Je, E. koli ni nini?
Escherichia koli, ambayo mara nyingi huitwa tu E. koli, ni kikundi cha bakteria. Kuna aina mbalimbali za E. koli. Baadhi ya aina huishi kwenye utumbo wako. Ikiwa E. koli hawa wataingia katika sehemu zingine za mwili wako, unawezaa kuumwa. Ikiwa aina nyingine ya E. koli itaingia kwenye utumbo, pia unaweza kuumwa.
Maambukizi kwenye utumbo wako yanaweza kusababisha kuharisha (mara kwa mara, kinyesi laini au chanye majimaji) na maumivu katika eneo la tumbo lako.
E. koli ndio chanzo kikuu cha maambukizi ya kibofu cha mkojo kwa wanawake
Maambukizi mengi ya E. koli yanaweza kutibiwa kwa dawa za kuua bakteria
Onana na daktari mara moja ikiwa unahara damu au kuhara kwako kunaambatana na homa.
Je, nini husababisha maambukizi ya E. coli?
Unaweza kupata maambukizi ya E. coli kwenye utumbo wako ikiwa:
Utakula chakula chenye bakteria wa E. koli ndani yake
Utagusa wanyama ambao wana maambukizi ya E. koli
Utakunywa maji yenye E. koli ndani yake, hasa kutoka kwenye maziwa, madimbwi, vijito, na mabwawa
Chakula kilichopikwa kinaweza kuwa na E. koli ndani yake kama hakikupikwa vizuri. Chakula kutoka shambani, kama vile saladi, kinaweza kuwa na E. coli ikiwa mazao yalioshwa kwa maji machafu baada ya kuchumwa.
Kushika wanyama katika bustani za wanyama vipenzi wakati mwingine husambaza E. koli.
Nchi mbalimbali zina aina mbalimbali za E. koli. Ikiwa utasafiri kwenda nchi nyingine, unaweza kuumwa kwa sababu ya E. koli ambazo zinapatikana sana katika nchi hiyo (tazama Kuhara kwa Wasafiri).
E. koli O157:H7
E. koli O157:H7 ni aina ya E. koli ambayo inaweza kuambukiza utumbo wako mpana (utumbo wako mkubwa) na kusababisha kolaitisi. Kolaitisi ni kuvurugika na kuvuja damu kwenye utumbo wako mpana.
Unaweza kupata maabukizi ya E. koli O157:H7 kwa namna ile ile sawa na maambukizi mengine yaE. koli.
Je, dalili za maambukizi ya E. koli ni zipi?
Dalili hutegemea sehemu ya mwili yalipo maambukizi na aina ya E. koli uliyonayo.
Maambukizi kwenye utumbo wako yanaweza kusababisha:
Kuhara kinye chenye majimaji, kwa haraka
Tumbo kukakamaa
Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika
Maambukizi ya E. coli O157:H7 kwenye utumbo wako pia yanaweza kusababisha damu kwenye kinyesi chako.
Maambukizi katika njia na kibofu cha mkojo yanaweza kusababisha:
Kuhitaji kukojoa mara kwa mara
Maumivu na hali ya kuchoma wakati wa kukojoa
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maambukizi ya E. koli?
Madaktari hufanya vipimo kutafuta E. koli kwa kuchukua sampuli za damu, mkojo, kinyesi chako, au vitu vingine vilivyo na maambukizi. Daktari wako atatuma sampuli kwenye maabara. Maabara itapima sampuli ili kujua una aina gani ya E. koli na ni dawa gani za kuua bakteria zinazoweza kuiua.
Je, madaktari hutibu vipi maambukizi ya E. koli?
Kama una kuhara kwa wasafiri kutokana na maambukizi ya E. koli kwenye utumbo wako, daktari anaweza kukufanya:
Kunywa vinywaji kwa wingi
Utumie dawa ya kupunguza kuhara
Utumie dawa za kuua bakteria, kama unaharisha mara kwa mara
Ikiwa una maambukizi ya E. koli katika kibofu cha mkojo, njia yako ya mkojo au sehemu nyingine ya mwili wako, daktari wako atakufanya:
Tumia dawa za kuua bakteria
Je, ninaweza kuzuia maambukizi ya E. koli?
Osha mikono yako baada ya kwenda uani au kubadilisha nepi
Mara zote osha mikono yako, kaunta, mbao za kukatia na vyombo kila mara baada ya kugusa nyama mbichi
Pika nyama ya ng'ombe hadi nyuzi joto 160°F (71°C) au zaidi kabla ya kuila—kwa kawaida ya kijivu au kahawia ndani, na si waridi au nyekundu
Jiepushe maziwa ambayo hayakuchemshwa, na bidhaa zingine za maziwa na juisi ambayo haijapitia hatua ya kuondoa vijidudu (tiba ya joto ambayo huua bakteria)
Jiepushe kumeza maji kutoka kwenye maziwa, madimbwi, vijito, na mabwawa
Wanawake wanapaswa kujipangusa kuanzia mbele kurudi nyuma na wajiepushe kuvaa nguo za ndani zinazobana ili kuepuka maambukizi ya njia na kibofu cha mkojo