Uvimbe wa Tezi ya Bartholin na Usaha wa Tezi ya Bartholin

(Uvimbe wa Bartholin)

NaCharles Kilpatrick, MD, MEd, Baylor College of Medicine
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Oct 2025
v13953167_sw

Uvimbe wa tezi ya bartolin ni vifuko vilivyojaa ute ambavyo vinaweza kujitengeneza wakati tezi zilizoko karibu na njia ya uke huziba. Uvimbe wa tezi ya bartolin unaweza kuambukiza na kuleta usaha wa maumivu.

  • Uvimbe wa tezi ya bartolin mara nyingi huwa hazina maumivu, lakini zikiwa kubwa, zinaweza kusababisha shinikizp au maumivu ma kutatiza kukaa, kutembea na ngono.

  • Mara nyingi uvimbe unaweza kuambukiza, ukitengeneza usaha wenye maumivu.

  • Madaktari wanaweza kuona au kuhisi uvimbe wakati wa uchunguzi wa fupanyonga.

  • Madaktari wanaweza kutengeneza uwazi wa kudumu kwenye uvimbe ili uvimbe uweze kutoa majimaji au wanaweza kufanya upasuaji wa kuondoa uvimbe.

Tezi za bartolin ni ndogo sana, tezi za mviringo zilizo katika vulva (ambazo zina labia na tishu nyingine kuzunguka uke). Zinaweza kutokea katika upande mwingine wa vulva. Kwa sababu ziko ndani ya ngozi, kawa kawaida huwezi kuhisi. Tezi hizi zinaweza kusaidia kutoa kiowevu cha kulainisha wakati ngono.

Anatomia ya Uzazi wa Kike wa Nje (Vulva)

Picha hii inaonyesha sehemu za nje za eneo la uzazi la mwanamke, ikijumuisha uke (ulio na tishu za misuli), uwazi wa urethra (ambapo mkojo hutolewa), na miundo inayozunguka kama vile labia na kisimi. Inaangazia pia tezi zinazosaidia kulainisha na maeneo yanayohusika na hisia za ngono, kama vile tezi za Bartholin, tezi za Skene, na tishu za uume kama vile balbu ya vestibular na crura ya kisimi.

BO VEISLAND/MAKTABA YA PICHA YA SAYANSI

Ikiwa njia ya tezi ya Bartholin imeziba, tezi hujaa ute na huongezeka ukubwa. Kisha huwa uvimbe. Uvimbe huu huwa takribani asilimia 3 kwa wanawake, mara nyingi wale walio katika umri wa miaka 20. Uvimbe unaweza kuambukiza, hali inayotengeneza usaha (eneo lililojifunga likiwa na usaha). Kadiri umri wa wanawake unavyozidi kusonga, kuna uwezekano mdogo sana wa kupata uvimbe na usaha.

Kwa kawaida, chanzo cha kuziba hakijulikani. Mara nyingine, uvimbe unaweza kuambukizwa na maambukizi kwa njia ya ngono, kama vile kisonono.

Mara chache, kunaweza kuwa na saratani katika tezi za Bartholin.

Je, Uvimbe wa Tezi ya Bartholin ni Nini?

Tezi ndogo katika upande mwingine wa uke, huitwa tezi za Bartholin, huweza kuzuiwa. Viowevu vinaweza kujikusanyana tezi kuvimba, hali inayosababisha uvimbe. Uvimbe huwa na uvimbe sawa na ukubwa wa haragwe hadi ukubwa mpira wa golfu au zaidi. Mara nyingi, hutokea tu upande mmoja. Huweza kuambukizwa, hali inayotengeneza usaha.

Dalili za Uvimbe wa Tezi ya Bartholin au Usaha

Uvimbe mwingi wa Bartholin hausababishi dalili zozote. Wanawake wanaweza kuhisi uvimbe usio na maumivu katika njia ya uke, hali inayofanya valva ipinde.

Ikiwa uvimbe utakuwa mkubwa, huweza kusababisha shinikizo na au maumivu. Huweza kutatiza uwezo wa kukaa, kutembea au ngono.

Ikiwa uvimbe utaambukizwa (ukitengeneza usaha), husababisha maumivu makali na wakati mwingine homa. Usaha huwa laini unapoguswa. Ngozi inayouzunguka huwa nyekundu.

Ngozi na tishu chini ya ngozi kwenye usaha huweza kuambukizwa, maambukizi yanayoitwa cellulitis. Ikiwa kutakuwa na cellulitis, sehemu iliyoathiriwa huwa nyekundu na laini, wanawake wanaweza kupata ute wa ukeni.

Utambuzi wa Uvimbe wa Tezi ya Bartholin au Usaha

  • Uchunguzi wa vulva

  • Wakati mwingine biopsi

Mwanamke anapaswa kumwona daktari katika hali zifuatazo:

  • Uvimbe unapoendelea kukua au kuendelea baada ya siku kadhaa za kuloweka eneo hilo katika maji ya uvuguvugu (kwenye beseni au tiba ya kukaa kwenye maji ya moto).

  • Uvimbe unapoleta maumivu (mara nyingi huwa na usaha).

  • Anapopata homa.

  • Uvimbe unapotatiza kutembea au kukaa.

  • Mwanamke ana umri mkubwa zaidi (kama vile ana umri wa miaka 40 au baada ya ukomo wa hedhi) kuliko kawaida kupata uvimbe.

