Mlipuko wa ukurutu wa ujauzito ni vipele vinavyowasha sana vinavyotokea wakati wa ujauzito pekee.
Mlipuko wa ukurutu wa ujauzito hutokea katika takriban mimba 1 kati ya 160 hadi 300. Ni kawaida zaidi miongoni mwa wanawake walio na mimba zenye zaidi ya kijusi kimoja (mimba ya watoto wengi). Upele huu kwa kawaida hutokea katika ujauzito wa kwanza. Kisababishaji hakijulikani.
Madoa mekundu, yenye umbo lisilo la kawaida, yaliyoinuliwa kidogo huonekana kwenye tumbo. Wakati mwingine madoa huwa na malengelenge madogo yaliyojaa umajimaji katikati. Mara nyingi, ngozi inaliyo karibu huwa na rangi iliyofifia. Upele huenea hadi kwenye mapaja, makalio na wakati mwingine mikononi. Mikono, nyayo, na uso kwa kawaida haziathiriwi. Mamia ya madoa yanayowasha yanaweza kutokea. Kuwashwa kunasumbua kiasi cha kumfanya mwanamke asilale usiku.
Uvimbe wa polimofiki wa ujauzito ni vipele vinavyowasha sana (ya uvimbe). Mabaka mekundu, yaliyo na umbo usio laini, yaliyofura kidogo huonekana kwenye tumbo, kisha huenea kwenye mapaja, makalio, na mara kwa mara kwa mikono.
© Springer Science+Business Media
Kwa kawaida, upele huonekana wakati wa wiki 2 hadi 3 za mwisho za ujauzito na mara kwa mara wakati wa siku chache za mwisho au baada ya kujifungua. Hata hivyo, inaweza kutokea wakati wowote baada ya wiki ya 24. Kwa kawaida, upele huisha ndani ya siku 15 baada ya kujifungua. Hujirudia katika hadi 5% ya mimba zinazofuata.
Madaktari hutambua mlipuko wa ukurutu wa ujauzito kwa kuchunguza ngozi. Hata hivyo, kufanya utambuzi dhahiri kunaweza kuwa vigumu kwa sababu kunafanana na vipele vingine vinavyowasha.
Kupaka krimu ya kotikosteroidi (kama vile triamcinolone) moja kwa moja kwenye ngozi mara nyingi husaidia. Mara chache sana, kwa dalili kali, kotikosteroidi (kama vile prednisone) hutolewa kwa njia ya mdomo.
Antihistamini ambazo hazisababishi kizunguzungu, zinazomezwa kupitia mdomo, zinaweza pia kutumika kupunguza kuwasha.