Slipped Capital Femoral Epiphysis (SCFE)

NaNora E. Renthal, MD, PhD, Harvard Medical School
Imekaguliwa naMichael SD Agus, MD, Harvard Medical School
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Sept 2025
v38721070_sw

Ugonjwa wa kuteleza kwa mfupa wa paja ni ugonjwa wa mfupa unaotokea wakati kichwa cha mfupa wa paja unateleza kutka kwenye shingo la mfupa wa paja kwenye sehemu ya juu ya sahani ya ukuaji karibu na kiungio.

  • Tatizo hili linaweza kusababishwa na kiongio cha nyonga dhaifu kinachokua.

  • Dalili za kawaida zinajumuisha ugumu au maumivu kidogo kwenye nyonga.

  • Utambuzi wa ugonjwa unatokana na eksirei na wakati mwingine vipimo vingine vya picha.

  • Upasuaji kwa kawaida unahitajika ili kurekebisha tatizo hilo.

Fupa la paja ni mfupa wa paja. Epifizi kubwa ya mfupa wa paja ni kichwa cha fupa la paja (kipira kwenye kipira na soketi ya kiungio cha nyonga). Epifisisi inaweza kuteleza kutoka kwenye shingo la fupa la paja. Kuteleza kunatokea upande wa juu wa sahani ya ukuaji ya mfupa wa paja karibu na kiungio cha nyonga. Sahani za ukuaji ni maeneo laini ya gegedu karibu na mwisho wa mifupa. Mifupa ya watoto inakua kutoka kwenye sahani za ukuaji.

Ugonjwa wa kuteleza kwa mfupa wa paja kwa kawaida unatokea katika umri wa balehe na kwa kawaida unawaathiri wavulana. Unene kupita kiasi mara nyingi ni sababu kubwa hatarishi. Watoto wengi ambao wanapata tatizo hili kwenye nyonga moja hatimaye wanaupata kwenye nyonga zote.

Ugonjwa wa Kuteleza kwa Mfupa wa Paja

Sababu za SCFE

Sababu ya ugonjwa wa kuteleza kwa mfupa wa paja haijulikani. Hata hivyo, tatizo hili kuna uwezekano mkubwa linatokana na kuwa dhaifu kwenye sahani ya ukuaji.

Udhaifu kwenye sahani ya ukuaji kunaweza kusababisha jeraha, ulemavu wa nyonga, matatizo kwa sababu ya unene kupita kiasi, mwako, au mabadiliko katika viwango vya homoni kwenye damu (kama vile viwango cha chini vya homoni ya dundumio), ambayo kwa kawaida hutokea wakati wa balehe (angalia Balehe kwa Wasichana pia angalia Balehe kwa Wavulana). Kuteleza husababisha sehemu ya juu ya mfupa wa paja kupoteza usambazaji wa damu, hatimaye unaoza na kuanguka.

Dalili za SCFE

Dalili ya kwanza ya ugonjwa wa kuteleza kwa mfupa wa paja unaweza kuwa mgumu au maumivu kidogo kwenye nyonga. Hata hivyo, maumivu yanaweza kuonekana kutoka kwenye goti au paja. Maumivu yanapungua kwa kupumzika na kuwa mabaya kwa kutembea au kuhamisha nyonga. Baadaye, kuchechemea kunatokea, kisha maumivu ya nyonga ambayo yanaenda hadi chini ya paja la ndani hadi kwenye goti. Mguu ulioathirika kwa kawaida hupinda kuelekea nje.

Utambuzi wa SCFE

  • Eksirei

  • Wakati mwingine upigaji picha kwa mwangwi wa sumaku (MRI) au kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti unahitajika

Utambuzi wa mapema wa ugonjwa wa kuteleza kwa mfupa wa paja ni muhimu kwa sababu matibabu yanakuwa magumu zaidi huleta matokeo ya kuridhisha kidogo baadaye.

Eksirei hufanywa kwa nyonga zote mbili. Eksirei ya nyonga iliyoathiriwa inaonyesha mtelezo au utengao wa kichwa cha mfupa wa paja kutoka kwenye sehemu ya mfupa iliyosalia.

Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti na MRI pia zinafaa, hasa endapo majibu ya eksirei yanaonyesha kuwa ni kawaida.

Matibabu ya SCFE

  • Upasuaji

Kwa kawaida upasuaji unahitajika ili kuoanaisha miisho iliyotenganishwa ya mfupa wa paja na kuikaza pamoja kwa skrubu za chuma.

Watoto hawapaswi kuweka uzito kwenye mguu ulioathiriwa hadi tatizo hilo liwe limetibiwa.