Shida ya Fetasi

Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Jul 2025
v35612248_sw

Shida ya fetasi ni nini?

Kijusi ni mtoto ambaye bado yuko kwenye tumbo lako la uzazi (uterasi). Shida ya fetasi humaanisha mtoto hafanyi vizuri kabla au baada ya uchungu wa uzazi.

  • Hutokea hasa wakati mtoto hapokea oksijeni ya kutosha

  • Shida ya fetasi inaweza kutokea ambapo ujauzito utadumu kwa muda mrefu sana au kuna matatizo mengine

  • Madaktari wataona shida ya fetasi kwa kugundua mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au kukugeuza kwa upande mwingine

  • Madaktari wanatibu shida ya fetasi kwa kukupatia osijeni na majimaji au kwa kukugeuzia kwa upande mwingine

  • Madaktari huenda wakahitaji kumzalisha mtoto wako haraka sana

Mkazo kwa mtoto unaweza kusababisha mtoto kuvuta maji ya amnioti wakati anapovuta hewa ambayo yanajumuisha kiasi cha kinyesi cha mtoto (kinyesi hiki kinaitwa mekoni). Mtoto anayevuta mekoni anaweza kupumua kwa shida na wakati mwingine akaacha kupumua.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana shida ya fetasi?

Unapokuwa kwenye uchungu wa uzazi, daktari au mkunga anapima mapigo ya moyo wa mtoto wako. Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida kwenye tumbo ni ishara ya shida ya kijusi.

Je, madaktari hutibu vipi shida ya fetasi?

Madaktari wanatibu shida ya fetasi kwa:

  • Kukupa oksijeni

  • Kukupa kiowevu kwenye mshipa wako (IV)

  • Kukuweka upande wako

Ikiwa mtoto bado ana matatizo, mtoto huzaliwa haraka iwezekanavyo kwa njia ya upasuaji au mara chache kwa kifaa cha kuvuta mtoto au koleo la kumvuta mtoto.