Daktari anatathmini vulva ili kutambua uvimbe wa tezi ya Bartholin. Ikiwa uvimbe una ukubwa zaidi hali inayofanya wanawake wautambue au kwa kuona dalili, daktari anaweza kuona au kuhisi uvimbe wakati wa uchunguzi wa fupanyonga. Kwa kawaida madaktari wanaweza kutambua ikiwa umeambukizwa kwa mwonekano. Ikiwa ina ute, madaktari wanaweza kutuma sampuli ili ipimwe na kutambua maambukizi mengine, ikiwa ni pamoja na maambukizi kwa njia ya ngono. Ikiwa kuna usaha madaktari pia huchukua majimaji kwenye usaha.

Ingawa mara chache sana saratani hutokea katika tezi za Bartholinm daktari anaweza kuondoa sampuli ya uvimbe ili kupima katika hadubini (biopsi), hasa ikiwa tezi ina uzito au imekwama katika tishu inayozunguka au iwapo inaonekana kuwa uvimbe si wa kawaida (kwa mfano, umetokea kwa mwanamke katika umri wa uzee zaidi kuliko wastani).

Matibabu ya Uvimbe wa Tezi ya Bartholin au Usaha

  • Kulowesha eneo hilo na maji ya uvuguvugu

  • Ikiwa kuna usaha, hatua za kutoa majimaji

  • Ikiwa uvimbe wa tezi ya Bartholin au usaha utatokea tena au ikiwa daktari atahisi kuna saratani, atashauri kufanywa kwa upasuaji wa tezi

Iwapo uvimbe wa tezi ya Bartholin unasababisha maumivu au hausababishi kabisa, wanawake wanaweza kuutibu wenyewe. Wanaweza kutumia tiba ya kukaa kwenye maji ya moto au kuloweka kwa inchi chache za maji ya uvuguvugu. Hatua ya kulowesha inapaswa kudumu kwa dakika 10 hadi 15 na inatakiwa kufanywa mara 2 kwa siku. Wakati mwingine uvimbe hutoweka baada ya siku kadhaa za matibabu hayo.

Ikiwa uvimbe hautoweki baada ya kuloweka kwenye maji ya uvuguvugu kwa siku kadhaa, wanawake wanapaswa kumwona daktari. Daktari anaweza kuchukua hatua za kutoa majimaji kwenye uvimbe. Baada ya kupewa ganzi ili kutoa maumivu katika eneo hilo, mojawapo ya hatua zifuatazo zinaweza kufanywa:

  • Kuweka katheta: Upasuaji mdogo hufanyika kwenye uvimbe ili mpira mdogo wenye ncha (katheta) iweze kuingizwa kwenye uvimmbe. Ikishawekwa, puto hupulizwa na katheta huachwa hapo kwa wiki 4 hadi 6, ili kuwepo na uwazi wa kudumu. Katheta huingizwa na kuondolewa katika ofisi ya daktari, ingawa mara nyingi katheta hutoka yenyewe. Mwanamke anaweza kufanya shughuli zake za kawaida huku katheta ikiwa imewekwa, ingawa huenda ngono isiwe ya starehe.

  • Upasuaji tezi: Madaktari hukata sehemu ndogo na kushona kingo za ndani za uvimbe kwenye sehemu ya vulva. Marsupialization hutengeneza uwazi wa kudumu kwenye uvimbe ili uvimbe uweze kutoa maji inapohitajika. Utaratibu huu unafanywa katika chumba cha upasuaji. Wakati mwingine nusukaputi ya jumla inahitajika.

Baada ya hatua hizi, wanawake huwa na ute unaotoka kwenye tezi ya Bartholin kwa wiki kadhaa. Tiba ya kukaa kwenye maji ya moto mara kadhaa kwa siku kunaweza kusaidia kupunguza maumivu na kusaidia kupona haraka.

Ikiwa uvimbe utatokea tena au daktari atashuku unaweza kuwa wenye kansa, huweza kuondolewa kwa upasuaji. Utaratibu huu unafanywa katika chumba cha upasuaji.

Bila kujali matibabu, wakati mwingine uvimbe hutokea tena. Ikiwa utatokea tena, tezi yote ya Bartholin inaweza kuondolewa.

Matibabu ya usaha

Kwa usaha, matibabu ya awali yanahusisha upasuaji mdogo kwenye usaha na kuweka katheta ili kuutoa. Ikiwa usaha utarejea tena baada ya kuutoa, upasuaji wa tezi, ambao hutengeneza uwazi wa kudumu unaweza kufanyika ili kuzuia usaha usitokee tena.

Wakati mwingine usaha hutibiwa kwa kutumia viua vijasumu. Uamuzi wa kutibu kwa kutumia viua vijasumu hutegemea iwapo kuna dalili za maambukizo zaidi makali yanayojitokeza (kama vile homa, cellulitis ya ngozi inayozunguka usaha) au ikiwa kuna hatari kubwa ya maambukizo (kama vile mfumo wa kingamwili dhaifu).

Ikiwa viua vijasumu vitatolewa, kawa kawaida kupitia mdomo kwa wiki 1 pamoja na hatua ya kukausha usaha. Huenda mwanamke akahitaji kusalia hospitalini na kutibiwa kwa viua vijasumu kwenye vena, kulingana na kiwango cha ugonjwa.