Mafua ya Kawaida

NaSophie Katz, MD, MPH, Vanderbilt University Medical Center
Imekaguliwa naBrenda L. Tesini, MD, University of Rochester School of Medicine and Dentistry
Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024 | Imebadilishwa Apr 2025
v788422_sw

Mafua ya kawaida ni maambukizi ya virusi ya utando wa pua, sanasi na koo.

  • Virusi vingi tofauti husababisha mafua.

  • Kwa kawaida, mafua huenea mikono ya mtu inapogusana na majimaji ya puani kutoka kwa mtu aliyeambukizwa.

  • Mafua mara nyingi huanza na koo linalowasha au kuuma au usumbufu puani, ikifuatiwa na kupiga chafya, pua zinazotoa makamasi, kikohozi, na hisia ya jumla ya ugonjwa.

  • Madaktari huhusisha utambuzi wa ugonjwa kulingana na dalili.

  • Usafi mzuri, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara, ndiyo njia bora ya kuzuia mafua.

  • Kupumzika, dawa za kupunguza msongamano wa damu, acetaminopheni, na dawa ya kupunguza uvimbe isiyo na asteroidi (NSAID, kama vile ibuprofeni) zinaweza kusaidia kupunguza dalili.

Mafua ya kawaida ni miongoni mwa magonjwa ya kawaida. Virusi vingi tofauti (rhinoviruses, adenovirusi, coronaviruses, na human metapneumoviruses) husababisha mafua, lakini rhinoviruses (ambavyo kuna aina zaidi ya 100) husababisha mafua mengi. Mafua yanayosababishwa na rhinoviruses hutokea kwa kawaida zaidi katika majira ya kuchipua na vuli. Virusi vingine husababisha magonjwa kama mafua ya kawaida wakati mwingine wa mwaka.

Mafua huenea hasa wakati mikono ya watu inapogusana na majimaji ya puani kutoka kwa mtu aliyeambukizwa. Viowevu hivi vina virusi vya mafua. Watu wanapogusa midomo yao, pua, au macho, virusi huingia mwilini na kusababisha mafua. Mara chache, mafua huenea watu wanapovuta hewa yenye matone ambayo mtu amekohoa au kupigwa chafya na mtu aliyeambukizwa. Mafua huambukiza zaidi wakati wa siku 1 au 2 za kwanza baada ya dalili kutokea.

Urahisi wa kupata mafua hauongezeki kutokana namambo yoyote kati ya yafuatayo:

  • Kufiduliwa kwa baridi

  • Afya ya jumla na tabia za kula

  • Kuwa na kasoro katika pua au koo (kama vile findo iliyopanuka au adenoidi)findo iliyopanuka

Je, Ulijua...

  • Kuhisi baridi hakusababishi mafua au kuwafanya watu waweze kupata mafua.

Dalili za Mafua ya Kawaida

Dalili za mafua huanza kati ya siku 1 hadi 3 baada ya maambukizi. Kwa kawaida, dalili za kwanza ni kujikuna au kuumwa na koo au maumivu kwenye pua. Baadaye, watu huanza kupiga chafya, kuwa na pua zinazotoa kamasi na kuhisi homa kiasi. Homa si kawaida, lakini huenda ikatokea homa kiasi mafua yanapoanza. Mara ya kwanza, kamasi zinazotoka puani huwa nyepesi na nyeupe na zinaweza kuwa nyingi, lakini baadaye huwa nzito, hubadilika rangi, huwa na rangi ya kijani manjano kisha hupungua. Watu wengi pia hupata kikohozi cha wastani. Kwa kawaida dalili huonekana katika siku 4 hadi 10, ingawa mara nyingi kikohozi hudumu hadi wiki ya pili.

Maradhi yanaweza kusababisha ugonjwa uendelee. Mara nyingi virusi vya rhino husababisha mashambulio ya pumu kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa pumu. Baadhi ya watu hupata maambukizi ya bakteria ya sikio la kati (kuvimba sehemu ya kati ya sikio) au sinasi (uvimbe puani). Maambukizi haya hutokea kwa sababu kuwepo kwa kamasi nyingi puani huzuia mtiririko wa kawaida sehemu hizo, hali inayoruhusu bakteria kukua katika mkusanyiko wa kamasi zilizozuia.

