Polipu za Shingo ya Kizazi

(Uvimbe utakanao na utando wa ute ute)

NaCharles Kilpatrick, MD, MEd, Baylor College of Medicine
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Oct 2025
v812320_sw

Polipu za mlango wa kizazi ni maumbo yanayofanana na vidole ya tishu ambayo hujitokeza katika njia ya mlango wa kizazi. Mara nyingi polipu zitokanazo na utando wa ute hazisababishi saratani (usio na saratani).

  • Polipu za mlango wa kizazi zinaweza kusababishwa na uvimbe sugu au maambukizi.

  • Mara nyingi, polipu za mlango wa kizazi hazisababishi dalili zozote, lakini husababisha kuvuja damu ukeni au ute unaolingana na usaha.

  • Kwa kawaida, madaktari wanaweza kutambua polipu kwenye mlango wa kizazi wakati wa uchunguzi wa fupanyonga.

  • Polipu zinazosababisha kuvuja damu au kutokwa na ute huondolewa wakati wa uchunguzi wa fupanyonga.

Takribani asilimia 2 hadi 5 ya wanawake wana polipu za mlango wa kizazi. Uvimbe utakanao na utando wa ute katika shingo ya kizazi unaweza kusababishwa na uvimbe sugu au maambukizi.

Dalili za Polipu za Shingo ya Kizazi

Polipu nyingi za mlango wa kizazi hazisababishi dalili zozote. Baadhi ya polipu husababisha kuvuja damu kati ya vipindi vya hedhi au baada ya tendo la ngono. Mara chache, polipu huambukizwa, hali inayosababisha ute unaolingana na usaha kutoka ukeni.

Polipu huwa na rangi ya waridi nyekundu na hazizidi ukubwa wa inchi 1/2 (takribani sentimeta 1) kwa kipenyo.

Utambuzi Polipu za Shingo ya Kizazi

  • Uchunguzi wa Fupanyonga

Madaktari wanaweza kutambua polipu wanapofanya uchunguzi wa fupanyonga. Mara nyingi polipu hazisababishi saratani, lakini polipu hiyo inapoondolewa hupelekwa maabara ili kuthibitishwa kuwa haina seli zisizo za kawaida.

Matibabu ya Polipu za Shingo ya Kizazi

  • Kuondoa polipu

Polipu zinazosababisha kuvuja damu au kutokwa na ute ukeni huondolewa wakati wa uchunguzi wa fupanyonga kwenye ofisi ya daktari. Kwa kawaida, hatua hii haina maumivu na haihitaji kutumia ganzi. Mara chache damu huvuja baada ya kuondolewa kwa polipu hizo. Ikiwa damu itavuja, dawa inayochoma, kama vile naitreti ya silva, huwekwa kwenye eneo lililoathiriwa pamoja na sufi ili kuzuia damu kuvuja.

Polipu huchunguzwa ili kuthibitisha kuwa hazina kansa.

Ikiwa dalili (kutokwa na damu pamoja na uchafu) zitaendelea baada ya polipu kuondolewa, sampuli ya tishu kutoka kwenye utando wa uterasi (endometriamu) hutolewa na kuchunguzwa kwa kutumia hadubini (bayopsi ya endometriamu) ili kuondoa saratani ya endometriamu.