Vifafa Vinavyohusiana na Homa

NaM. Cristina Victorio, MD, Akron Children's Hospital
Imekaguliwa naAlicia R. Pekarsky, MD, State University of New York Upstate Medical University, Upstate Golisano Children's Hospital
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Apr 2025
v11677090_sw

Vifafa vinavyohusiana na homa ni vifafa vinavyosababishwa na homa ya angalau 100.4°F (karibia 38°C).

  • Vifafa vingi vinavyosababishwa na homa si hatari na husababishwa na homa inayotokana na maambukizi.

  • Mara chache sana, kifafa kinachohusishwa na homa kinaweza kuwa ishara ya kwanza ya ugonjwa wa neva ambao haukubainishwa hapo awali.

  • Wakati mwingine madaktari hufanya vipimo vya damu na uwekaji wa mrija kwenye uti wa mgongo ili kuona matatizo makubwa ambayo yanaweza kusababisha kifafa.

  • Kwa kawaida watoto wanahitaji dawa za kukomesha kifafa ikiwa tu kinadumu kwa dakika 5 au zaidi.

  • Watoto wengi hawahitaji kutumia dawa ili kuzuia kifafa kinachohusishwa na homa.

Kifafa ni utoaji wa umeme usio wa kawaida, usiodhibitiwa, wa seli za neva katika ubongo au sehemu ya ubongo. Utoaji huu wa umeme usio wa kawaida unaweza kusababisha

  • Degedege

  • Miendo isiyo ya hiari

  • Ufahamu uliogeuzwa

  • Uhisi usi wa kawaida

Degedege ni kali, isiyo ya hiari, ya kutetemeka na kukaza kwa misuli katika sehemu kubwa ya mwili.

Vifafa vya homa hutokea kwa takriban asilimia 2 hadi 5% ya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 lakini mara nyingi hutokea kwa watoto wenye umri kati ya miezi 12 na miezi 18. Kifafa kinachotokea kwa mtoto mwenye homa na ana umri wa miaka 6 au zaidi hakichukuliwi kuwa kifafa kinachohusiana na homa. (Angalia pia Vifafa kwa Watoto.)

Vifafa vinavyohusiana na homa vinaweza kutokea katika familia. Jeni kadhaa zinazohusiana na kifafa kinachohusiana na homa zimetambuliwa.

Vifafa vingi vinavyohusiana na homa huchukua chini ya dakika 15, na takriban silimia 20 hadi 35 ya watoto walio na kifafa kinachohusiana na homa huwa hawapati kingine.

Je, Ulijua...

  • Takriban asilimia 20 hadi 35% ya watoto walio na kifafa cha homa huwa hawapati tena.

Vifafa vinavyohusiana na homa vinaweza kuwa rahisi au changamano:

  • Rahisi: Mwili mzima hutetemeka (kinaitwa kifafa cha jumla) kwa chini ya dakika 15 na watoto kwa kawaida hupoteza fahamu. Zaidi ya asilimia 90% ya kifafa kinachohusishwa na homa ni rahisi. Aina hii ya kifafa kinachohusishwa na homa haitokei zaidi ya mara moja katika kipindi cha saa 24.

  • Changamano: Mwili mzima hutetemeka kwa dakika 15 au zaidi (mara kwa mara au kwa kusimama), au upande mmoja tu au sehemu moja ya mwili hutetemeka (huitwa kifafa kidogo au cha mahali mahususi), au kifafa hutokea angalau mara mbili ndani ya saa 24. Watoto walio na kifafa changamano kinachohusishwa na homa wana uwezekano mdogo wa kupata ugonjwa wa kifafa baadaye utotoni.

Baada ya kifafa kinachohusishwa na homa, watoto mara nyingi husinzia. Kipindi hiki cha muda baada ya kifafa (kipindi cha baada ya kifafa) huchukua dakika kadhaa au wakati mwingine huchukua saa kadhaa.

