Kupunguza Uchungu wa Uzazi na Kujifungua

NaJulie S. Moldenhauer, MD, Children's Hospital of Philadelphia
Imekaguliwa naOluwatosin Goje, MD, MSCR, Cleveland Clinic, Lerner College of Medicine of Case Western Reserve University
Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024 | Imebadilishwa Jun 2024
v88381706_sw

Kwa ushauri wa daktari au mkunga wake, mwanamke kwa kawaida anaweka mipango ya njia ya kupunguza maumivu muda mrefu kabla uchungu haujaanza. Anaweza kuchagua moja wapo kai ya hizi zifuatazo:

  • Kujifungua kwa njia ya kawaida, ambayo inategemea mbinu ya kutulia na kuvuta pumzi ili kushughulika na maumivu

  • Dawa za maumivu zinadungwa kwenye au karibu na uke

  • Dawa za maumivu zinatolewa kwa njia ya mishipa

  • Dawa za maumivu zinatolewa kupitia kudungwa sindano karibu na uti wa mgongo, huitwa nusukaputi ya eneo maalumu

Baada ya uchungu kuaza, mipango ya kupunguza maumivu inaweza kurkebishwa, kutegemeana na jinsi maumivu yanavyoendelea, jinsi mwanamke anavyojihisi, kile anachopendelea na kile ambacho daktari au mkunga anapendekeza.

Uhitaji wa mwanamke wa dawa ya kupunguza maumivu wakati wa uchungu hutofautiana sana, inategemea sababu nyingi. Kuhudhuria madarasa ya maandalizi ya kujifungua mtoto husaidia kumwandaa mwanamke kwa ajili ya uchungu na kujifungua. Maandalizi na usaidizi wa kihisia kutoka kwa wataalamu wa huduma ya afya na watu wa kusaidia wakati wa uchungu waliochaguliwa kunaweza kuwasaidia wanawake kujua kile cha kutarajia na kufanya machaguo kuhusu jinsi ya kudhibiti maumivu wakati wa uchungu na kujifungua.

Nusukaputi ya eneo maalumu kwa kawaida hutia ganzi eneo kubwa kuanzia kwenye tumbo hadi kwenye miguu na makanyagio. Hutumika kwa wanawake wanaohitaji kuondoa maumivu kabisa. Taratibu zifuatazo zinaweza kutumika:

  • Nusukaputi ya mgongoni ni aina iliyozoeleka sana ya kudhibiti maumivu inayotumika wakati wa uchungu wa kujifungua. Nusukaputu inadungwa sehemu ya chini ya mgongo, kwenye sehemu iliyo kati ya uti wa mgongo na utando wa juu wa tishu inayofunika uti wa mgongo (sehemu ya uti wa mgongo). Kwa kawaida, katheta inawekwa kwenye sehemu ya uti wa mgongo, na nusukaputi ya eneohusika (kama vile bupivacaine) inatolewa kwa kuendelea na taratibu kupitia katheta. Dawa za afyuni (kama vile fentanyl au sufentanil) mara nyingi pia inadungwa. Kudungwa mgongoni kwa ajili ya uchungu na kujifungua hakumzuii mwanamke asisukume na hakuwafanyi wanawake kuonekana kuhitaji kujifungua kwa njia ya upasuaji. Sindano ya maumivu ya mgongoni pia inaweza kutumika katika ckujifungua kwa njia ya upasuaji.

  • Nusukaputi ya kwenye uti wa mgongo inahusisha kudunga nusukaputi kwenye nafasi kati ya utando wa kati na wa ndani wa tishu inayofunika uti wa mgongo (sehemu ya subaraknoidi). Sindano ya kwenye uti wa mgongo kwa kawaida inatumika wakati udhibiti wa haraka wa maumivu unahitajika, lakini thari yake inadumu tu kwa karibu saa 1 hadi 2. Nusukaputi ya uti wa mgongo mara nyingi inatumika kwa ajili ya kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati mwanamke hana katheta ya mgongoni.

Wakati mwingine, matumizi ya ama sindano ya mgongoni au uti wa mgongo husababisha kushuka kwa shinikizo la damu kwa mwanamke huyo. Matokeo yake, ikiwa moja wapo ya taratibu hizi zinatumika, shinikizo la damu la mwanamke hupimwa mara kwa mara.

