Udhaifu wa misuli ya kiuno na mabega hujumuish kundi la udhaifu wa misuli ambao unaweza kurithiwa kwa njia mbalimbali. Misuli ya bega au nyonga huathiriwa.
Kudhoofika kwa misuli ni kundi la matatizo ya misuli ya kurithi ambapo jeni moja au zaidi zinazohitajika kwa ajili ya muundo wa kawaida wa misuli na utendaji kazi zina matatizo na kusababisha udhaifu wa misuli na kupotea kwa misuli (ulegevu wa misuli) kwa ukubwa tofauti.
Kama kundi, udhiafu wa misuli ya mabega na kiuno ni aina ya nne ambayo imeenea sana ya matatizo ya misuli ya kurithi. Udhaifu huu unaathiri watu 2 hadi 10 kati ya watu 100,000. Wanaume na wanawake wanaathiriwa kwa usawa.
Aina za udhaifu wa misuli ya kiuno na mabega zinaweza kurithishwa kwa njia mbalimbali kwa sababu ya jeni mbalimbali zinaweza kuhusishwa. Wakati mwingine ni jeni moja pekee yenye kasoro inahitajika, ambayo inaweza kurithiwa kutoka kwa mzazi yeyote (autosomal dominant). Wakati mwingine jeni yenye tatizo inapaswa irithiwe kutoka kwa wazazi wote wawili (kuwa kawaida na tulivu).
Udhaifu wa misuli ya kiuno na mabega husababisha udhaifu kwenye misuli ya moja wapo ya nyonga (udhaifu wa misuli wa Leyden-Möbius) au bega (udhaifu wa misuli wa Erb). Matatizo haya ya kurithi mara nyingi huanza mapema utotoni lakini huenda usionekane hadi mtu anapokuwa mtu mzima. Ni nadra kusababisha udhafu mkubwa.
Ugunduzi wa Kudhoofika kwa Misuli ya Kiuno na Mabega
Upimaji wa jeni
Bayopsi ya musuli
Utambuzi wa ugonjwa wa udhaifu wa misuli ya mabega na kiuno unatokana na dalili za sifa, umri wa mtu dalili zilipoanza na historia ya familia.
Kwa kawaida madaktari hufanya bayopsi ya misuli na upimaji wa jeni kuthibitisha utambuzi.
Matibabu ya Kudhoofika kwa Misuli ya Kiuno na Mabega
Udumishaji wa utendaji kazi huu na uzuiaji wa mikazo
Matibabu ya udhaifu wa misuli ya kiuno na mabega yamejikita katika kudumisha utendaji wa misuli na kuzuia misuli isigande kabisa, sehemu jongevu zinazoitwa mikazo.
Taarifa Zaidi
Nyenzo zifuatazo za lugha ya Kiingereza zinaweza kuwa muhimu. Tafadhali kumbuka kuwa Mwongozo hauwajibiki kwa maudhui ya nyenzo hizi.
Shirika la Udhaifu wa Misuli: Taarifa kuhusu utafiti, matibabu, tekonolojia na usaidizi kwa watu wanaoishi na udhaifu wa misuli ya kiuno na mabega