Virusi vya korona ni familia kubwa ya virusi vinavyosababisha magonjwa yaliyo katika kiwango cha mafua ya kwaida hadi nimonia hatari.
Kuna aina nyingi tofauti za virusi vya korona. Aina nyingi kati ya hizo husababisha magonjwa kwa wanyama.
Aina nne za maambukizi ya virusi kwa binadamu huhusisha magonjwa ya sehemu ya juu ya njia ya upumuaji ambayo husababisha dalili za mafua ya kawaida.
Hata hivyo, maambukizo ya aina 3 za virusi vya korona kwa binadamu vinaweza kuwa hatari zaidi na hivi karibuni vimesababisha milipuko mikubwa ya nimonia iliyosababisha vifo:
SARS-CoV-2 ni virusi vya kisasa vya korona ambavyo vilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2019 kama chanzo cha ugonjwa wa korona mwaka 2019 (COVID-19). MaambukizI haya yamejadiliwa sehemu nyingine (angalia COVID-19).
MERS-CoV vilitambuliwa mwaka 2012 kama chanzo cha ugonjwa upumuaji wa Mashariki ya kati (MERS).
SARS-CoV-1 vilitambuliwa mwaka 2003 kama chanzo cha mlipuko wa ugonjwa mkali wa mfumo wa upumuaji (SARS) ulioanza nchini Chinia karibu na mwishoni mwa mwaka 2002.
Virusi vya korona vinavyosababisha maambukizi makali ya mfumo wa upumuaji husambazwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (vimelea vya wanyama).
Ugonjwa wa Kupumua Mashariki ya Kati (MERS)
Ugonjwa wa mfumo wa upumuaji wa Mashariki ya kati ni maambukizi ya virusi vya korona vinavyosababisha dalili kali zinazolingana na mafua.
Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Mfumo wa Upumuaji wa Mashariki ya kati (MERS) ni virusi vya korona.
Virusi vya MERS vilitambuliwa kwa mara ya kwanza nchini Jordani na Saudia mwaka 2012. Kufikia mwaka 2021, kulikuwa na zaidi ya visa 2,500 vilivyothibitishwa vya MERS, pamoja na vifo 900 vilivyohusishwa na virusi hivyo. Zaidi vilitokea Saudia, ambapo visa vipya vinaendelea kutokea. Mlipuko mkubwa unaofahamika wa MERS nje ya Peninsula ya Uarabuni ulitokea Jamhuri ya Korea mwaka 2015. Mlipuko huo ulihusishwa na msafiri aliyerejea kutoka Peninsula ya Urabuni. Visa pia vimetokea katika nchi zilizoko Ulaya, Asia, Afrika Kaskazini, Mashariki ya kati na Marekani kwa watu ambao walihamishiwa huko ili kupata matibabu au waliugua baada ya kurejea kutoka Mashariki ya kati. Visa vya makundi tu ndivyo vimeripotiwa tangu mwaka 2019.
Katika baadhi ya nchi huko Mashariki ya Kati, ngamia warefu wanashukiwa kuwa chanzo kikuu cha maambukizi kwa watu, lakini jinsi gani virusi hivyo vinasambaa kutoka kwa ngamia kwenda kwa watu haijulikani.
Maambukizi yanatokea zaidi kwa wanaume na ni makali zaidi kw wazee na watu walio na matatizo sugu kama vile kisukari au moyo au figo. Maambukizi yamekuwa mabaya kwa takribani theluthi moja ya watu walioambukizwa.
Virusi vya MERS husambazwa kwa kugusana kwa ukaribu na watu walio na MERS au kupitia matone kwa njia ya hewa ambayo yametoka kwa mtu aliyeambukizwa kwa kukohoa au kupiga chafya. Inaaminika kuwa watu hawawezi kuambukiza hadi dalili zionekane. Visa vingi vya uambukizaji kati ya binadamu vimetokea kwa wahudumu wa afya wanaowatibu watu walioambukizwa.
Kwa kawaida dalili zinaonekana takribani baada ya siku 5 (lakinisiku yoyote kuanzia siku 2 hadi siku 14) baada ya watu kuambukizwa. Watu wengi hupata homa, kuhisi baridi, maumivu ya misuli na kukohoa. Takribani theluthi moja huwa na dalili za kuharisha, kutapika na maumivu ya tumbo.
Utambuzi wa MERS
Kupima majimaji ya njia ya upumuaji
Vipimo vya damu
Madaktari hushuku MERS kwa watu ambao wana maambukizi ya njia ya chini ya upumuaji na ambao wamesafiri au kuishi katika maeneo ambako huenda wamekumbana na virusi au wale waliogusana kwa ukaribu sana na mtu ambaye anaweza kuwa na virusi vya MERS.
Ili kutambua virusi vya MERS, madaktari wanachukua sampuli za majimaji kutoka kadhaa katika njia ya upumuaji katika wakato tofauti na kupima ili kubaini ikiwa yana virusi. Pia hufanya vipimo vya damu ili kutambua virusi au kingamwili. Vipimo vya damu hufanyika kwa watu ambao wamegusana kwa ukaribu na mtu ambaye huenda ana virusi vya MERS.
