Pitiriasisi rosea ni nini?
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Pityriasis rosea ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha kuwasha na viraka vidogo vya mviringo kwenye ngozi yako. Kwenye ngozi nyeusi, viraka vinaweza kuwa vya zambarau, kahawia, au kijivu. Kwenye ngozi nyeupe, viraka vinaweza kuwa na rangi nyekundu au rangi ya waridi.
Pitiriasisi rosea inaweza kusababishwa na virusi, lakini madaktari hawadhani unaweza kuenea kwa watu wengine
Wasichana na wanawake wenye umri wa kati ya miaka 10 na 35 wana uwezekano mkubwa wa kupata pityriasis rosea
Pitiriasisi rosea kwa kawaida inaondoka yenyewe kwa karibu wiki 5, lakini wakati mwingine inaweza kudumu kwa miezi 2 au zaidi
Nini kinachosababisha pitiriasisi rosea?
Madaktari hawaji kwa hakika kinachosababisha pitiriasisi rosea, lakini wanadhani unaweza kuwa unasababishwa na virusi.
Je, dalili za pitiriasisi rosea ni zipi?
Kwa kawaida mwanzoni utapata kiraka cha ngozi kwenye kifua chako, sehemu ya tumbo, au mgongoni ambayo ni:
Ni la mviringo
Lina magamba
Rangi ya waridi au rangi nyekundu kwenye ngozi nyekundu au rangi ya zambarau, kahawia au kijivu kwenye ngozi nyeusi
Karibu upana wa nhcini 1 hadi 4 (sentimita 2.5 hadi 10)
Baka hili linaitwa baka la ngozi au baka mama. Wakati mwingine, unahisi kuchoka na mdhaifu, unaumwa kichwa au unapata maumivu ya maungo siku chache kabla baka halijatokea.
Awali, watu wengi walio na pitiriasisi rosea wanakuwa na doa moja kubwa lenye magamba linaloitwa baka la ngozi (mshale) na ndani ya wiki 1 hadi 2, mabaka madogo ya rangi ya kahawia au wadiri yanaweza kutokea kwenye pingili, mikono na miguu.
Baada ya wiki 1 hadi 2 unaweza kuwa na:
Viraka vingi vidogovidogo kwenye sehemu nyingine za mwili wako
Mwasho unaoweza kuwa mkali
Kwa watoto, viraka vinaweza kuanza katika eneo la kinena (eneo kati ya mapaja yako ya juu na tumbo lako) au chini ya mikono na kisha kuenea. Watoto na wanawake wajawazito wenye pitiriasisi rosea wanaweza kuwa na madoa wenye magamba kidogo au yasiwepo.
Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina pitiriasisi rosea?
Daktari wako mara nyingi anaweza kukuambia ikiwa una pitiriasisi kulingana na jinsi mabaka ya kwenye ngozi yako yanavyoonekana na kwa sababu baka kubwa linatokea kwanza.
Madaktari hutibu vipi pitiriasisi rosea?
Daktari wako anaweza kupendekeza:
Kukaa kwenye mwanga wa jua wa asili au taa za jua
Dawa inayoitwa antihistamini unayotumia kwa kinywa kutibu mwasho
Krimu za kotikosteroidi kutibu mwasho mkali ikiwa antihistamini haisaidii