Sistoisosporiasisi ni maambukizi ya kimelea Sitoisospora (Isospora) belli. Dalili kuu ni kuhara kwa maji na mikakamao ya tumbo na kichefuchefu.
Watu wanaweza kuambukizwa Cystoisospora kwa kula chakula au kunywa maji yenye vimelea.
Dalili za Cystoisosporiasis ni mbaya zaidi na za muda mrefu kwa watu wenye mfumo wa kingamwili dhaifu, kama vile watu wenye VVU.
Dalili hutofautiana lakini ni pamoja na kuhara maji mengi, mikakamao ya tumbo, homa, na kupunguza uzito.
Madaktari kwa kawaida wanatambua maambukizi kwa kubainisha Cystoisospora kwenye sampuli ya kinyesi.
Cystoisosporiasis inaweza kutibiwa na trimethoprim/sulfamethoxazole (TMP/SMX).
(Angalia pia Muhtasari wa Maambukizi ya Vimelea.)
Cystoisosporiasis inapatikana sana kwenye hali ya hewa ya kitropiki na nusutropiki.
Cystoisospora belli oocysts are not sporulated (ie, infective) when passed in stool. Thus, direct fecal-oral transmission does not occur.
1. Immature oocysts are excreted in stool. Each oocyst usually contains one sporoblast. The sporoblast divides in two and secretes a cyst wall, becoming 2 sporocysts. The sporocysts divide and produce sporozoites.
2. Oocysts are ingested and excyst. Sporozoites are released and invade the epithelial cells.
3-5. Inside the cells, they multiply asexually. After at least one week, male and female gametocytes develop. Fertilization results in oocysts, which are shed in stool.
Image from the Centers for Disease Control and Prevention Image Library.
Dalili za Sistoisosporiasisi
Dalili ya kwanza ya cystoisosporiasis ni kuhara kwa ghafula kusiko na damu, kwa majimaji. Dalili zingine zinajumuisha homa, mikazo ya tumbo, kichefuchefu, uchovu, na kupunguza uzito. Dalili kwa watu wenye mfumo wa kinga mwili wa kawaida kwa kawaida hudumu kwa wiki kadhaa, kusha hutoweka.
Kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kingamwili, ikiwa ni pamoja na watu wenye VVU iliyo katika hatua za mwisho, cystoisosporiasis inaweza kusababisha hali mbaya ya kuharisha ambayo inaweza kudumu kwa muda mrefu.
Utambuzi wa Ugonjwa wa Sistoisosporiasisi
Vipimo vya kinyesi
Ili kutambua cystoisosporiasis, sampuli ya kinyesi inachunguzwa kwa hadubini ili kuona mayai ya Cystoisospora. Mbinu maalum zinaweza kutumika kuongeza nafasi za kutambua mayai.
Uchanganuzi wa kinyesi unapokuwa haubainishi chanzo cha kuharisha kusikokoma, madaktari wanaweza kutumia neli jongevu ya kutazamia (endoscope) ili kuchunguza sehemu ya juu ua njia ya mmeng'enyo wa chakula. Madaktari wanaweza kutumia utaratibu huu kupata sampuli ya tishu ili kuchunguzwa na kuchanganuliwa (bayopsi). Cystoisospora, ikiwa ipo, inaweza kuonekana kwenye kipande cha tishu kutoka kwenye utumbo.
Matibabu ya Sistoisosporiasisi
Trimethoprim/sulfamethoxazole (TMP/SMX)
Watu wenye maambukizi wenye dalili wanaweza kutibiwa kwa TMP/SMX kwa kumeza kwa mdomo.
Watu wenye VVU, ni muhimu sana kutibu maambukizi ya VVU kwa ufanisi kadiri iwezekanavyo kwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI. Matibabu kama hayo yanaweza kuimarisha mfumo dhaifu wa kingamwili, ambao kwa kawaida husaidia kudhibiti kuhara na dalili nyingine. Watu wenye VVU ya hatua ya mwisho wanaweza kuhitaji dozi ya juu ya TMP/SMX na matibabu ya muda mrefu. Wakati mwingine tiba ya kukarabati ya muda mrefu ya TMP/SMX inahitajika kwa watu wenye VVU ili kuzuia kurudia tena.
Kwa sistoisosporiasisi, watu wenye mzio wa TMP/SMX wanaweza kutibiwa kwa pyrimethamine. Leucovorin inatolewa ili kuzuia upungufu wa damu na idadi ya chini ya seli nyeupe za damu, ambayo ni madhara ya pyrimethamine.
Ciprofloxacin imekuwa ikitumiwa kutibu cystoisosporiasis, lakini ina ufanisi kidogo kuliko TMP/SMX.
Uzuiaji wa Sistoisosporiasisi
Kuzuia ni kwa kunawa mikono na tahadhari za chakula na maji.
Unaposafiri kwenda kwenye maeneo yenye hali ya hewa ya kitropiki na nusutropiki ambapo maambukizi yameenea, watu wanapaswa kuepuka kula vyakula ambavyo havijapikwa, ikiwa ni pamoja na saladi na mboga za majani, na wanapaswa kuepuka kutumia maji au barafu ambayo imechafuliwa. Kunawa mikono kwa sabuni na maji ni muhimu. Kunywa maji ambayo yamechemshwa ni salama. Kuchuja maji kupitia kichujio cha mikroni 0.1 au 0.4 kunaweza kuondoa mayai ya Cystoisospora na vimelea vingine, vilevile bakteria inayoweza kusababisha magonjwa. Mapendekezo ya kina kwa wasafiri wa kimataifa yanapatikana kwenye Kitabu cha Njano cha Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC): Tahadhari za Chakula na Maji.
Taarifa Zaidi
Nyenzo zifuatazo za lugha ya Kiingereza zinaweza kuwa muhimu. Tafadhali kumbuka kuwa MWONGOZO hauwajibiki kwa maudhui ya nyenzo hizi.