Dharura za Shinikizo la Juu la Damu kwa Watoto

(Shinikizo la Damu Kali la Mara Moja)

NaMichael A. Ferguson, MD, Harvard Medical School
Imekaguliwa naMichael SD Agus, MD, Harvard Medical School
Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2025 | Imebadilishwa Jul 2025
v53580278_sw

Dharura ya shinikizo la juu la damu linakuwa baya kabisa, aina ya ghafula ya shinikizo la juu la damu ambalo linaweza kudhuru kiungo muhimu kimoja au zaidi.

(Angalia pia Shinikizo la Juu la Damu kwa Watoto na Shinikizo la Juu la Damu kwa watu wazima.)

  • Dharura za shinikizo la juu la damu hutokea pale ambapo shinikizo la damu linaongezeka kwa haraka.

  • Kwa watoto, dalili ya kwanza ya dharura ya shinikizo la juu la damu ni hasa maumivu ya kichwa, utepetevu, ukanganyikiw na mishtuko na kwa watoto wachanga, harara.

  • Madaktari wanatambua dharura ya shinikizo la juu la damu kwa kupima shinikizo la damu na kufanya vipimo kujua madhara kwenye ubongo, moyo na figo (elektrokadiografia, elektrokadiografia, uchanganuzi wa CT wa ubongo au MRI na vipimo vya damu na mkojo).

  • Matibabu ya dharura za shinikizo la juu la damu huhusisha kuwapeleka watoto kwenye kitengo cha uangalizi wa kina na kuwapa dawa kwa njia ya mishipa ili kushusha shinikizo la damu mapema kadiri iwezekanavyo.

Wakati shinikizo la damu linachunguzwa, thamani 2 zinarekodiwa. Namba ya juu inaakisi shinikizo la juu zaidi kwenye atari, ambalo linafikiwa moyo unakaza (wakati wa sistoli). Namba ya chini inaakisi shinikizo la chini zaidi kwenye atri, ambalo linafikiwa kabla ya moyo haujaanza kukazi tena (wakati wa diastoli). Shinikizo la damu huandikwa kama shinikizo la sistoli/shinikizo la diastoli—kwa mfano, mm Hg 120/80 (milimita za zebaki), inayorejelewa kama 120 juu ya 80.

Shinikizo la juu la damu linakuwa baya zaidi, aina ya ghafula ya shinikizo la juu la damu. Shinikizo la damu linaweza kuwa pointi 30 au juu zaidi kuliko kile kinachohitajika kutambua shinikizo la juu la damu na kuna ushahidi wa madhara yanayoendelea kwenye kiungo muhimu kimoja au zaidi (hasa ubongo, moyo, macho na figo). Watoto wanaweza kuwa na aina mbalimbali za dalili.

Dharurua za shinikizo la juu la damu ni nadra sana kwa watoto. Zinaweza kutokea kwa watoto ambao hapo awali wamegunduliwa au hawajagunduliwa kuwa na shinikizo la juu la damu.

Dharura za shinikizo la juu la damu kwa kawaida hutokea wakati ambapo shinikizo la damu huongezeka kwa haraka. Kinachosababisha ongezeko la haraka hutofautiana kulingana na umri. Sababu za kawaida pamoja na:

Dharura ya shinikizo la juu la damu, ikiwa haitatibiwa kwa haraka, kwa kawaida husababisha madhara endelevu kwenye kiungo muhimu kimoja au zaidi, hasa vifuatavyo:

  • Ubongo, ambao unaweza kusababisha kuzorota kwa utendajikazi wa ubongo, mshituko na/au kiharusi

  • Moyo, ambayo inaweza kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi

  • Macho, ambayo yanaweza kusababisha papilledema (kuvimba kwa neva za macho) na kuvuja damu kwenye retina

  • Figo ambazo zinaweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi

Ikiwa haitatibiwa, dharura ya shinikizo la damu inaweza kusababisha kifo.

Dharura ya shinikizo la juu la damu ni shinikizo la juu la damu baya ambalo bado halijasababisha uharibifu wa kutosha wa viungo kuweza kusababisha dalili.

Kwa pamoja dharura za shinikizo la juu la damu zinaitwa shinikizo kali sana la juu la damu.

Dalili za Dharura ya Shinikizo la Juu la Damu kwa Watoto

Shinikizo la damu liko juu sana, hasa katika hatua ya 2 (kali) kiwango cha shinikizo la juu la damu au juu zaidi (140/90 au juu zaidi).

Watoto wenye shinikizo kali la juu la damu wanaweza wasiwe na dalili zozote au wanaweza kuwa na dalili mbaya. Dalili zinaweza kuhusiana na umri wa mtoto. Kwa watoto wachanga na watoto wadogo, dalili za kwanza za dharura za shinikizo la juu la damu zinaweza zisiwe mahususi ikiwa ni pamoja na harara, lishe duni au ukuaji mbovu au kutoongezeka uzito. Watoto wadogo wanweza kuwa pia na badiliko la ufahamu au vifafa. Watoto wakubwa wanaweza kuwa na maumivu ya kichwa, mabadiliko ya uoni, kizunguzungu, utepetevu (uchovu) au kichefuchefu na kutapika.

Watoto wanaweza kuwa na mapigo ya haraka ya moyo, maumivu ya kifua, kukosa pumzi na/a vifundo vilivyovimba. Watoto wanaweza kupata kiharusi.

Watoto wote wenye dharura ya shinikizo la juu la damu wana ushahidi wa madhara kwenye kiungo cha mwili. Kwa watoto wenye dharura ya shinikizo la juu la damu, madhara kwenye kiungo huenda yasiwepo.

