Giardiasis

NaChelsea Marie, PhD, University of Virginia;
William A. Petri, Jr, MD, PhD, University of Virginia School of Medicine
Imekaguliwa naChristina A. Muzny, MD, MSPH, Division of Infectious Diseases, University of Alabama at Birmingham
Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024 | Imebadilishwa Jan 2025
v786737_sw

Giardiasis ni maambukizi ya utumbo mdogo yanayosababishwa na kimelea cha seli moja cha protozoa Giardia. Dalili kuu ni maumivu ya tumbo na kuhara.

  • Watu wanaweza kuwa na mikazo ya tumbo, gesi, teuka, kuhara na kichefuchefu na kuhisi kuchoka.

  • Watu wanapata maambukizi kwa kunywa maji au kula chakula ambacho kina vimelea vya Giardia au kwa kugusana na kinyesi kutoka kwa mtu mwenye maambukizi.

  • Madaktari wanatambua maambukizi kwa kupima au kuchunguza sampuli ya kinyesi.

  • Watu walioambukiza wanatibiwa na dawa ya kuua vimelea, kama vile tinidazole, metronidazole, secnidazole, au nitazoxanide kwa kunywa kwa mdomo.

  • Kuchemsha maji kunaua protozoa Giardia na ni njia salama kabisa kwa watembeaji milimani kuhakikisha kwamba maji kutoka kwenye vijito na maziwa yapo salama kwa kunywa.

(Angalia pia Muhtasari wa Maambukizi ya Vimelea.)

Giardiasis ni maambukizi ya protozoa yanayotokea duniani kote na maambukizi ya vimelea kenye utumbo yaliyoenea zaidi nchini Marekani. Protozoa Giardia inaweza kuunda ganda la nje (linaloitwa uvimbe). Linawawezesha kuishi nje ya mwili kwa vipindi virefu (kwa mfano, kwenye maziwa na kwen ye vijito) na kuwafanya wasiweze kuuliwa na klorini (kwa mfano, kwenye mabawa ya kuogelea). Uvimbe huu unapita kwenye kinyesi na unaweza kusababisha maambukizi.

Protozoa Giardia protozoa ni vimelea vinavyopatikana sana kwenye maji baridi, ikiwa ni pamoja na maziwa na vijito vingi, na hata vile vinavyoonekana kuwa safi. Maji ya manispaa ambayo hayajachujwa vizuri huchangia baadhi ya milipuko. Watu wengi wanapata maambukizi kwa kunywa maji yenye vimelea. Lakini watu wanaweza kupata maambukizi ikiwa watakula chakula chenye vimelea au wamegusa kinyesi kutoka kwa mtu mwenye maambukizi, hali inayoweza kutokea kati ya watoto au wenzi wa ngono.

Giardiasis hupatikana sana miongoni mwa

  • Watoto kwenye vituo vya kulelea watoto

  • Watu ambao wanafanya ngono ya mdomoni na sehemu ya haja kubwa

  • Watu ambao wamesafiri kwenda kwenye nchi zenye usafi duni

  • Watembea milimani wanaokunywa maji ya vijito na kwenye maziwa

  • Watu wanaoogelea kwenye mabwawa au maziwa yenye vimelea

Giardia wanaweza kuishi kwa wanyama wa mwituni.

Je, Ulijua...

  • Giardiasis wanaweza kupatikana kwenye maziwa na vijito vinavyoonekana safi na maji yake hayana chumvi.

Dalili za Giardiasisi

Baadhi ya watu wenye maambukizi hawana dalili, lakini watu hawa wanaweza kupitisha uvimbe wa Giardia kwenye kinyesi chao na hivyo kuwaambukiza wengine. Dalili, zinapotokea, hutokea karibu wiki 1 hadi 2 baada ya maambukizi.

Dalili za giardiasis kwa kawaida hujumuisha mikazo ya tumbo, gesi, teuka na maharisho ya majimaji yenye harufu mbaya. Kichefuchefu kinaweza kuja na kuondoka. Watu wanaweza kuhisi kuchoka na kutojisikia vizuri na kupoteza hamu ya chakula. Isipotibiwa, kuharisha kunaweza kudumu kwa wiki kadhaa. Watu wenye giardiasis mara nyingi huleta kutovumilia maziwa (kutokuwa na uwezo wa kumeng'enya maziwa, sukari kwenye maziwa), jambo ambalo linaweza kusababisha kuhara, gesi na kuvimba tumbo.

Watu wachache wenye giardiasis wanakuwa na hali ya kuhara inayodumu kwa muda mrefu. Watu hawa wanaweza wasifonze virutuisho vya kutosha kutoka kwenye chakula (huitwa hali ya kushindwa kunyonya virutubishi), inayotokana na kupoteza uzito kwa kiasi kikubwa.