Je, Ulijua...

  • Viua vijasumu havifai katika kutibu mafua. Kutumia viua vijasumu ili kutibu virusi kunaweza kusababisha madhara yasiyo ya lazima ya dawa kwa mtu anayezitumia na kupelekea kuwepo bakteria sugu dhidi ya viua vijasumu.

Utambuzi wa Mafua ya Kawaida

  • Tathmini ya daktari

Mara nyingi madaktari wanaweza kutambua mafua kutokana na dalili za kawaida. Homa kali, maumivu makali ya kichwa, upele, kupumua kwa shida au maumivu ya kifua hubainisha kuwa maambukizi hayo si mafua ya kawaida.

Mara nyingi vipimo vya maabara havihitajiki kutambua mafua. Ikiwa madaktari wanahisi ugonjwa, wanaweza kuagiza vipimo vya damu na eksirei.

Matibabu ya Mafua ya Kawaida

  • Pumzika nyumbani ili kuzuia kusambaza kwa wengine

  • Kunywa viowevu vingi

  • Ikihitajika, tumia dawa za kawaida za kutuliza dalili

Watu wenye mafua wanapaswa kujikinga na baridi, kukaa sehemu inayofaa na kupumzika. Wanapaswa kujaribu kuepuka kusambaza maambukizi kwa wengine kwa kusalia nyumbani. Kunywa maji au kutumia kifaa cha kuongeza hewa ya unyevu kunaweza kusaidia kiasi kupunguza ukali wa kamasi na kufanya iwe rahisi kuzitoa. Vitoa mvuke vinavyotoa mvuke wa uvuguvugu vinaweza kusababisha kuungua ikiwa mtu atavikaribia au kugusa kwa bahati mbaya kifaa hicho kilicho na maji ya moto.

Dawa zilizopo sasa za kutibu maradhi ya virusi hazifai katika kudhibiti mafua. Viua vijasumu hazisaidii watu wenye mafua, hata kama kuna kamasi nzito puani au kikohozi. Kutumia antibayotiki wakati ambapo haihitajiki kunaweza kusababisha madhara ya dawa yasiyo ya lazima na kupelekea kuwepo kwa bakteria sugu dhidi ya antibayotiki.

Matumizi ya Echinacea, zinki na vitamini C zinashauriwa kutumika kama tiba. Baadhi ya tafiti ndogo zimeonyesha kuwa tiba hizo zinafaa. Nyinginezo zimeonyesha kuwa hazifai. Lakini hakuna tafiti kubwa, zenye mpango thabiti za kimatibabu zilizothibitisha ufanisi wake. Hata kama tafiti zimeonyesha manufaa, manufaa hayo yalikuwa madogo. Kwa mfano, wakati zinki ilipunguza muda wa dalili za mafua, ilionekana kupunguza kwa siku isiyozidi 1. Pia, vidonge vya zinki vinaweza kusababisha uchachu kinywani na kichefuchefu na kinyunyizi cha puani cha zinki kinaweza kusababisha kupoteza kabisa uwezo wa kuhisi harufu. Kwa hivyo, wataalamu wengi hawapendekezi dawa au tiba hizi.

