Ugonjwa wa kuziba kwa utumbo, Hirschsprung ni kasoro ya kuzaliwa ambapo sehemu ya utumbo mkubwa haunaa neva zinazothibiti mwendo wa kubana na kuachia wa utumbo. Dalili za kuziba kwa utumbo hutokea.
Kasoro hii huathiri sehemu za utumbo mpana ili usogezaji chakula kwa mwendo wa kubana na kuachia kawaida wa utumbo usitokee katika sehemu zilizoathiriwa.
Dalili za kawaida ni pamoja na kuchelewa kwa kinyesi cha kwanza (mekoniamu) kutoka kwa mtoto aliyetoka kuzaliwa, kutapika, kukataa kula, na tumbo kuvimba katika utoto wa baadaye.
Utambuzi huo unategemea kipande cha tishu (biopsi) ya puru kwaajili ya uchunguzi na kipimo cha presha ndani ya rektamu.
Upasuaji hufanywa ili kurejesha njia ya kawaida ya chakula kupitia matumbo.
Kasoro hii ya kuzaliwa hutokea kama neva za utumbo hazikuumbika vizuri wakati mtoto anapokua katika tumbo la uzazi. Mabadiliko fulani ya jeni yanaweza pia kuchangia katika ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung). Kasoro hii inaweza kutokea katika familia.
Baadhi ya watoto walio na ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung) wana matatizo mengine wakati ya kuzaliwa.
Utumbo mkubwa unategemea mtandao wa neva ndani ya kuta zake ili kusawazisha mikazo ya kubana na kuachia ili kusogeza vyakula vilivyomeng'enywa kuelekea kwenye tundu la haja kubwa, ambapo vitu hivyo hutolewa kama kinyesi. Katika ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung), sehemu ya utumbo iliyoathiriwa haiwezi kubana na kuachia kawaida. Bila kubana na kuachia huku kwa kawaida, vitu vilivyo ndani ya matumbo hujikusanya. Wakati mwingine, ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung) unaweza kusababisha uvimbe unaohatarisha maisha wa utumbo mpana (koloni) unaoitwa enterokolaitisi.
(Tazama pia Muhtasari wa Kasoro za Kuzaliwa Nazo za Njia ya Mmeng'enyo wa Chakula.)
Dalili za Ugonjwa wa Matatizo ya Utumbo Mkubwa Kupitisha Kinyesi
Watoto wengi wachanga walio na ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung) huwa na dalili mapema sana maishani. Hata hivyo, ikiwa sehemu ndogo tu ya utumbo imeathiriwa, mtoto anaweza kuwa na dalili zisizo kali na huenda asigunduliwe hadi baadaye utotoni au, mara chache, utu uzimani.
Kwa kawaida, karibu watoto wote wanaozaliwa hutoa mekoniamu (kinyesi cha kijani kibichi kinachochukuliwa kuwa haja kubwa ya kwanza) katika saa 24 za kwanza za maisha. Watoto wengi waliotoka kuzaliwa walio na ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung) hawapati choo cha kwanza (mekoniamu) katika masaa 48 ya kwanza ya maisha. Watoto waliotoka kuzaliwa walioathiriwa wanavimba tumbo na kutapika. Huenda wasiongeze uzito na kukua kama ilivyotarajiwa. Watoto wachanga walio na enterokolaitisi inayohusiana na Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung) wana homa ya ghafla, tumbo kuvimba, na kuhara kwa mlipuko na, wakati mwingine, kuhara damu.
Kwa watoto wachanga na watoto wakubwa, dalili zinaweza kujumuisha kukataa kula, kutojisikia kujisaidia, na kufunga choo.
Utambuzi wa Ugonjwa wa Matatizo ya Utumbo Mkubwa Kupitisha Kinyesi
Bariumu kwa njia ya haja kubwa
Biopsi ya puru
Kipimo cha presha kwenye rektamu
Mwanzoni, kipimo cha bariumu kwa njia ya haja kubwa hufanywa ili kutathmini kasoro. Wakati wa bariumu kwa njia ya haja kubwa, daktari huingiza bariumu na hewa ndani ya rektamu ya mtoto kisha huchukua eksirei. Bariamu ni majimaji yenye kutofautisha yanayoonesha weupe kwenye eksirei na kuonyesha njia ya mmeng'enyo wa chakula, na hivyo kurahisisha daktari kuona utumbo. (Madaktari hawafanyi bariumu kwa njia ya haja kubwa ikiwa wanashuku kuwa mtoto ana enterokolaitisi inayohusiana na Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung).)
Biopsi ya sehemu ya puru (kutolewa kwa kipande cha tishu kutoka kwenye rektamu kwa ajili ya uchunguzi kwenye hadubini) na kipimo cha presha ndani ya rektamu (manometry) ni vipimo vingine ambavyo madaktari hufanya ili kutambua ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung).
Madaktari wanaweza kufanya vipimo vya damu ikiwa wanafikiri mtoto ana mabadiliko ya kijenetiki.
Matibabu ya Ugonjwa wa Matatizo ya Utumbo Mkubwa Kupitisha Kinyesi
Upasuaji
Ugonjwa wa Kuziba kwa utumbo kwa kawaida hutibiwa kwa upasuaji ili kuondoa sehemu isiyo ya kawaida ya utumbo na kuunganisha utumbo wa kawaida na rektamu na tundu la haja kubwa. Kipindi cha upasuaji hutegemea ni kiasi gani cha utumbo wa mtoto umeathiriwa.
Hali mbaya sana ya ugonjwa wa kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung) lazima itibiwe haraka ili kupunguza hatari ya enterokolaitisi inayohusiana na Hirschsprung.
Watoto wanaopata ugonjwa wa ini unaohusishwa na kuziba kwa utumbo mpana (hirschsprung) hulazwa hospitalini ili kuwapa matumbo yao muda wa kupumzika na hupewa vitu vya majimaji na dawa za kuua bakteria kupitia mshipa. Kisha mrija mrefu na mwembamba hupitishwa kupitia pua na kuwekwa tumboni au utumbo (mrija wa nasogastriki) na mrija mwingine huwekwa kwenye rektamu (mrija wa rektamu). Kusudi kuu la mirija hii ni kupunguza shinikizo lililojikusanya kwa kuondoa majimaji na gesi. Wakati mwingine madaktari huingiza chumvichumvi kwenye rektamu ya mtoto ili kuosha kinyesi (huitwa unyweshaji wa rekatamu) ambacho kimejikusanya kwenye utumbo. Upasuaji hufanywa ili kuondoa sehemu ya utumbo ambayo haifanyi kazi.