Kyphosisi

NaNora E. Renthal, MD, PhD, Harvard Medical School
Imekaguliwa naMichael SD Agus, MD, Harvard Medical School
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Sept 2025
v38720749_sw

Kifosisi ni kupinda kusiko kwa kawaida kwa uti wa mgongo kunakosababisha mgongo kuwa na nundu.

Sehemu ya juu ya mgongo kwa kawaida unapinda kuelekea mbele kwa kiasi fulani. Baadhi ya watoto wana kiwango kikubwa cha kupinda. Kupinda kulikozidi kunaweza kuwa

  • Jongevu

  • Usiojongevu (kimuundo)

Katika kifosisi jongevu, watoto wanaweza kunyoosha uti wa mgongo kwa kufanya misuli yao kuwa myepesi na pingili za mgongo ziko katika hali ya kawaida. Kisababishaji hakijulikani. Mazoezi ya kuimarisha misuli yanaweza kusaidia, lakini hakuna matibabu mengine mahususi yanayohitajika.

Kwenye kifosisi isiyojongevu, watoto hawawezi kunyoosha uti wa mgongo kwa sababu pingili kadhaa za mgongo kwenye sehemu ya juu ya mgongo zina umbo la kabari badala ya mstatili. Kwa kawaida, pingili 3 au zaidi zinahusishwa. Mara chache, watoto wachanga wanazaliwa na kifosisi isiyojongevu, lakini inatokea sana baadaye kwenye maisha kwa kawaida katika umri wa balehe. Kuna sababu nyingi za nadra, ikiwa ni pamoja na mivunjiko na saratani, lakini chanzo kikubwa zaidi ni ugonjwa wa Scheuermann.

Mara nyingi kifosisi haionyeshi dalili. Wakati mwingine maumivu madogo ya mgongo yasiyokoma yanatokea. Kifosisi inaweza kuonekana kwa sababu tu inabadilisha mwonekano wa mwili. Mabega yanaweza kuonekana ya mviringo. Uti wa mgongo wa juu unaweza kuonekana umepinda zaidi kuliko kawaida au nundu inaweza kuonekana. Baadhi ya watu wana mwonekano sawa na ule wa ugonjwa wa Marfan, ambao miguu na mikono ni mirefu zaidi kuliko kiwiliwili.

Kifosisi ndogo ambayo haisababishi dalili wakati mwigine inagundulika tu wakati wa uchunguzi wa kimwili wa kawaida. Daktari anaweza kuthibitisha utambuzi wa ugonjwa wa kifosisi kwa kufanya eksrei ya uti wa mgongo.

Matibabu ya kifosisi ni sawa na yale ya ugonjwa wa Scheuermann.

Kyphosis: Kibyongo

Ugonjwa wa Scheuermann

(Ugonjwa wa Scheuermann)

Ugonjwa wa Scheuermann ni ugonjwa unaojulikana sana wa aina ya kifosisi isiyojongevu. Kwa kawaida unaanza katika umri wa balehe, ukiathiri kidogo wavulana zaidi kuliko wasichana. Chanzo cha ugonjwa wa Scheuermann hakijulikani, lakini wakati mwingine upo kwenye familia. Skoliosisi, mwinuko wa pembeni wa uti wa mgongo, pia mara nyingi hutokea kwa watoto wenye kifosisi (huitwa kifoskoliosisi).

Ugonjwa wa Scheuermann ni osteokondrosisi. Osteochondrosis ni tatizo la viungo vya ndani maeneo ya ukuaji wa mifupa hilo hutokea wakati mtoto anakua kwa kasi.

Watoto wengi wenye ugonjwa wa Scheuermann wana mgongowa juu wenye mviringo au mkao wa kupinda na wanaweza kuwa na maumivu madogo au makali ya mgongo. Watoto wanaweza kuwa na mikono na miguu mirefu isiyowiana na kiwiliwili chao, sawa na watoto ambao wana ugonjwa wa Marfan. Hali ya kupinda ya kawaida ya sehemu ya juu ya mgongo inaweza pia kuonekana kuliko kawaida, ama kupitia uti wa mgongo wa juu au katika eneo mahususi. Kifosisi mbaya huenda ikasababisha kutojisikia vizuri na wakati mwingine kunaweza kuzuia mjongeo wa kifua, kusababisha ugonjwa wa mapafu kubana.

Ugonjwa wa Scheuermann unaweza kuguduliwa shuleni wakati wa uchunguzi wa kawaida wa matatizo ya uti wa mgongo. Madaktari wanathibitosha utambuzi wa ugonjwa wa Scheuermann kwa kufanya eksirei ya uti wa mgongo. Wakati mwingine MRI au tomografia ya kompyuta (CT) hufanyika.

Matibabu ya Ugonjwa wa Scheuermann

  • Kupunguza kubaba uzito au shughuli ngumu

  • Wakati mwingine ufungaji wa uti wa mgongo

  • Upasuaji kwa nadra

Kifosisi ndogo inaweza kutibiwa kwa kupunguza mkazo wa kubeba mzigo (kwa mfano, kupunguza michezo yenye mshindo mkubwa au kunyanyua vitu vizito) na kwa kuepuka shughuli nzito, ambazo zinasaidia kupunguza maumivu na kuzuia mbinuko wa uti wa mgongo usiwe mbaya zaidi. Uti wa mgongo unaweza kunyooka kidogo kwa matibabu, lakini dalili huenda zisipungue.

Kifosisi inapokuwa mbaya zaidi, matibabu mara nyingi yanajumisha kuvaa kifungio cha uti wa mgongo au kulala kwenye godoro gumu. Matibabu yanaweza kupunguza dalili na kuzuia mbinuko usiwe mbaya.

Kwa nadra, licha ya matibabu, kifosisi inakuwa mbaya kwa kiasi ambacho upasuaji unahitajika ili kunyoosha mgongo.