Ugonjwa wa haiba ya utegemezi ni hali ya afya ya akili ambayo ina sifa ya hitaji la kupita kiasi la kutunzwa wengine, na husababisha kujitiisha na tabia za kuwaning'ing'inia watu wengine.
Watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi hawafikirii kwamba wanaweza kujitunza wenyewe na hutumia tabia ya kunyenyekea kujaribu kuwafanya watu wengine wawatunze.
Madaktari hutambua ugonjwa wa haiba ya utegemezi kulingana na dalili maalum, ikiwa ni pamoja na hitaji la mtu kutunzwa na hofu ya kulazimika kujitunza mwenyewe.
Tiba ya kisaikolojia inayolenga kuchunguza hofu ya kujitegemea inaweza kusaidia.
Ugonjwa wa haiba ni hali za afya ya akili zinazohusisha mifumo ya muda mrefu na iliyoenea ya kufikiri, kutambua, kuguswa, na kuhusisha ambayo humsababishia mtu dhiki kubwa na/au kudhoofisha uwezo wa mtu kufanya kazi.
Watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi hutaka kuhudumiwa na huwa na wasiwasi mkubwa sana kuhusu suala la kujihudumia. Ili kupata huduma wanayotaka, wako tayari kusalimisha uhuru wao na maslahi yao. Kwa hivyo wanakuwa tegemezi na watiifu kupita kiasi.
Ugonjwa wa haiba ya utegemezi hutokea kwa chini ya 1% ya watu nchini Marekani. Imegunduliwa mara nyingi zaidi kwa wanawake, lakini baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa huathiri jinsia zote mbili kwa usawa.
Matatizo mengine huwepo mara nyingi pia. Mara nyingi watu pia wana moja au zaidi ya yafuatayo:
Tatizo la unyogovu kama vile tatizo kubwa la unyogovu au ugonjwa wa unyogovu unaoendelea
Ugonjwa mwingine wa utu (kama vile borderline au ugonjwa wa hisia zisizo thabiti)
Sababu za Ugonjwa wa Haiba ya Utegemezi
Taarifa kuhusu kinachosababisha ugonjwa wa haiba ya utegemezi ni chache. Sababu zinazoweza kuchangia zinajumuisha
Hali za kitamaduni
Uzoefu hasi wa awali
Tabia ya kuzaliwa nayo ya kuwa na wasiwasi
Sifa zinazojitokeza katika familia (kama vile utiifu, kutojiamini, na tabia ya kujidharau)
Dalili za Ugonjwa wa Haiba ya Utegemezi
Haja ya kutunzwa
Watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi hawafikirii kwamba wanaweza kujitunza wenyewe. Wanatumia tabia ya utiifu kujaribu kuwafanya wengine wawatunze.
Watu wenye ugonjwa huu kwa kawaida huhitaji uhakikisho mwingi na ushauri mwingi wanapofanya maamuzi ya kawaida. Mara nyingi huwaruhusu wengine, mara nyingi mtu mmoja, kuwajibikia vipengele vingi vya maisha yao. Kwa mfano, wanaweza kumtegemea mwenzi wao kuwaambia nini cha kuvaa, ni aina gani ya kazi ya kutafuta, na ni nani wa kushirikiana naye.
Watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi huwa wanaingiliana kijamii na watu wachache tu ambao huwategemea. Uhusiano wa karibu unapoisha, watu wenye tatizo hili hujaribu mara moja kutafuta uhusiano mbadala. Kwa sababu ya hamu yao ya kutamani kutunzwa, huenda wasibague katika kuchagua uhusuano huo mbadala.
Watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi wana hofu kubwa kupita kiasi ya kuachwa na wale ambao wao huwategemea, hata kama hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Kunyenyekea kupindukia
Kwa sababu watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi wanaogopa kupoteza usaidizi au idhini, wanaona ugumu kueleza kutokubaliana na wengine. Wanaweza kukubali jambo wanalojua ni kosa kuliko kuhatarisha uwezo wa kupata msaada kutoka kwa wengine. Hata wakati kukasirika kunafaa, hawawakasirikii marafiki na wafanyakazi wenzao kwani wanaogopa kupoteza usaidizi wao.
Watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi hufanya kila wawezalo kupata huduma na usaidizi. Kwa mfano, wanaweza kufanya kazi zisizopendeza, kujisalimisha kwa madai yasiyo ya sababu, na hata kuvumilia unyanyasaji wa kimwili, kingono, au kihisia. Kuwa peke yao huwafanya wahisi wasiwasi au hofu kubwa kwa sababu wanaogopa kwamba hawawezi kujitunza.
Kutokuwa na imani
Watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi hujiona kuwa duni na huwa wanadharau uwezo wao. Wanatafsiri ukosoaji wowote au kutoridhika kama uthibitisho wa kutokuwa na uwezo kwao, na hivyo kudhoofisha zaidi kujiamini kwao.
Kutokuwa na uhuru
Kwa sababu watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi wana uhakika kwamba hawawezi kufanya chochote peke yao, wanapata shida kuanza jukumu jipya na kufanya kazi kwa kujitegemea. Wanaepuka kazi zinazohitaji uwajibikaji. Wanajionyesha kuwa hawana uwezo na kwamba wanahitaji msaada na uhakikisho wa kila mara. Wanapohakikishiwa kwamba mtu mwenye uwezo anawasimamia na kuwaridhia, watu wenye ugonjwa wa haiba ya utegemezi huwa wanafanya kazi ipasavyo. Hata hivyo, hawataki kuonekana kuwa na uwezo kupita kiasi ili wasije wakaachwa. Matokeo yake, taaluma yao inaweza kuathiriwa vibaya. Wanadumisha utegemezi wao kwa sababu wanaepuka kujifunza stadi za maisha ya kujitegemea.
Utambuzi wa Matibabu ya Ugonjwa wa Utu tegemezi
Tathmini ya daktari, kulingana na vigezo vya kawaida vya uchunguzi wa magonjwa ya akili
Kwa kawaida madaktari hugundua ugonjwa wa haiba kulingana na vigezo vilivyopo katika Mwongozo wa Utambuzi na Takwimu wa Matatizo ya Akili, toleo la 5, Marekebisho ya Maandishi (DSM-5-TR), marejeleo ya kawaida ya utambuzi wa magonjwa ya akili kutoka American Psychiatric Association.
Ili madaktari waweze kugundua ugonjwa wa haiba ya utegemezi, watu lazima wawe na hitaji la kudumu na la kupita kiasi la kutunzwa, linalosababisha utiifu na tabia ya kung'ang'ania, kama inavyoonyeshwa na angalau 5 kati ya yafuatayo:
Wanapata shida kufanya maamuzi ya kila siku bila kupata kiasi kikubwa kupita kiasi cha ushauri na hakikisho kutoka kwa watu wengine.
Wanataka watu wengine wawajibike kwa mambo muhimu ya maisha yao.
Wanapata shida kuonyesha kutokubaliana na wengine kwa sababu wanaogopa kupoteza usaidizi au kukubaliwa na wengine.
Wanapata shida kuanzisha miradi peke yao kwa sababu hawajiamini katika uamuzi wao na/au uwezo wao (si kwa sababu hawana motisha au nguvu).
Wako tayari kujitahidi sana (kwa mfano, kufanya kazi zisizopendeza) ili kupata msaada kutoka kwa wengine.
Wao huhisi wasiwasi au kuwa hawana uwezo wanapokuwa peke yao kwa sababu wanaogopa kwamba hawawezi kujitunza.
Wakati uhusiano wa karibu unapoisha, wao huhisi hitaji la haraka la kuanzisha uhusiano mpya na mtu ambaye atatoa utunzaji na usaidizi.
Wanasumbuliwa na hofu ya kuachwa wajitunze wenyewe.
Pia, ni lazima dalili lazima ziwe zimeanza mapema katika utu uzima wa mapema.
Matibabu ya Ugonjwa wa Utu Tegemez
Tiba ya tabia-tambuzi
Tiba ya akili kwa mazungumzo
Kanuni za jumla za matibabu ya ugonjwa wa utu tegemezi zinafanana na zile za matatizo yote ya utu.
Tiba ya kisaikolojia ya kisaikodinamiki na tiba ya utambuzi natabia zinazozingatia kuchunguza hofu ya kujitegemea na matatizo ya kujithibitisha zinaweza kuwasaidia watu wenye ugonjwa wa utu tegemezi.
Haijulikani iwapo dawa zina manufaa. Wakati mwingine, dawa za kupunguza mfadhaiko, kama vile vizuizi teule vya ufyonzaji upya wa serotonini (SSRIs), zinaweza kutumika kutibu mfadhaiko na wasiwasi.