza kupita kwenye uke.

  • Hatua ya pili: Mama anasukuma na mtoto anatoka.

  • Hatua ya tatu: Kondo la nyuma (kiungo abacho kinakuwa ndani ya mji wa mimba ili kutoa oksijeni na virutubishi kwa mtoto) linatolewa. Hatua hii pia inaitwa "baada ya kujifungua."

Uchungu wa uzazi kwa kawaida unaanza ndani ya wiki 2 (kabla au baada) za tarehe ya kujifungua iliyokadiriwa. Kile hasa kinachosababisha uchungu kuanza hakijulikani. Kuelekea mwisho wa ujauzito (baada ya wiki 37) daktari anachunguza shingo ya kizazi ili kujaribu kutabiri ni lini uchungu utaanza.

Kwa wastani, uchungu wa zuzazi unadumu saa 12 hadi 18 kwa ujauzito wa kwanza na huwa unakuwa mfupi, kwa wastani wa saa 6 hadi 8, kwa ujauzito unaofuata. Kusimama na kutembea wakati wa hatua ya kwanza ya uchungu wa uzazi kunaweza kusaidia kusimamia maumivu na kunaweza kufupisha uchungu wa uzazi kwa zaidi ya saa 1.

Awamu za Leba

HATUA YA KWANZA

Kuanzia mwanzo wa uchungu wa kujifungua hadi kufunguka kikamilifu (kutanuka) kwa shingo ya kizazi, kwa karibu sentimita 10.

Awamu ya Awali (Tuli)

  1. Mikazo inatokea bila utaratibu mwanzoni lakini inaendelea kuwa imara na yenye mapigo zaidi.

  2. Usumbufu ni mdogo lakini unaweza kuongezeka kadiri muda unavyosonga.

  3. Shingo ya kizazi inaanza kuwa nyembamba na kutanuka kwa karibu sentimita 4 hadi 5.

  4. Awamu ya awali inadumu kwa wastani wa saa 8 (kwa kawaida zaidi ya saa 20) katika ujauzito wa kwanza na saa 5 (kwa kawaida si zaidi ya saa 14) kwenye ujauzito unaofuata.

Awamu Amilifu

  1. Shingo ya kizazi inatanuka kutoka sentimita 4 hadi sentimita 10 kamili. Inanywewa na kuvuta nyuma hadi inaungana na sehemu nyingine ya mji wa mimba.

  2. Sehemu inayowasilishwa ya mtoto (sehamu ya mtoto ambayo inatoka kwanza), kwa kawaida ni kichwa, inaanza kushuka kwenye njia ya uzazi ya mwanamke.

  3. Mwanamke anaanza kuhisi hali ya kusukuma kadiri mtoto anavyoshuka, lakini anapaswa kusubiri hadi shingo ya kizazi itanuke kabisa. Kusukuma mapema zaidi kunaweza kuchoshe isivyo lazima na kunaweza kuchana shingo ya kizazi.

  4. Awamu hii inadumu kwa wastani wa saa 5 hadi 7 kwenye ujauzito wa kwanza na saa 2 hadi 4 kwenye ujauzito unaofuata.

HATUA YA PILI

Kuanzia kufungua kikamilifu shingo ya kizazi hadi kujifungua mtoto: Hatua hii kwa kawaida inadumu kwa karibu saa 2 kwenye ujauzito wa kwanza na karibu saa 1 kwenye ujauzito unaofuata. Inaweza kudumu kwa saa moja nyingine au zaidi ikiwa mwanamke huyo amepewa sindano za maumivu mgongoni ili kupoza maumivu. Wakati wa hatua hii, mwanamke anasukuma.

HATUA YA TATU

Kutoka kujifungua mtoto hadi kutoa kondo la nyuma: Hatua hii kwa kawaida inadumu kwa dakika chache tu lakini inaweza kudumu hadi dakika 30.

