Ruwaza ya mapigo ya moyo ya kijusi inafuatiliwa wakati wa uchungu wa kujifungua, kama njia moja ya kugundua ikiwa kijusi kipo kwenye msongo.
Kuanzia mapema mwanamke anapokuwa kwenye uchungu anapokuwa amepelekwa hospitalini, daktari au mtaalamu mwingine wa afya anafuatilia mapigo ya moyo ya kijusi ama kwa kipindi au kwa kuendelea. Kufuatilia mapigo ya moyo ya kijusi ni njia rahisi kabisa ya kujua endapo kijusi kinapokea oksijeni ya kutosha. Hali ya kutokuwa kawaida kwenye mapigo ya moyo (haraka sana au taratibu sana) na mabadiliko katika mapigo ya moyo (kadiri muda unavyokwenda na kwa kuitikia mikazo) inaweza kuonyesha kwamba kijusi kipo katika shida (shida ya kijusi).
Aina za Kipimo cha Mapigo ya Moyo ya Kijusi
Mapigo ya moyo ya kijusi yanaweza kufuatiliwa kwa njia zifuatazo:
Kwa nje: Fetoscope (aina ya stethoscope) au kifaa cha kupiga picha kwa mawambi ya sauti cha kushika kwa mkono (kinachotoa na kupokea mawimbi ya sauti) kinaweza kuwekwa kwenye tumbo la mwanamke kufuatilia mapigo ya moyo ya kijusi katika mwachano wa kawaida. Aina nyingine ya kifaa cha Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kinawekwa kwenye tumbo la mwanamke ili kufuatilia mapigo ya moyo kwa kuendelea. Vifaa ambavyo vinafanya ufuatiliaji kwa kuendelea (vinaitwa ufuatiliaji wa kijusi wa kielektroniki) kwa kawaida pia vina king'amuzi kinachoweza kufuatilia na kubaini mikazo.
Kwa ndani: Elektrodi (king'amuzi kidogo cha mviringo kinaunganishwa kwenye waya) kinaingizwa kwenye uke wa mwanamke kwenye ngozi ya kicha cha kijusi. Njia ya ndani inatumika hasi kukiwa kuna hatari ya matatizo wakati wa uchungu au wakati ambapo ishara zinanaswa na kifaa cha nje haziwezi kurekodiwa. Njia hii inaweza kutumiwa baada tu ya utando unaobeba kjusi umepasuka (inaelezwa kama "kuvunjika kwa maji").
Wakati ambapo ufuatiliaji wa kijusi wa kielektroniki huanza wakati wa uchungu wa kuzaa, mara nyingi kipimo cha kutokuwa na msongo hufanywa. Kipimo cha kutokuwa na msongo hutathmini mapigo ya moyo ya kijusi kwa dakika 20 hadi 40 ili kuangalia ruwaza mahususi. Matokeo yanachukuliwa kuwa ni mazuri au si mazuri. Ikiwa matokeo si mazuri, tathmini zaidi ya siha ya kijusi hufanywa, kama vile wasifu wa biofizikia.
Kwa wasifu wa biofizikia, ultrasonografia inatumika ili kuzalisha picha ya kijusi katika wakati halisi, na kijusi kinaangaliwa kwa hadi dakika 30. Madaktari wanatathmini mapigo ya moyo, kiwango cha majimaji ya amnioti, upumuaji wa kijusi na mjongeo, na kuweka alama ya hadi 10.
Kutokana na matokeo ya vipimo hivi, madaktari wanaweza kuruhusu uchungu uendelee au kujifungua kwa njia ya upasuaji.