Microsporidiosisi

NaChelsea Marie, PhD, University of Virginia;
William A. Petri, Jr, MD, PhD, University of Virginia School of Medicine
Imekaguliwa naChristina A. Muzny, MD, MSPH, Division of Infectious Diseases, University of Alabama at Birmingham
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa May 2024
v787003_sw

Microsporidiosisi ni maambukizi yanayosababishwa na Microsporidia, ambao ni kuvu vimelea. Dalili zinategemea viungo vilivyoambukizwa, lakini maambukizi yanaweza kusababisha kuharisha, dalili nyingine za utumbo au dalili za macho.

  • Microsporidiosis husababisha dalili hasa kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kingamwili, kama vile watu wenye VVU.

  • Dalili zinatofautiana lakini zinajumuisha kuharisha sugu, maumivu ya tumbo, homa, kupoteza uzito na mwako wa macho.

  • Madatari wanatambua maambukizi kwa kubainisha microsporidia kwenye sampuli ya tishu iliyo na maambukizi au kwenye kinyesi, mkojo au majimaji mengine ya mwili.

  • Dawa zinaweza kudhibiti lakini si kuondoa maambukizi.

(Angalia pia Muhtasari wa Maambukizi ya Vimelea.)

Microsporidia imekuwa ikiainishwa kama protozoa lakini sasa wanachukuliwa kama fungi. Vimelea hivi vya fungi vinavyotengeneza mbegu huishi ndani ya seli zilizoambukizwa.

Microsporidia huweza kuathiri utumbo, ini, kibofu cha mkojo, njia ya biliari (neli inayounganisha ini na kibofu nyongo kwa utumbo mdogo), macho, sinasi, misuli, njia za upumuaji, njia ya njia ya mkojo na wakati mwingine, ubongo. Maambukizi yanaweza kuenea katika mwili wote.

Spishi mbalimbali za Microsporidia zinaweza kusababisha maambukizi kwa watu, lakini dalili zinatokea hasa kwa wale wenye VVU ya hatua za juu au matatizo mengine ambayo yanadhoofisha sana mfumo wa kingamwili. Watu walio na mfumo wa kingamwili wenye afya wanaweza kupata dalili za macho ikiwa microsporidia inaathiri kornea.

Microsporidia inaenea kupitia mbegu ambazo zinaweza

  • Kumezwa

  • Kuvutwa kwa hewa

  • Kuingia kwenye tishu kupitia jicho

Uenezaji wa microsporidia hutokea hasa kupitia chakula, ikiwa ni pamoja na samaki na kaa. Usambazaji pia unatokea kupitia maji ikiwa ni pamoja na maji ya baharini, maji ya kunwa na vyanzo vingine vya kimazingira.

Ndani ya mwili, mbegu za microsporidia huingia kwenye seli, ambapo mbegu zinakua, kuongezeka na kutegeneza mbegu zaidi. Seli zilizoambukizwa hatimaye zinapasuka, zikitoa mbegu. Mbegu hizi zinaweza kuenea katika mwili wote, zikisababisha mwako au zinaweza kutolewa kwenye mazingira katika kutoa hewa, kinyesi au mkojo.

Dalili za Microsporidiosisi

Dalili za Microsporidiosisi zinatofautiana kutegemeana na

  • Ni spishi ipi inayosababisha maambukizi hayo

  • Ni viungo gani ambavyo vinaathiriwa

  • Ni vizuri kiasi gani mfumo wa kingamwili unafanya kazi

Watu wenye kingamwili ya kawaida kwa kawaida hwana dalili au kuharisha kidogo. Maambukizi ya macho yanaweza pia kutokea yameendelea kuripotiwa kwa watu wenye afya.

Watu wenye VVU au matitizo mengine ambayo yanadhoofisha mfumo wa kinga mwili, microsporidiosis inaweza kusababisha hali sugu ya kuharisha na maambukizi mbalimbali (kama vile homa ya ini na sinusitisi). Endapo microsporidiosis inaathiri utumbo, watu huenda wasinyonye virutubisho vya kutosha (huitwa hali ya kushindwa kunyonya virutubishi), na kusababisha kupungua uzito.

