Ugonjwa wa kuonyesha sehemu za siri huhusisha kufichua sehemu za siri ili kusisimka kingono au kuwa na hamu kubwa ya kutazamwa na watu wengine wakati wa tendp la ngono. Tatizo la kuonyesha sehemu za siri huhusisha kutekeleza misukumo au mawazo ya kuonyesha sehemu za siri au kusumbuliwa kisaikolojia au kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya tamaa na ndoto hizo. Tatizo la kuonyesha sehemu za siri unaweza pia kuhusisha kutekeleza misukumo kwa mtu ambaye hajatoa ridhaa.
Watu wengi wanaoonyesha sehemu za siri hawa tatizo la kuonyesha sehemu za siri.
Madaktari hutambua tatizo la kuonyesha sehemu za siri wakati watu wanahisi mfadhaiko mkubwa au kushindwa kufanya kazi vizuri kwa sababu ya tabia zao, au wametekeleza misukumo yao na mtu ambaye hajaridhia.
Matibabu, ambayo kwa kawaida huanza baada ya watu wanaoonyesha sehemu za siri kukamatwa, yanajumuisha tiba ya kisaikolojia, vikundi vya msaada na baadhi ya dawa za kupunguza mfadhaiko.
Uonyeshaji wa sehemu za siri ni aina ya parafilia.
Watu wanaoonyesha sehemu za siri (kwa kawaida wanaume) huonyesha sehemu zao za siri, mara nyingi kwa wageni wasiojua, na hupata msisimko wa kingono wanapofanya hivyo. Huenda wakawa wanajua hitaji lao la kumshangaza, kumshtua, au kumvutia mtazamaji asiyetaka. Mwathirika karibu kila mara huwa mwanamke au mtoto wa jinsia yoyote. Idadi kubwa ya watu wenye tabia ya kuonyesha sehemu za siri hawafanyi kulingana na misukumo yao (yaani, hawashiriki katika tabia za ngono zinazosababisha ukatili wa kimwili). Mgusano halisi wa kingono karibia kamwe si tamanio, kwa hivyo watu wanaoonyesha sehemu za siri ni nadra sana wafanye tendo la ubakaji.
Ingawa tabia ya kuonyesha sehemu za siri ni ya kawaida sana, kiwango halisi cha tatizo la kuonyesha sehemu za siri haijulikani, lakini kinakadiriwa kuwa hadi takribani asilimia 8% kwa wanaume na kinaonekana kuwa cha chini kwa wanawake (asilimia 3 hadi 6%).
Tatizo la kuonyesha sehemu za siri kwa kawaida huanza wakati wa ujana, lakini wakati mwingine tendo la kwanza linaweza kutokea kabla ya ujana au katika umri wa makamo. Watu wengi wenye tabia ya kuonyesha sehemu za siri wameoa au wameolewa, lakini ndoa zao mara nyingi huwa na matatizo.
Takriban asilimia 30% ya wahalifu wa kijinsia wa kiume wanaokamatwa ni watu wenye tabia ya kuonyesha sehemu za siri. Huwa na mazoea ya kuendelea tabia zao. Takribani asilimia 20 hadi 50 hukamatwa tena.
Kujionyesha sehemu za siri kwa wageni wasiotarajia kwa ajili ya msisimko wa kingono ni nadra miongoni mwa wanawake. Wanawake wana njia nyingine za kujionyesha: kuvaa kwa njia ya kuchochea hisia (jambo ambalo linazidi kukubalika kama la kawaida) na kuonekana katika kumbi mbalimbali za vyombo vya habari na burudani. Kushiriki katika maeneo haya peke yake hakumaanishi kuwa mtu ana tatizo la afya ya akili.
Kwa baadhi ya watu, tatizo la kuonyesha sehemu za siri hujitokeza kama hamu kubwa ya kuwafanya watu wengine watazame vitendo vyao vya kingono. Watu wa aina hii wanataka waonekane na hadhira inayokubali, badala ya kuwashangaza watu. Watu wenye aina hii ya tabia ya kuonyesha sehemu za siri wanaweza kutengeneza filamu za ngono au kuwa wasanii wa burudani ya watu wazima. Ni nadra sana kwa wao kusumbuliwa kisaikolojia au kushindwa kufanya kazi vizuri kwa sababu ya hamu yao, hivyo huenda wasiwe na tatizo la afya ya akili.
Watu wengi wenye tabia ya kuonyesha sehemu za siri hawana tatizo, lakini baadhi yao wanaweza kuwa na tatizo la ugonjwa wa haiba linalowakabili (kwa kawaida ugonjwa wa utu wa kupinga jamii) au tatizo la mwenendo.
Utambuzi wa Ugonjwa wa Kuonyesha Sehemu za Siri
Tathmini ya daktari, kulingana na vigezo vya kawaida vya uchunguzi wa magonjwa ya akili
Madaktari hutambua tatizo la kuonyesha sehemu za siri wakati
Watu wamekuwa wakisisimka mara kwa mara na kwa nguvu kwa kuonyesha sehemu zao za siri au kutazamwa na watu wengine wakati wa sshughuli za kingono, na msisimko huo umejitokeza kupitia mawazo, hamu kali, au tabia.
Kutokana na hali hiyo, watu hupata mfadhaiko au hushindwa kufanya kazi zao vizuri (kazini, katika familia, au katika mahusiano na marafiki), au wametenda kulingana na hamu zao kwa mtu ambaye hakuridhia.
Amekuwa na hali hiyo kwa kipindi cha miezi 6 au zaidi.
Katika kutambua tatizo la kuonyesha sehemu za siri kimapenzi, daktari pia hubainisha kama mtu husisimka kingono kwa kuonyesha sehemu zake za siri kwa watoto ambao hawajafikia balehe, watu waliokomaa kimwili, au makundi yote mawili.
Matibabu ya Ugonjwa wa Kuonyesha Sehemu za Siri
Tiba ya kisaikolojia na makundi ya msaada
Dawa fulani za kuzuia mfadhaiko
Wakati mwingine dawa nyingine
Matibabu ya tatizo la kuonyesha sehemu za siri kwa kawaida huanza baada ya watu wenye tabia ya kuonyesha sehemu za siri kukamatwa. Inajumuisha tiba ya saikolojia, makundi ya msaada na dawa za kuzui mfadhaiko zinazoitwa vizuizi vya uchaguzi wa kutumia tena serotonini (SSRIs).
Ikiwa dawa za SSRI hazifanyi kazi, dawa zinazobadilisha hamu ya ngono na kupunguza viwango vya testosteroni zinaweza kutumika. Dawa hizi zinajumuisha leuprolide na medroxyprogesterone acetate. Watu ni sharti watoe idhini yao iliyoarifiwa ya kutumia dawa hizi, na madaktari hufanya vipimo vya damu mara kwa mara ili kufuatilia athari za dawa kwenye ini, pamoja na vipimo vingine (ikiwa ni pamoja na vipimo vya uwiano wa mifupa na vipimo vya damu ili kupima viwango vya testosteroni).