Udhaifu wa misuli ya uso na mabega ni aina ya tatu iliyoenea sana ya udhaifu wa misuli. Misuli ya uso na mabega inaathiriwa.
Kudhoofika kwa misuli ni kundi la matatizo ya misuli ya kurithi ambapo jeni moja au zaidi zinazohitajika kwa ajili ya muundo wa kawaida wa misuli na utendaji kazi zina matatizo na kusababisha udhaifu wa misuli na kupotea kwa misuli (ulegevu wa misuli) kwa ukubwa tofauti.
Udhaifu wa misuli ya uso na mabega (FSHMD) unarithishwa kupitia jeni ya kuwa kawaida na inayotawala. Kwa hivyo, jeni moja isiyo ya kawaida inatosha kusababisha tatizo na tatizo hilo linaweza kuonekana kwa watoto wa kiume au wa kike. Ni aina ya tatu iliyoenea zaidi ya udhaifu wa misuli na hutokea katika karibu watu 4 hadi 12 kati ya watu 100,000.
Dalili za Facioscapulohumeral ya Kudhoofika kwa Misuli
Dalili za udhaifu wa misuli ya uso na mabega kwa kawaida huanza taratibu kati ya umri wa miaka 7 na 20. Misuli ya sura na mabega siku zote inaathiriwa, kwa hivyo mtoto anapata shida kupiga mbinja, kufumba macho kwa nguvu, au kuinua mikono. Baadhi ya watu wenye tatizo hili hupata pia tone la mguu (mguu huanguka chini). Mara kwa mara watu pia wanapata matatizo ya kutosikia na matatizo ya macho.
Udhaifu huo ni nadra sana kuwa mkali na watu wengi si walemavu na wanaweza kuishi kiwango cha kawaida cha matarajio ya kuishi. Hata hivyo, watu wengine wanahitaji kutumia kiti cha magurudumu wanapokuwa watu wazima. Katika aina moja ambayo inakua mtoto akiwa mchnga, watoto wanakuwa wamepata udhaifu wa misuli unaoongezaka kwa haraka na ulemavu mbaya.
Utambuzi wa Facioscapulohumeral ya Kudhoofika kwa Misuli
Upimaji wa jeni
Utambuzi wa ugonjwa wa udhaifu wa misuli ya uso na mapega unajikita na sifa ya dalili, umri wa mtu wakai dalili zilianza, historia ya familia na matokeo ya upimaji wa jeni.
Matibabu ya Facioscapulohumeral ya Kudhoofika kwa Misuli
Matibabu ya kimwili
Hakuna matibabu ya udhaifu, lakini tiba ya viungo inaweza kusaidia kudumisha utendaji kazi wa misuli.
Taarifa Zaidi
Nyenzo zifuatazo za lugha ya Kiingereza zinaweza kuwa muhimu. Tafadhali kumbuka kuwa Mwongozo hauwajibiki kwa maudhui ya nyenzo hizi.
Shirika la Udhaifu wa Misuli: Taarifa kuhusu utafiti, matibabu, teknolojia na usaidizi kwa watu wanaoishi na udhaifu wa misuli ya uso na mabega