Mara chache, giardiasis sugu huzuia watoto wasikue kama inavyotarajiwa (hali inayoitwa kushindwa kustawi).

Utambuzi wa ugonjwa wa Giardiasisi

  • Vipimo vya kinyesi

Dalili mara nyingi zinaonyesha giardiasis.

Njia rahisi kabisa ya kufanya vipimo vya giardiasis ni kwa kupima kinyesi kuona kama kuna protini (antijeni) inayotolewa na Giardia lamblia kuona DNA yake.

Uchunguzi wa hadubini wa sampuli za kinyesi unaweza pia kugundua kimelea. Hata hivyo, kwa sababu watu ambao wameambukizwa kwa muda mrefu huwa wanatoa vimelea hivyo kwa mwachano usiotabirika, uchunguzi wa kurudia wa hadubini wa kinyesi mara nyingi huhitajika.

Ikiwa vipimo hivi havibainishi kile kinachosababisha dalili za utumbo, madaktari wanaweza kutumia neli jongevu ya kutazamia (endoscope) kuchunguza sehemu ya juu ya njia ya mmeng'enyo wa chakula, ikiwa ni pamoja na sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (dodenamu). Madaktari wanaweza kutumia utaratibu huu kupata sampuli ya tishu za utumbo mdogo kwa ajili ya uchunguzi.

Matibabu ya Giardiasisi

  • Tinidazole, metronidazole, secnidazole, au nitazoxanide

Watu walioambukizwa wenye dalili wanaweza kutibiwa na tinidazole, metronidazole, secnidazole, au nitazoxanide, kwa kumeza mdomoni.

Tinidazole, ikitumiwa katika dozi moja, ina madhara machache kuliko metronidazole, ambayo inatumiwa kwa siku 5 hadi 7.

Secnidazole inamwezwa kwa mdomo kama dozi moja.

Nitazoxanide inapatikana ikiwa katika kimiminika, ambayo inafaa kwa watoto na kama tembe. Inatumiwa kwa siku 3. Ina madhara machache.

Hata baada ya kutibu maambukizi, watu wanaweza kupitia hali ya kutovumilia maziwa au ugonjwa wa matumbo kuwasha. Kuepuka bidhaa za maziwa kunasaidia kwa watu ambao wamekuwa na hali ya kutovumilia maziwa.

Uzuiaji wa Giardiasisi

Kuzuia Giardiasis kunahitaji

  • Matibabu yanayofaa ya maji yanayotumiwa na umma (ikiwa ni pamoja na maji ya kwenye mabwawa ya kuogelea)

  • Kuwa na usafi bora wakati wa kuandaa chakula

  • Usafi bora binasi (kwa mfano, kunawa mikono kwa kina baada ya kutumia choo).

  • Kuepuka kugusana na kinyesi wakati wa kushiriki ngono

Kuchemsha maji kunaua vimelea na ni njia salama kabisa kwa watembea milimani ili kuhakikisha kwamba maji kutoka kwenye vijito na maziwa ni salama kwa ajili ya kunywa.

Maji kutoka kwenye vijito na maziwa wakati mwingine yanaweza kutibiwa kuondolewa vimelea kwa kutumia klorini au iodini. Mbinu hii haitegemeki sana kwa sababu ufanisi wake unatofautiana kutegemea na ni kwa kiasi gani maji yana vumbi au tope na halijoto ya maji ikoje. Kiwango cha klorini kinachotumika mara kwa mara kwenye maji ya kunwa huenda kisitoshe kuua uvimbe.

Vichujio vya maji ambavyo vinatumia osmosisi rejea vina maneno "kimepimwa na kuthibitishwa na NSF/ANSI Kiwango Na. 53 au Na. 58 kwa ajili ya kuondoa/kupunguza mayai ya vimelea" vya Giardia na protozoa wengine vilevile bakteria kutoka kwenye maji, lakini mifumo mingine ya kuchuja huenda isiwe na ufanisi.

(Angalia pia Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa [CDC]: Vimelea - Giardia: Kuzuia na kudhibiti na Kitabu cha Njano cha CDC: Giardiasisi).

Taarifa Zaidi

Nyenzo zifuatazo za lugha ya Kiingereza zinaweza kuwa muhimu. Tafadhali kumbuka kuwa Mwongozo hauwajibiki kwa maudhui ya nyenzo hizi.

  1. Schnell K, Collier S, Derado G, na wengine: Giardiasisi nchini Marekani, uchmbuzi wa kiepidemiolojia na kijiografia wa data za kiwango cha nchi ya maji ya kunya na usafi, 1993-2010. J Water Health 14(2):267–279, 2016. doi: 10.2166/wh.2015.283