Vifafa kinavyohusishwa na homa kwa kawaida husababishwa na homa yenyewe. Mara nyingi, homa husababishwa na maambukizi madogo kama vile maambukizi ya virusi vya upumuaji au maambukizi ya sikio. Katika hali kama hizo, maambukizi hayo na kifafa havina madhara. Sehemu muhimu ya fasili ya kifafa kinachohusishwa na homa ni kwamba homa na kifafa havisababishiwi na maambukizi ya ubongo kama vile meningitis au encephalitis.

Kifafa cha muda mrefu kinachohusiana na homa

Hali ya kifafa inarejelea kifafa kimoja cha muda mrefu, au vifafa kadhaa vifupi vinavyotokea bila mtoto kupata fahamu tena kati ya kifafa. Vifafa vinavyohusishwa na homa vinavyodumu kwa dakika 30 au zaidi huchukuliwa kuwa hali ya homa na kifafa.

Watoto walio na hali ya homa na kifafa wako katika hatari ya kuharibika ubongo ikiwa hawatatibiwa haraka.

Utambuzi wa Vifafa Vinavyohusiana na Homa

  • Tathmini ya daktari

  • Wakati mwingine uwekaji wa mrija kwenye uti wa mgongo, vipimo vya damu, au picha za ubongo

Kwa sababu wazazi hawawezi kujua endapo watoto wana maambukizi ya ubongo, ambayo ni hatari kwa uhai, watoto walio na homa na ambao wamepata kifafa kwa mara ya kwanza au ni wagonjwa sana wanapaswa kupelekwa kwenye idara ya dharura mara moja kwa ajili ya tathmini.

Kipimo cha Maabara

Madaktari huwachunguza watoto na, kulingana na kile wanachokibaini, wakati mwingine hufanya vipimo ili kuangalia matatizo makubwa ambayo yanaweza kusababisha kifafa. Vipimo hivi vinaweza kujumuisha

  • Kinga majimaji ya uti wa mgongo (kupenyeza sindano kwenye uti wa mgongo) kwa kutumia uchanganuzi wa majimaji kutoka sehemu zinazozunguka uti wa mgongo (majimaji ya uti wa mgongo) ili kuangalia kama kuna meningitis na encephalitis.

  • Vipimo vya damu ili kuangalia viwango vya sukari (glukosi), kalsiamu, magnesiamu, sodiamu, au vitu vingine ili kuangalia matatizo ya umetaboli

  • Cultures za damu na mkojo ili kuangalia maambukizi

  • Wakati mwingine, picha za ubongo kwa kutumia upigaji picha kwa mwangwi wa sumaku (MRI) au tomografia ya kompyuta (CT) (ikiwa MRI haipatikani)

  • Electroencephalography (EEG) (kipimo kinachobaini shughuli zisizo za kawaida za umeme kwenye ubongo) kwa watoto wenye dalili fulani au ambao wana kifafa kinachorudia

Matibabu ya Vifafa Vinavyohusiana na Homa

  • Dawa za kupunguza homa

  • Dawa za kukomesha kifafa ikiwa kitaendelea kwa dakika 5 au zaidi

Kwa kawaida, vifafa vinavyosababishwa na homa huchukua chini ya dakika 5, na hakuna matibabu yanayotolewa zaidi ya dawa za kupunguza homa.

Madaktari kwa kawaida hutoa dawa za kukomesha kifafa kinachohusishwa na homa kinachodumu kwa dakika 5 au zaidi ili kuzuia hali ya kifafa. Dawa zinajumuisha dawa za kutuliza na dawa ya kuzuia kifafa. Kwa kawaida dawa hizi hutolewa kwa njia ya mshipa (ndani ya mishipa). Ikiwa dawa haiwezi kutolewa kwa njia ya mishipa na mtoto ana umri wa zaidi ya miaka 2, jeli ya kupoza inaweza kuwekwa kwenye rektamu au kioevu cha kupoza kinaweza kuwekwa puani (ndani ya pua). Watoto ambao wamepokea dawa hizi au ambao wana kifafa cha muda mrefu au hali ya kifafa hufuatiliwa kwa umakini kwa matatizo ya kupumua na shinikizo la damu.