Matibabu ya MERS
Dawa za kutuliza homa na maumivu ya misuli
Kujitenga
Hakuna matibabu mahususi ya virusi vya MERS. Acetaminophen au dawa ya kupunguza uvimbe isiyo na steroidi (NSAID) kama vile ibuprofeni hutolewa ili kutuliza homa na maumivu ya misuli.
Tahadhari huchukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi. Kwa mfano, mtu hutengwa katika chumba chenye mfumo wa hewa safi ambayo inazuia kusambaza kwa vimelea katika hewa. Watu wanaoingia katika chumba hicho sharti wavae barakoa maalum, kinga ya macho na vazi refu pamoja na glovu. Milango ya chumba hicho inapaswa kusalia ikiwa imefungwa isipokuwa watu wanapoingia na kutoka mara chache iwezekanavyo.
Ugonjwa Mkali wa Mfumo wa Upumuaji (SARS)
Ugonjwa mkali wa mfumo wa upumuaji ni maambukizi ya virusi vya korona ambavyo vinasababisha dalili zinazolingana na mafua.
Hakuna matukio yameripotiwa kote duniani tangu 2004.
Dalili za SARS zinalingana na zile nyingine za kawaida za virusi maambukizi ya njia ya upumuaji (kama vile homa, maumivu ya kichwa, kuhisi baridi na maumivu ya misuli) lakini ni makali zaidi, hasa miongoni mwa wazee.
Madaktari wanashuku virusi vya SARS ikiwa tu mtu amekumbana na mtu aliyeathiriwa.
Ikiwa madaktari wanafikiri mtu anaweza kuwa na SARS, mtu huyo hutengwa katika chumba na mfumo wa uingizaji hewa unaozuia kuenea kwa viumbe vidogo zaidi katika hewa.
(Tazama pia Muhtasari wa Maambukizi ya Virusi.)
Ugonjwa Mkali wa Mfumo wa Upumuaji (SARS) ulitambuliwa kwa mara kwanza nchini Uchina mwishoni mwa mwaka 2002. Mlipuko wa ulimwenguni ulitokea, hali iliyopelekea zaidi visa 8,000 ulimwenguni kote ikiwa ni pamoja Kanada na Marekani na takribani vifo 800 katikati ya mwaka 2003. Hakuna matukio yameripotiwa kote duniani tangu 2004.
Ingawa hakuna visa vipya ambavyo vimeripotiwa tangu 2004, SARS inachukuliwa kuwa imeondolewa kwa sababu virusi vina masalia madogo ambavyo kupitia mabaki hayo vinaweza kuibuka upya.
Chanzo cha haraka kilihisiwa kuwa vipepe, mamalia wanaolingana na paka, ambao waliuzwa kwenye masoko ya wanyama kama chakula cha kipekee. Jinsi ambavyo vipepeo hao waliambukizwa haifahamiki, ingawa inadhaniwa kuwa inawezekana popo wamebeba virusi vya SARS kiasili.
SARS inasababishwa na virusi vya korona. SARS ni vikali zaidi kuliko aina nyingine zaidi za maambukizi ya virusi vya korona, ambavyo kwa kawaida husababisha dalili zinazolingana na mafua. Hata hivyo, Ugonjwa wa Upumuaji wa Mashariki ya Kati (MERS) na COVID-19 ni magonjwa mengine makali yanayosababishwa na virusi vya korona.
Virusi vya SARS husambazwa kwa kugusana kwa ukaribu na mtu aliyeambukizwa au kupitia matone kwa njia ya hewa ambayo yametoka kwa mtu aliyeambukizwa kwa kukohoa au kupiga chafya.
Dalili za SARS
Dalili za SARS hulingana na zile za maambukizi ya kawaida zaidi ya virusi vinavyoathiri njia ya upumuaji lakini ni kali zaidi. Hujumuisha homa, maumivu ya kichwa, kuhisi baridi na maumivu ya misuli, ikifuatiwa na kikohozi kikavu na wakati mwingine kupumua kwa shida.
Watu wengi hupona ndani ya wiki 1 hadi 2. Hata hivyo, baadhi walionyesha dalili za kupumua kwa shida na takribani asilimia 10 walikufa.
Utambuzi wa SARS
Tathmini ya daktari
Vipimo vya kutambua virusi
SARS hushukiwa ikiwa tu kuna uwezekano kuwa watu wamekumbana na mtu aliyeambukizwa, kuwa na homa pamoja na kupumua kwa shida.
Vipimo vinaweza kufanya ili kutambua virusi.
Matibabu ya SARS
Kujitenga
Ikihitajika, oksijeni
Wakati mwingine vipitisha hewa ili kusaidia kupumua
Ikiwa madaktari wanafikiri mtu anaweza kuwa na SARS, mtu huyo hutengwa katika chumba na mfumo wa uingizaji hewa unaozuia kuenea kwa viumbe vidogo zaidi katika hewa. Katika mlipuko pekee na wa kwanza wa SARS, hatua hiyo ya kutenga ilizuia virusi kusambazwa na hatimaye kuviondoa.
Watu walio na dalili ndogo hawahitaji matibabu mahususi. Wale walio na shida ya wastani ya kupumua kwa shida wanaweza kuhitaji kupewa oksijeni. Wale wanaokumbwa na shida ya kupumua wabaweza kuhitaji kupumua kwa kutumia na mashine ili kusaidia kupumua.