Magonjwa ya Matumizi ya Vilevi

(Uteja)

Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Oct 2025
v39737126_sw

Ugonjwa wa matumizi ya vilevi ni nini?

Matumizi ya baadhi ya vitu (kama vile dawa fulani haramu) husababisha hisia za raha. Raha hiyo humfanya mtu atake kuendelea kutumia dutu hio. Dawa hizo zinaweza kuwa dawa halali kama vile pombe na tumbaku, dawa haramu, au dawa za kuagizwa na daktari. Baadhi ya watu hupata dawa za agizo la daktari, kama vile dawa za afyuni, kinyume cha sheria.

Ugonjwa wa matumizi ya vilevi ni pale unapoendelea kutumia kilevi japokuwa unapokitumia kinakusababishia matatizo nyumbani au kazini.

  • Watu wenye ugonjwa wa matumizi ya vilevi hawawezi kudhibiti matumizi yao ya vilevi

  • Ugonjwa wa matumizi ya dawa za kulevya unaweza kutokea kwa kutumia dawa halali au haramu

  • Hakuna aina maalumu ya haiba ambayo ina uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa matumizi ya vilevi

  • Si kila mara unapotumia kilevi inamaanisha kuwa una ugonjwa wa matumizi ya vilevi

  • Madaktari hutibu magonjwa haya kwa ushauri nasaha na wakati mwingine kwa dawa

Je, nini husababisha ugonjwa wa matumizi ya vilevi?

Si kila mtu anayetumia kilevi ana ugonjwa wa matumizi ya vilevi. Japokuwa karibu kila mtu anaweza kupata ugonjwa wa matumizi ya vilevi, lakini hatari yako huongezeka ikiwa:

  • Kilevi hukupatia starehe sana na ni rahisi kukipata

  • Huamini kwamba kilevi kina hatari sana

  • Mara nyingi una majonzi, upweke au wasiwasi

  • Una tatizo fulani la akili, kama vile matatizo ya utu au mfadhaiko mkubwa

  • Wanafamilia au marafiki zako wanatumia vilevi (huu ni ukweli hasa kwa vijana)

Na hatari yako pia huongezeka ikiwa unatumia dawa za kutuliza maumivu za opioid ulizoagizwa na daktari kwa ajli ya jeraha lenya kuuma au maumivu sugu. Opioid, japo ni njia halali ya kudhibiti maumivu, ni za kulevya sana.

Zipi ni dalili za ugonjwa wa matumizi ya vilevi?

Ukiwa na ugonjwa wa matumizi ya vilevi, unaweza:

  • Kushindwa kudhibiti matumizi ya kilevi: Unakitumia hata kama unajua kuwa ni kibaya kwako

  • Kuwa na ustahimilivu kwa kilevi: Unahitaji kukitumia zaidi na zaidi ili uweze kupata athari ile ile

  • Uzoefu wa kujiondoa: Unapata dalili mbaya unapoacha kutumia kilevi

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtu ana ugonjwa wa matumizi ya vilevi?

Wakati mwingine watu huwambia madaktari kuwa wana hilo tatizo. Au madaktari wanaweza kukushuku kuwa una ugonjwa wa matumizi ya vilevi ikiwa:

  • Unatumia muda mwingi ukitafuta, ukitumia au ukipona kutokana na matumizi ya vilevi

  • Unataka kuacha kutumia kilevi lakini unashindwa

  • Unatamani sana kutumia kilevi

  • Unashindwa kutekeleza majukumu yako kazini, shuleni au nyumbani kwa sababu ya kilevi

  • Unatumia kilevi katika mazingira hatarishi, kama vile unapokuwa unaendesha gari

  • Unaacha kujishughulisha na shughuli za kijamii au kazi kwa sababu ya kilevi

Ustahimilivu na kuacha pia ni ishara za ugonjwa wa matumizi ya vilevi, isipokuwa kama zitatokea wakati ukitumia kilevi kihalali. Kwa mfano, unaweza pia kuacha kutumia opioid baada ya kutumia opioid chini ya wiki moja, ambayo inaweza kuwa muhimu kwa aina fulani ya majeraha yenye maumivu, kama vile kuungua kwa kiasi kikubwa.

Ingawa vipimo vya mkojo na damu vinaweza kuonyesha kama una dawa au dawa fulani katika mfumo wako, haviwezi kuonyesha kama una tatizo la matumizi ya dawa za kulevya.

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa matumizi ya vilevi?

Matibabu hutegemea kilevi. Madaktari wanaweza kutibu ugonjwa wa matumizi ya vilevi kwa kutumia:

  • Usaidizi wa kisaikolojia

  • Usaidizi wa familia

  • Usaidizi wa kikundi

  • Dawa

Ugonjwa wa matumizi ya vilevi maalum, kwa mfano tatizo la matumizi ya pombe na tatizo la matumizi ya opioid, hutofautiana matibabu.

Ninaweza kupata wapi taarifa zaidi kuhusu ugonjwa wa matumizi ya vilevi?

  1. Al-Anon Family Groups (al-anon.org/)

  2. Alcoholics Anonymous (aa.org)

  3. Hazelden Betty Ford Foundation (hazelden.org)

  4. LifeRing (lifering.org)

  5. Narcotics Anonymous (na.org)

  6. Muungano wa Kitaifa kuhusu Ugonjwa wa Akili (nami.org)