Ujumuishaji wa Vulva na Uvimbe wa Ngozi ya Nje

(Uvimbe Katika Ngozi ya Uke)

NaCharles Kilpatrick, MD, MEd, Baylor College of Medicine
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Oct 2025
v13953288_sw

Uvimbe unaojitokeza kwenye vulva ni pamoja na uvimbe wenye majimaji na uvimbe wa nje. Uvimbe wenye majimaji kwenye valva ni vifuko vidogo vilivyo na tishu katika eneo la valva. Uvimbe wa nje wa vulva unalingana lakini huwa na majimaji kutoka kwenye tezi za mafuta (tezi za mafuta) karibu na ufumwele wa nywele.

Uvimbe wenye majimaji ni uvimbe wa kawaida zaidi wa vulva. Vulva ni eneo ambalo lina viungo vya nje vya uzazi. Uvimbe wenye majimaji unaweza pia kujitokeza ukeni. Huweza kutokana na majeraha, kama vile kuchanika kbaada ya kujifungua. Vulva ikijeruhiwa, tishu yake (tishu ya epithelial) huweza kuonekana katika sehemu hiyo. Baadhi ya uvimbe wenye majimaji huanza wenyewe.

Anatomia ya Uzazi wa Mwanamke wa Nje

Uvimbe wa nje unaweza kuanza pale ambapo mirija ya tezi za mafuta huziba. Kisha majimaji ya tezi hizi hujikusanya chini ya ngozi.

Aina hizi zote mbili za uvimbe hatimayue huongezeka ukubwa na wakati mwingine kuambukizwa. Uvimbe ulioambukizwa unaweza kuwa mwekundu na mwepesi na husababisha tendo la ngono liwe na maumivu.

Uvimbe ambao hauambukizwi mara nyingi hausababishi dalili, lakini mara chache husababisha sonona. Huwa mweupe au manjano na mara nyingi huwa na inchi zisizozidi 1/2 (takribani sentimeta 1) kwa kipenyo.

Kushirikishwa na Uvimbe wa Ngozi ya Nje
Uvimbe wa Ndani ya Uke

Vaginal inclusion cysts are usually small and do not cause symptoms.

Vaginal inclusion cysts are usually small and do not cause symptoms.

By permission of the publisher. From Spitzer M, Mann M. In Atlas of Clinical Gynecology: Gynecologic Pathology. Edited by M Stenchever (series editor) and B Goff. Philadelphia, Current Medicine, 1998. (Courtesy of the International Society for the Study of Vulvar Disease.)

Kifuko cha Pamoja cha Ngozi cha Vulva

Many cysts are visible on both sides of the vulva.

Many cysts are visible on both sides of the vulva.

By permission of the publisher. From Kaufman R, Brown D. In Atlas of Clinical Gynecology: Gynecologic Pathology. Edited by M Stenchever (series editor) and B Goff. Philadelphia, Current Medicine, 1998.

Utambuzi wa Ugonjwa

  • Uchunguzi wa Fupanyonga

Kwa kawaida madaktari wanaweza kuona au kuhisi uvimbe wakati wa uchunguzi wa fupanyonga.

Matibabu

  • Kuondolewa kwa uvimbe

Iwapo uvimbe unasababisha dalili, huondolewa. Ikiwa wanawake wana uvimbe mmoja tu, hupewa sindano ya ganzi ya sehemu ndogo ili kuepusha kuhisi maumivu katika eneo hilo. Ikiwa wanawake wana uvimbe kadhaa, watalaamu wa matibabu wanaweza kutumia ganzi ya eneo kubwa ili kuondoa maumivu katika sehemu kubwa au ganzi ya jumla ili kusababisha kupoteza fahamu.