Utambuzi wa Dharura ya Shinikizo la Juu la Damu kwa Watoto

  • Upimaji wa shinikizo la damu

  • Vipimo vya kutathmini uharibifu wa viungo

Wakati wa kushuku dharura ya shinikizo la juu la damu, madaktari wanaweza kutumia oscillometer kupima shinikizo la damu badala ya kutumia stethoscope. Oscillometer inarekodi shinikizo la damu kiotomatiki na kwa haraka, hali inayosaidia kupata kipimo kinachohitajika (kila baada ya dakika 2 hadi 3). Shinikizo la damu linapimwa tena kwa kutumia sphygmomanometer na stethoscope ili kuthibitisha upimaji. Inapowezekana, madaktari wanafanya ufuatiliaji wa shinikizo la damu ndani ya ateri, hali inayojumuisha kuweka neli ndogo ya plastiki ndani ya ateri na kuiunganisha na kifuatiliaji cha shinikizo la damu. Vifuatiliaji hivi vya shinikizo la damu kwenye atari hupima shinikizo la damu kwa kuendelea na pia viko sahihi zaidi kuliko vifaa vingine.

Madaktari manachukua historia ya matibabu, ambayo inajumuisha maswali kuhusu dalili za sasa za mtoto, tatizo lolote alilonalo mtoto na dawa zozote ambazo mtoto anatumia.

Uchunguzi wa kina wa kimwili na vipimo vya kawaida vya damu na mkojo hufanywa.

Vipimo pia vinafanywa ili kuamua iwapo vungo muhimu vimeharibiwa na, ikiwa ndivyo, kuna madhara kiasi gani. Vipimo hujumuisha:

  • Elektrokadiografia (ECG), eksirei ya kifua, na ikiwa inawezekana, ekokadiografia ili kuangalia matatizo ya moyo

  • Kipima mkojo ili kuangalia matatizo ya figo

  • Vipimo vya damu ili kuangalia uharibifu kwenye figo au matatizo ya homoni

  • Hesbu kamili ya chembe za damu ili kuangalia idadi seli za dambu zisizo za kawaida, hasa chembe sahani (ambazo husaidia kuganda kwa damu)

  • Tomografia ya kompyuta (CT) au upigaji picha kwa mwangwi wa sumaku (MRI) wa kichwa ili kuangalia uvimbe au kuvuja damu kwenye ubongo na kuondoa sababu nyingine yoyote ya dalili zinazohusiana na ubongo

  • Dawa na vipimo vya dawa kwa watoto walio katika umri wa balehe

Ikiwa shinikizo la juu la damu halikutambuliwa hapo awali au kutathminiwa, kipimo kingine ili kubaini sababu ya shinikizo la juu la damu kinaweza kufanywa baadaye.

Matibabu ya Dharura ya Shinikizo la Juu la Damu kwa Watoto

  • Kwa dharura za shinikizo la juu la damu, kulazwa kwenye kitengo cha uangalizi maalumu na kupewa dawa kwa njia ya mshipa ili kupunguza shinikizo la damu.

  • Kwa dahrura za shinikizo la juu la damu, kupelekwa kwenye kitengo cha dharura au hospitalini na dawa kwa njia ya kinywa ili kushusha shinikizo la damu (mara chache dawa kwa njia ya mshipa zinahitajika)

Watoto wenye dharura ya shinikizo la juu la damu wanapelekwa haraka kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU) au, endapo ICU haipo, kwenye idara ya dharura, ili kwamba aweze kutibiwa haraka na kutathminiwa na kufuatiliwa kwa karibu. Hapo, dawa za kushusha shinikizo la damu (dawa za kupunguza shinikizo la damu) zinaweza kutolewa kwa njia ya mishipa haraka kadiri iwezekanavyo.

Lengo la matibabu ya dharura ya shinikizo la juu la damu ni kushusha shinikizo la damu kutosha kuondoa hatari za dalili za kuhatarisha maisha na kuzuia zaidi uharibifu zaidi wa viungo muhimu. Madaktari wanahakikisha kwamba shinikizo la damu halishushiwa haraka sana, hali ambayo pia inaweza kusababisha mtiririko wa damu hafifu kwenda kwenye ubongo na figo.

Kwa dharura za shinikizo la juu la damu, dawa za kutolewa kwa njia ya mshipa zinazopendelewa ni labetalol na nicardipine.

Endapo dawa inayopendelewa haiwezi kutumia wau haiwezi kufanya kazi, sodiamu nitroprusside, hydralazine, na esmolol ni dawa nyingine zinazotolewa kwa njia ya mshipa zinazoweza kutumia.

Mara baada ya shinikizo la damu kushushwa, madaktari wanaweza kuwapa watoto dawa kwa mdomo.

Watoto wenye uharaka wa shinikizo la juu la damu (shinikizo la juu la damu baya lakini halina dalili lakini hakuna matatizo ya viungo) pia wanapelekwa hospitalini au kwenye idara ya dharura na wanatathmiiwa haraka, lakini shinikizo la damu halihitaji kushushwa haraka kama kwa dharura ya shinikizo la juu la damu. Watoto hawa kwa kawaida wanapewa dawa kwa mdomo. Mara nyingine, dawa zinazotolewa kwa njia ya mshipa zinahitajika.

Kwa uharaka wa shinikizo la damu la juu, clonidine, hydralazine, isradipine, au minoxidil hutolewa kwa mdomo. Wakati mwingine dawa zinazotolewa kwa njia ya mshipa zinatumiwa ama kwa mbadala wa dawa zinazotolewa kwa mdomo au sambamba na hizo.

Inapowezekana, watoto wenye tatizo moja wapo wanapaswa kutibiwa na daktari au daktari bingwa mwenye uzoefu wa kusimamia shinikizo kali la juu la damu kwa watoto.

Jedwali
Jedwali
Jedwali
Jedwali