Ubashiri wa Vifafa Vinavyohusiana na Homa

Takriban asilimia 20 hadi 35 ya watoto hupata kifafa cha ziada kinachohusishwa na homa (kifafa kinachohuishwa na homa kinachojirudia). Watoto wana uwezekano mkubwa wa kupata kifafa zaidi ikiwa walikuwa chini ya mwaka 1 walipopata kifafa cha kwanza kinachohusishwa na homa au ikiwa wana jamaa wa karibu ambao wamewahi kupata kifafa cha homa.

Watoto ambao wamekuwa na kifafa kinachohusishwa na homa wana hatari iliyoongezeka kidogo (karibu asilimia 2 hadi 6) ya kupata ugonjwa wa kifafa hiyo haihusishi homa (kifafa kisicho na homa, au kifafa). Ikiwa watoto wamekuwa na kifafa cha homa au wana vihatarishi vya ziada (kama vile kuchelewa kwa ukuaji au historia ya kifafa katika familia), hatari ni kubwa zaidi (hadi asilimia 10).

Kwa baadhi ya watoto, kuwa na kifafa kinachohusishwa na homa kwa muda mrefu husababisha mabadiliko katika ubongo ambayo husababisha kifafa kisicho na homa hapo baadaye. Katika baadhi ya visa, madaktari wanakuwa hawana uhakika endapo kuwa na kifafa cha muda mrefu kinachohuishwa na homa pekee yake hufanya kifafa kisicho na homa kiwe na uwezekano mkubwa zaidi au kama baadhi ya mambo ya msingi yanawafanya watoto wawe na uwezekano mkubwa wa kupata kifafa cha muda mrefu kinachohusishwa na homa kisha baadaye kisicho na homa.

Vifafa rahisi vinavyohusishwa na homa havifikiriwi kusababisha vifafa au matatizo mengine ya neva. Hata hivyo, kifafa kinachohusishwa na homa wakati mwingine ni ishara ya kwanza ya ugonjwa wa neva ambao haukutambuliwa hapo awali au ugonjwa wa kifafa. Wakati mwingine madaktari wanaweza kutazama nyuma na kuona dalili za ugonjwa huo katika historia ya mtoto wa zamani. Wakati mwingine dalili zingine za ugonjwa hazionekani hadi baadaye. Katika hali yoyote ile, kifafa kinachohusiahwa na homa hakifikiriwi kusababisha matatizo hayo.

Kinga ya Vifafa Vinavyohusiana na Homa

Endapo watoto wamewahi kupata kifafa kinachohusishwa na homa, wazazi wanapaswa kuwa waangalifu na kutibu homa kali, ambayo inaweza kusababisha kifafa. Hata hivyo, kifafa kinachohusishwa na homa mara nyingi hutokea mapema wakati wa homa, halijoto ya mtoto inapoongezeka, au kabla wazazi hawajajua kwamba mtoto ni mgonjwa na kujua ana homa.

Dawa za kuzuia kifafa zaidi (dawa za kuzuia kifafa—angalia upau wa pembeni Kutumia Dawa Kutibu Kifafa kwa Watoto) kwa kawaida hazitolewi kwa watoto ambao wamekuwa na kifafa kinachohusishwa na homa mara chache. Hata hivyo, dawa za kuzuia kifafa zinaweza kutolewa kwa watoto ambao wana mojawapo ya yafuatayo:

  • Kifafa changamani kinachohusishwa na homa na matatizo ya neva (kama vile kupooza kwa ubongo au matokeo yasiyo ya kawaida ya upigaji picha wa ubongo)

  • Historia thabiti ya kifafa katika familia na kifafa rahisi au changamani cha homa kinachojirudia

  • Kifafa cha muda mrefu kinachohusiana na homa

  • Zaidi ya vifafa 4 vinavyohusiana na homa kwa mwaka

Endapo watoto ambao wamekuwa na kifafa kinachohusishwa na homa kwa muda mrefu watapata kifafa kinachofuata ambacho huchukua zaidi ya dakika 5, madaktari wanaweza kutoa agizo la jeli ya diazepam ili iwekwe kwenye rektamu. Watoto wanaweza kutibiwa na dawa hii nyumbani.