Mwanzo uchungu wa uzazi

Uchungu wa kujifungua kwa kawaida huwa unaanza na

  • Mikazo katika tumbo la chini kwa mwachano wenye mpangilio

  • Wakati mwingine maumivu

Mwanamke ambaye amezaa harakaharaka anapaswa kutaarifu daktari wake mapema anapofikiri kwamba anakwenda kupata uchungu wa kujifungua. Mikazo katika tumbo la chini inapoanza kwanza, inaweza kuwa dhaifu na yenye mwachano wa mbali. Inaweza kuonekana kama mikazo ya hedhi. Kadiri muda unapopita, mikazo ya mji wa mimba inakuwa mirefu, thabiti na ya karibu. Mikazo na maumivu ya mgongo inaweza kutanguliwa au kuambatana na ishara nyingine za uchungu wa kujifungua, kama zifuatazo:

  • Onyesho la damu: Kiasi kidogo cha damu kikiwa kimechanganywa na ute ("kupistisha plagi ya ute") kutoka kwenye uke inaweza kuwa ishara ya awali kwamba uchungu wa kujifungua unakaribia kuanza. Hata hivyo, mwonekano wa damu unaweza pia kutokea kama matokeo ya kufanya ngono. Mwonekano wa damu unaweza kutokea mapema saa 72 kabla ya mikazo kuanza. Wanawake wajawazito wanapaswa kuwasiliana na watoa huduma wao wa afya ikiwa uvujaji wowote wa damu kwenye uke unatokea, kwa sababu ya tathmini kwenye ofisi ya daktari au hospitali inaweza kuhitajika.

  • Kupasuka kwa utando: Kwa kawaida, utando uliojaa majimaji ambo una kijusi (kifuko cha uterasi) unapasuka wakati wa uchungu wa kujifungua na maji ya amnioti yanatiririka kupitia kwenye uke. Tukio hili kwa kawaida linaelezea kama "maji yanapasuka." Mara nyingine, utando unapasuka kabla ya uchungu wa kuzaa haujaanza. Kupasuka kwa utando kabla ya uchungu wa kujifungua haujaanza huitwa kupasuka kwa utando kabla ya uhungu wa kujifungua. Baadhi ya wanawake wanahisi kutoka kwa majimaji kwenye uke, ikifuatiwa na uvujaji endelevu. Wakati mwingine ni vigumu kujua ikiwa majimaji yanayovuja ni maji ya amnioti, mkojo, au ute wa uke.

Ikiwa utando wa mwanamke unapasuka, anapaswa kuwasiliana na daktari wake au mkunga haraka sana. Karibu asilimia 80 hadi 90 ya wanawake ambao utando wao unapasuka siku ya kujifungua au karibu na siku ya kujifungua wanapata uchungu wakati huohuo ndani ya saa 24. Ikiwa uchugu wa kujifungua haujaanza baada ya saa kadhaa na mtoto amekaribia, wanawake kwa kawaida wanapelekwa hospialini, ambapo wanapewa dawa ya kuanzisha uchungu (kuanzishiwa uchungu) ili kupunguza hatari ya maambukizi. Baada ya utando kupasuka, bakteria kutoka kwenye uke wanaweza kuingia kwenye mji wa mimba kwa urahisi zaidi na kusababisha maambukizi kwa mwanamke, kijusi au wote wawili.

Baada ya mwanamke aliyepasuka utando kabla ya kupata uchungu wa kujifungua anapelekwa kwenye kituo cha kujifungulia, oksitosini (mbayo inasababisha mji wa mimba kukaza) au dawa kama hiyo, kama vile prostagladini, inatumiwa kuweka uchungu wa uzazi. Hata hivyo, ikiwa utando unapasuka kwa zaidi ya wiki 6 kabla ya tarehe ya kujifungua (kabla ya kipindi au kabla ya wiki ya 34), madaktari kwa kawaida hawaanzishi uchungu hadi kijusi kiwe kimekomaa zaidi.

Kulazwa kwenye hospitali au kituo cha kujifungua

Mwanamke anapaswa kumpigia mtoa huduma wake wa afya ili kuona endapo anapaswa kwenda hospitalini au kwenye kituo cha kujifungulia pale ambapo moja ya haya yafuatayo yanatokea:

  • Kupasuka kwa utando ("kupasuka kwa maji").

  • Kwa saa 1, kukaza kunadumu kwa angalau sekunde 30 na hutokea mara kwa mara katika mwachano wa karibu dakika 6 au pungufu.

Kwenye kituo, mtaalamu wa huduma za afya atamwangalia mama huyo na kijusi. Ikiwa mwanamke mjamzito yupo katika uchungu wa kujifungua au utando wake umepasuka, mwanamke huyo anapelekwa kwenye kitengo cha uchungu wa kujifungua na kujifungua. Ikiwa daktari au mkunga hana uhakika endapo uchungu wa kujifungua umeanza, mwanamke huyo kwa kawaida anaangaliwa na kijusi kinafuatiliwa kwa saa moja hivi. Ikiwa uchungu haujathibitishwa wakati huo, anaweza kupelekwa nyumbani.