Nusukaputi ya mahali husika hutia ganzi uke na tishu zinazozunguka mlango wake. Eneo hili linaweza kutiwa ganzi kwa kutunda nusukaputi ya eneo husika kupitia ukuta wa uke kwenye eneo linalozunguka neva inayotoa hisia kwenye eneo la sehemu ya chini ya uke (neva ya pundendali). Utaratibu huu, unaitwa kizuizi chapudendali, unatumika baadaye tu katika hatua ya pili ya uchungu wa kujifungua, wakati kichwa cha mtoto kinakaribia kuibuka kutoka kwenye uke. Utaratibu usio na ufanisi sana unahusisha kudunga nusukaputi ya mahali husika katika mlango wa uke. Utaratibu huu unatumika katika mazingira machache, kwa mfano, wakati ambapo mwanamke anakuwa na maumivu hata kiwa na kizuizi cha pudendali. Kwa taratibu zote mbili, mwanamke anaweza kusilia kuwa macho na kusukuma, na utendaji wa kijusi hauathiriwi. Taratibu hizi zinafaa kwa ajili ya kujifungua ambako hakuna matatizo.

Dawa za maumivu ni dawa za kupunguza maumivu, ikiwa ni pamoja na dawa za afyuni (kama vile fentanyl au morphine) zinazoweza kutolewa kwa njia ya mishipa au kwa kudunga sindano. Zinatolewa tu ikiwa nusukaputi ya eneo maalumu haipo. Hata hivyo baadhi ya klini zinatoa dawa hizi za kuondoa maumivu kama chaguo wakati wa hatu ya kwanza ya uchugu wa kujifungua. Kwa sababu baadhi ya dawa hizi zinaweza kupunguza kasi ya kupumua na utendaji mwingine wa mtoto mchanga, kiwango kinachotolewa ni kidogo kadiri iwezekanavyo. Ikiwa zinatolewa karibu sana na wakati wa kujifungua, mtoto anaweza kuwa ametiwa ganzi kupita kiasi, na kufanya mtoto kukabiliana na maisha mapya kuwa vigumu zaidi. Ikiwa ni lazima, ili kushughulikia athari hizi za ganzi za dawa hizi kwa mtoto, daktari anaweza kumpa mtoto dawa ya kuondoa sumu ya opioid naloxone muda mfupi baada ya kuzaa.

Nusukapiti ya jumla humfanya mwanamke asiwe na fahamu kwa muda. Ni nadra kutumika na haitumiki mara kwa mara kwa sababu inaweza kupunguza kasi ya shughuli za moyo, mapafu na ubongo wa mtoto. Ingawa athari hii kwa kawaida ni ya muda, inaweza kuingiliana na mtoto kuanza kuzoea maisha mapya. Nusukaputi ya jumla kwa kawaida hutumika pekee kwa ajili ya dharura ya kujifungua kwa njia ya upasuaji kwa wanawake ambao hawana katheta ya mgongobi, kwa sababu nusukaputi ya jumla ni njia ya haraka zaidi kutoa ganzi inayohitajika kwa ajili ya upasuaji.

Kuzaa kwa Njia ya Kawaida

Kujifungua kwa asili kunatumia mbinu za kutilia na kupumua ili kudhibiti maumivu wakati wa kujifungua mtoto.

Kujiandaa kwa ajili ya kujifungua kwa kawaida, mwanamke mjamzito (akiwa na mwenzi wake au la) anaingia kwenye mfunzo ya kujifungua, kwa kawaida vipindi 6 hadi 8 kwa wiki kadhaa, ili kujifunza kile kinachotokea katika hatua mbalimbali za uchungu wa kujifungua na kujifungua na jinsi ya kutumia mbinu za kuligeza mwili na kuvuta pumzi.

Mbinu ya kulegeza mwili inahusisha kukaza kwa kutambua sehemu ya mwili kisha kuilegeza. Mbinu hii inamsaidia mwanamke kulegeza sehemu iliyosalia ya mwili wake wakati mji wa mimba unakaza wakati wa uchungu na kulegeza mwili wake wote kati ya mikazo.

Mbinu ya kuvuta pumzi inahusisha aina kadhaa za kuvuta pumzi, ambazo zinatumiwa nyakati mbalimbali wakati wa uchungu. Wakati wa hatua ya kwanza ya uchungu, kabla mwanamke hajaanza kusukuma, aina zifuatazo za kuvuta pumzi zinaweza kusaidia:

  • Kuvuta pumzi kwa kina huku akiachia pumzi taratibu ili kumsaidia mwanamke apumzike mwanzoni na mwishoni mwa mkazo.

  • Kuvuta pumzi kwa haraka na si kwa kina katika sehemu ya juu ya kifua kwenye kilele cha mkazo

  • Ruwaza ya kuvuta pumzi harakaharaka na kushusha humsaidia mwanamke kuepuka kusukuma wakati anahisi kutaka sana kusukuma kabla shingo ya kizazi haijafunguka kikamilifu (kupanuka) kuvuta kurudi nyuma

Mbinu inayofaamika vizuri zaidi ya kujifungua kwa kawaida pengine ni mbinu ya Lamaze. Mbinu nyingine, mbinu ya Leboyer, hujumuisha kujifungua kwenye chumba chenye giza na kumzamisha mtoto kwenye maji ya vuguvugu mara baada ya kujifungua.