Dalili nyingine za microsporidiosis zinaweza kujumuisha maumivu ya tumbo, homa ya nyongo ya manjano, homa, kukohoa kusikokoma, maumivu y misuli, maumivu ya kichwa na mwako wa macho yakiwa na wekundu. Kuona kunaweza kuwa na ukungu. Ikiwa maambukizi ya macho ni makubwa, upofu unaweza kutokea.

Utambuzi wa ugonjwa wa Microsporidiosisi

  • Uchunguzi wa sampuli ya tishu iliyoathiriwa, kinyesi, mkojo au majimaji mengine ya mwili

Ili kutambua microsporidiosis, madaktari wanachunguza sampuli ya tishu iliyoathiriwa (inachukuliwa kwa kuondoa kipande kwa ajili ya uchunguzi) au sampuli ya majimaji ya mwili. Wanachunguza sampuli kwa kutumia hadubini, kwa kawaida kwa kutumia mbinu maalumu ili kufanya microsporidia ionekane zaidi. Kwa mfano, sampuli za kinyesi, mkojo, damu, makohozi, majimaji ya uti wa mgongo (huchukuliwa kwa kinga majimaji ya uti wa mgongo), kornea (huchukuliwa kwa kukwangua) huenda zikachunguzwa.

Vipimo pia vinaweza kufanywa ili kubainisha nyenzo zakijeni za kimelea (DNA) kwenye sampuli.

Matibabu ya Microsporidiosisi

  • Albendazole au fumagillin

  • Kwa watu wenye VVU, pia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI

  • Kwa maambukizi ya jicho, albendazole (ikichukuliwa kwa mdomo) na fumagillin (kama matone)

Endapo mfumo wa kingamwili ni wa kawaida, hali ndogo za microsporidiosis kwa kawaida huisha bila matibabu.

Watu wenye VVU, ni muhimu sana kutibu maambukizi ya VVU kwa ufanisi kadiri iwezekanavyo kwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI. Matibabu kama hayo yanaweza kuimarisha mfumo dhaifu wa kingamwili, ambao kwa kawaida husaidia kudhibiti kuhara na dalili nyingine. Vilevile ni muhimu kuziondao sababu zozote za kudhoofisha kingamwili, ikiwa zipo.

Tiba ya kupambana na bakteria wa microsporidiosis hutegemea ni spishi ipi ya Microsporidia inasababisha maambukizi, endapo mfumo wa kingamwili wa mtu huyo ni wa kawaida, na viungo vipi vinahusika. Albendazole, ikimezwa kwa mdomo, inaweza kudhibiti kuharisha ikiwa spishi inayosababisha maambukizi ya matumbo inaweza kudhibitiwa nayo. Hata hivyo, dawa hiyo haiondoi maambukizi hayo na ina madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na ukandamizaji wa uboho (kusababisha seli chache za damu kutengenezwa kwenye uboho) na mwako wa ini (homa ya ini).

Albendazole inatumiwa pia kutibu microsporidiosis ambayo inaathiri misuli au ambayo imeenea katika mwili wote ikiwa spishi inayosababisha maambukizi inadhibitiwa nayo.

Tembe za Fumagillin zikitumiwa kwa kumeza zimetumiwa kudhibiti kuharisha ambapo spishi zenye maambukizi za Microsporidia zinaweza kudhuriwa, lakini inaweza pia kuwa na madhara makubwa. Tembe za Fuagillin hazipatikani nchini Marekani.

Maambukizi ya macho yanatibiwa kwa kutumia albendazole inayomezwa na matone ya macho ya fumagillin. Dawa za macho za Fluoroquinolone au voriconazole wakati mwingine zinafaa. Endapo dawa hizi hazitaondoa dalili hizo, upasuaji ili kurekebisha kornea (keratoplasti) huenda ikahitajika.