Mwanamke anapopelekwa kwenye kitengo cha uchungu na kujifungua, dalili zake muhimu zinapimwa na damu inatolewa kwa ajili ya uchunguzi.

Uwepo na sauti ya mapigo ya moyo ya kijusi yanarekodiwa na uchunguzi wa kimwili unafanywa. Tumbo la mwanamke linachunguzwa ili kukadiria kijusi ni kikubwa kiasi gani, endapo kijusi kinatazama nyuma au mbele (mkao) na iwapo kichwa, uso, matako au mabega yanaongoza njia kwenda nje (mwonekano). Wakati mwingine Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti hufanywa.

Mkao na mwonekano wa kijusi huathiri jinsi kijusi kinavyopita kwenye uke. Muunganiko uliozoeleka sana na ulio salama kabisa unajumuisha yafuatayo:

  • Kichwa kwanza

  • Kutazama nyuma (kutazama chini mwanamke anapolala kwa mgongo wake)

  • Shingo kuinama mbele

  • Kidevu kikita chini

Kichwa kwanza huitwa mwonekano wa kilele au sefaliki. Wakati wa wiki moja au mbili zilizopita kabla ya kujifungua, vijusi wengi hugeuka nyuma ya kichwa kunaonekana kwanza. Mkao au mwonekano usio wa kawaida, kama vile matako kwanza, au mabega kwanza au kijusi kinatazama mbele, hufanya kujifungua kuwa vigumu sana kwa mama, mtoto na daktari. Kujifungua kwa njia ya upasuaji kunapendekezwa.

Uchunguzi wa uke kwa kutumia spekulamu unaweza kufanywa ili kubaini endapo utando umepasuka. (Spekulamu ni kifaa cha metali au plastiki kinachotenga ukuta wa uke). Rangi ya maji ya amnioti inabainishwa. Majimaji hayo yanapaswa kuwa meupe yasiyokuwa na harufu. Ikiwa utando unapasuka na majimaji ya maji ya amnioti ni ya kijani, matokeo ya uondoaji rangi kutoka kwenye kinyesi cha kwanza cha kijusi (mekoni ya kijusi).

Kisha daktari au mkunga anachunguza shingo ya kizazi kwa vidole vyake ili kubaini shingo ya kizazi imetanuka (inaangaliwa kwa sentimita) na imevutwa nyuma kwa kiasi gani (inaangaliwa kwa asilimia au kwa sentimita). Uchunguzi huu unaweza kuondolewa ikiwa mwanamke huyo anavuja damu au ikiwa kuta zimepasuka zenyewe.

Ikiwa kuna wasiwasi kuhusu matatizo baada ya uchunguzi wa awali, ufuatiliaji wa kijusi na vipimo vya maabara, upimaji wa ziada au ufuatiliaji unafanywa.

Bomba la mshipani kwa kawaida linaingizwa kwenye mkono wa mwanamke wakati wa uchungu wa kujifungua kwenye hospitali. Bomba hili linatumika kupatia mwanamke majimaji ili kuzuia kupungukiwa maji na ikiwa inahitajika, kutoa dawa.

Vimiminika vinapotolewa kwa njia ya mishipa, mwanamke huyo hahitaji kula au kunuwa wakati wa uchungu wa kujifungua, ingawa anaweza kuchagua kunywa baadhi ya vimiminika na kula baadhi ya vyakula rahisi mapema wakati wa uchungu wa kujifungua. Tumbo lisilo na chakula wakati wa kujifungua hufanya mwanamke asiwe na uwezekano wa kutapika. Kwa nadra sana, matapishi yanavutwa kwenye hewa, kwa kawaida baada ya nusukaputi ya jumla ambayo inaweza kusababisha nimonia kali.

Mkao wa Kawaida na Uwasilishaji wa Kijusi

Kuelekea mwisho wa ujauzito, kijusi kinahama kuelekea kwenye mkao wa kujifungua. Kwa kawaida, mkao wa kijusi unatazama nyuma (kuelekea mgongo wa mwanamke) huku uso na mwili ukiwa upande mmoja na shingo likiwa linanyumbuka, na mwonekano ni kichwa kwanza.