Je, ugonjwa wa Marfan ni nini?
Ugonjwa wa Marfan ni ugonjwa ambao huathiri tishu unganishi za mwili. Tishu zinazounganisha ni pamoja na misuli, kano, gegedu, na sehemu zingine zinazoshikilia mifupa, vifundo, viungo, na tishu pamoja. Katika ugonjwa wa Marfan, tishu unganishi huwa dhaifu kuliko kawaida hivyo hutanuka, kuvimba, au kuchanika. Ugonjwa wa Marfan unaweza kusababisha matatizo yanayoathiri macho, moyo, na mapafu.
Ugonjwa wa Marfani ni ugonjwa wa kurithi katika familia.
Watu wenye ugonjwa wa Marfan huwa wanakuwa warefu sana na wembamba
Ugonjwa wa Marfan unaweza kuwa wa kawaida au mbaya sana
Watu wenye ugonjwa wa Marfan wanaweza kuwa na matatizo ya macho, moyo na mapafu
Tatizo kubwa zaidi litokanalo na ugonjwa wa Marfan ni shida ya mkole (mshipa mkubwa zaidi kwenye mwili)
Miaka kadhaa nyuma, watu wenye ugonjwa wa Marfan walikuwa na maisha mafupi, lakini kwa sasa watu wenye ugonjwa wa Marfan wanaishi hadi kufikisha umri wa miaka 70
Madaktari hawawezi kutibu ugonjwa wa Marfan, lakini wanaweza kutibu baadhi ya dalili zake
© Springer Science+Business Media
Ni nini husababisha ugonjwa wa Marfan?
Ugonjwa wa Marfan husababishwa na jeni zisizo za kawaida ambazo hutoka kwa mzazi mmoja.
Jeni huathiri jinsi mwili unavyounda protini fulani. Kwa kawaida, protini hii husaidia kuunda tishu unganishi ambazo ni imara. Katika watu wenye ugonjwa wa Marfan, tishu unganishi huwa dhaifu.
Je, dalili za ugonjwa wa Marfan ni zipi?
Dalili za ugonjwa wa Marfan zinaweza kuwa kiasi au kali. Watu wengi wenye ugonjwa wa Marfan hawana dalili yoyote. Baadhi hawana dalili wakiwa watoto lakini hupata dalili wanapokuwa watu wazima.
Watu wenye ugonjwa wa Marfan wanaweza kuwa na:
Urefu usio wa kawaida
Vidole na miguu mirefu, myembamba, huku urefu wa mikono yao ukizidi kimo chao
Mfupa wa kidari (mfupa wa kifua) wenye umbo lisilo la kawaida na huchomoza au kuzama ndani isivyo kawaida
Viungo vilivyolegea
miguu bapa
Magoti yanayopinda kuelekea nyuma
Mgongo unaopinda mbele isivyo kawaida katika sehemu ya juu ya mgongo (kifoskoliosisi)
Pia wanaweza kuwa na matatizo ya moyo, mapafu na macho kama vile:
Uvimbe kwenye mapafu
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa Marfan?
Iwapo madaktari watashuku kuwa una ugonjwa wa Marfan, watakuuliza kuhusu dalili zako na ikiwa familia yako ina historia ya uwepo wa ugonjwa wa Marfan. Watakufanyia uchunguzi wa kimwili na:
Wakati mwingine, kuchukua sampuli ya damu ili kupima jeni zako (upimaji wa jenetiki)
Ikiwa una ugonjwa wa Marfan, madaktari watachunguza moyo, mifupa na macho yako kwa kukufanyia vipimo vingine kama vile:
MRI (picha inayoonyesha sehemu ya ndani ya mwili wako)
Ekokadiografia (Upigaji picha wa moyo kwa kutumia mawimbi ya sauti)
Vipimo vya macho ili kuchunguza uwezo wako wa kuona
Eksirei
Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa Marfan?
Madaktari hawawezi kutibu ugonjwa wa Marfan. Ili kutibu baadhi ya dalili, wanaweza:
Andika dawa zinazoweza kufanya mtiririko wa damu upite kwa upole zaidi na kuzuia matatizo ya aorta
Kuwafanya watoto wavae mkanda wa kufunga mgongo ili kutibu hali ya mgongo kupinda kuliko kawaida (au wakati mwingine kufanya upasuaji wa kuurekebisha)
Fanya upasuaji wa moyo ili kurekebisha matatizo yoyote ya aorta au vali za moyo
Fanya upasuaji wa macho ili kurekebisha matatizo yoyote ya lenzi au retina
Madaktari watakagua mifupa, moyo na macho ya mtu kila mwaka ili kutibu tatizo lolote litokanalo na ugonjwa wa Marfan.