Dawa za maarufu zisizoandikwa na daktari (dawa za kawaida) husaidia kupunguza dalili za mafua. Kwa sababu hazitibu maambukizi, ambayo kwa kawaida huisha baada ya wiki bila kujali iikiwa dawa zimetumika, madaktari wanaamini matumizi yake si lazima, kulingana na hali ambayo mtu anahisi. Aina kadhaa tofauti za dawa zinatumika:

  • Dawa za kuzibua njia za pua, mbazo husaidia kufungua mianzi ya pua iliyoziba

  • Antihistamini, ambazo zinaweza kusaidia kukauka kamasi

  • Kinyunyizi chenye chumvi cha puani, ambazo husaidia kulainisha kamasi

  • Dawa za kupunguza kuvimba zisizo na steroidi (NSAID) au acetaminophen, ambazo zinaweza kupunguza maumivu na kutuliza homa

  • Shira ya kikohozi, ambayo hupunguza ukali wa kikohozi kwa kukifanya kiwe chepesi na kulainisha (vidhibiti kikohozi) au ambazo zinaweza kukomesha kikohozi (viondoa kikohozi au shira)

Dawa hizi mara nyingi huuzwa kama muunganiko lakini pia zinaweza kupatikana kama moja.

Dawa za kuzibua njia za pua za kuvuta zinafaa zaidi kuliko vidongea ambavyo mtu humeza kupitia mdomo ili kuzibua njia za pua. Hata hivyo, kutumia dawa za kuvuta kwa zaidi ya siku 3 hadi 5, kisha kuacha, kunaweza kuzidisha hali ya pua kuziba kuliko ilivyokuwa hapo awali. Ipratropiamu, kinyunyizi cha puani kichonapatikana tu kwa kuandikiwa na daktari, husaidia kukausha kamasi.

Antihistamini za zamani kama vile klofeniramini, zinaweza kusababisha hali ya kusinzia. Antihistamini za kisasa, kama vile loratadine zina uwezekano mdogo sana wa kusababisha hali ya usingizi lakini hazina ufanisi wa kutibu mafua ya kawaida.

Dawa za kuzibua njia za pua na antihistamini hazipaswi kutumiwa na watoto walio na umri wa chini ya miaka 4.

Dawa za kupunguza uvimbe zisizo na steroidi (NSAID), kama vile aspirini, ibuprofen na naproxen zinaweza kupunguza maumivu na kutuliza homa, sawa na acetaminophen. Aspirini haipendekezwi kabisa kwa watototo kwa sababu, inawaongezea hatari ya kupata Ugonjwa wa Reye, ambao si rahisi lakini ni tatizo la kutishia maisha.

Vidhibiti kikohozi hazipendekezwi kutumiwa mara kwa mara kwa sababu kukohoa njia nzuri ya kuondoa kikohozi na uchafu katika njia za hewa wakati wa maambukizi ya virusi. Hata hivyo, kikohozi kikali ambacho kinakatiza usingizi au kusababisha hali isiyo ya kawaida kinaweza kutibiwa na dawa za kudhibiti kikohozi.

Jedwali
Jedwali

Uzuiaji wa Mafua ya Kawaida

Kwa sababu aina nyingi tofauti za virusi zinasababisha mafua na kwa kuwa kila aina ya virusi inabadilika taratibu kadiri muda unavyosonga, hakuna chanjo ya kudhibiti mafua ya kawaida.

Hatua bora ya kuzuia ni kufanya usafi mzuri. Kwa sababu aina nyingi za virusi zinasambaa kwa kugusa majimaji ya mwili wa aliyeambukizwa, hatua zifuatazo zinaweza kusaidia:

  • Watu wenye dalili za mafua na watu walioko nyumbani pamoja na ofisini wanapaswa kunawa mikono yako mara kwa mara.

  • Wanapaswa kupiga chafya na kukohoa kwenye tishu, ambayo inapaswa kutupwa kwa umakini.

  • Ikiwezekana, watu wenye dalili wanaaswa kulala katika chumba tofauti.

  • Watu wanaokohoa au kupicha chafya kwa sababu ya mafua hawapaswi kwenda kazini au shuleni au katika hali ambapo wanaweza kuwaambukiza wengine.

  • Kusafisha vifaa na sehemu zinazotumiwa pamoja kwa kutumia dawa ya kuangamiza vijidudu kunaweza pia kusaidia kupunguza kusambaa kwa virusi vya mafua ya kawaida.

Licha ya kuwa maarufu, echinacea, zinki na vitamini C hazizuii au kutibu mafua wala kula matunda ya jamii ya machungwa.