Endokadaitisi inayoambukizwa ni nini?
Endokadaitisi ni hali ya kuvimba kwa sehemu ya ndani ya moyo wako. Endokadaitisi inayoambukizwa ni:
Maambukizi ya sehemu ya ndani ya moyo wako
Maambukizi yanaweza kuwa kwenye utando wa chemba ya moyo wako au kwenye vali za moyo wako.
Endokadaitisi inayoambukizwa hutokea pale bakteria wanapoingia kwenye damu yako na kusafiri hadi kwenye moyo wako
Endokadaitisi inayoambukizwa kimsingi hutokea kwenye tishu za moyo zenye kasoro, kwa mfano hutokea pale unapokuwa na kasoro ya kuzaliwa kwenye moyo au vali za moyo zilizoharibika, au ikiwa una vali ya moyo ya bandia
Maambukizi yanaweza kuharibu vali za moyo hivyo kushindwa kufanya kazi vizuri na kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi
Madaktari hufanya vipimo vya damu na echocardiografia ili kuona kama una endokadaitisi inayoambukizwa
Madaktari hutibu endokadaitisi inayoambikizwa kwa kutumia dawa za kuua bakteria na wakati mwingine kwa upasuaji wa moyo
Ikiwa una vali ya moyo ya bandia au kasoro ya kuzaliwa katika moyo wako, unaweza kutakiwa kutumia dawa za kuua bakteria kabla ya upasuaji au tiba ya meno ili kuzuia endokadaitisi
Je, nini husababisha endokadaitisi inayoambikizwa?
Endokadaitisi inayoambukizwa husababishwa na bakteria au kuvu ambao huingia kwenye damu yako na kuasfiri hadi kwenye moyo wako. Bakteria wanaweza kuingia kwenye damu yako unapokuwa na:
Maambukizi ya ngozi kama vile cellulitis au usaha wa ngozi
Aina fulani za upasuaji au tiba ya meno
Bomba lililochomekwa kwenye vena (IV) kwa muda mrefu
Una hatari kubwa ya kupata endokadaitisi inayoambukizwa kama:
Ulizaliwa ukiwa na tatizo la moyo
Una vali ya moyo yenye kasoro au iliyoharibika
Kujidunga dawa za kulevya
Una vali ya moyo ya bandia, kifaa cha kurekebisha mapigo ya moyo, au kifaa cha kuamsha moyo uliosimama
Umewahi kuwa na endokadaitisi inayoambukizwa hapo awali
Zipi ni dalili za endokadaitisi inayoambukizwa?
Kwa kawaida endokadaitisi ya kuambukizwa huanza taratibu. Lakini wakati mwingine hutokea kwa ghafla.
Endokardaitisi ya kuambukizwa ya wastani hutokea pale endokadaitisi inapotokea taratibu, ikichukua wiki hadi miezi. Taratibu unapata dalili kama vile:
Uchovu
Homa ya chini (99° to 101° F or 37.2° to 38.3° C)
Kupungua uzito
Kutokwa jasho
Endokardaitisi kali ya kuambukizwa huanza ghafla, na unakuwa mgonjwa sana kwa haraka. Mojawapo ya vali za moyo wako inaweza kuharibika vibaya ndani ya siku chache. Dalili zinajumuisha:
Homa kali (102° to 104° F or 38.9° to 40° C)
Uchovu mwingi
Ugumu wa kupumua
Ukiwa na aina yoyote ya endokadaitisi, unaweza pia kuwa na:
Mzizimo
Maumivu ya viungo
Ngozi ya yenye rangi iliyofifia
Viuvimbe uchungu chini ya ngozi yako
Wakati mwingine vitu vyenye maambukizi kutoka kwa moyo wako husambaa kupitia damu yako hadi sehemu zingine za mwili wako. Unaweza kupata maambukizi kwenye mapafu, ubongo, figo au ogani zako nyingine.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina endokadaitisi inayoambukizwa?
Madaktari hushuku uwepo wa endokadaitisi inayoambukizwa kutokana na dalili zako. Ili kuthibitisha, daktari atafanya:
Ekokadiografia (kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa moyo wako)
Vipimo vya damu ili kutafuta bakteria
Je, madaktari wanatibu vipi endokadaitisi inayoambukizwa?
Madaktari hutibu endokadaitisi inayoambukizwa kwa kutumia:
Dawa za kuua bakteria, zinazoingizwa kupitia vena (IV), kwa angalau wiki 2 na hadi wiki 8
Wakati mwingine, upasuaji wa moyo ili kurekebisha au kurudishia vali ya moyo iliyoharibika
Ninawezaje kuzuia endokadaitisi inayoambukizwa?
Ili kuzuia endokadaitisi inayoambukizwa:
Usijidunge dawa za kulevya
Tibu maambukizi kwa haraka
Tunza vizuri meno na fizi zako
Ikiwa uko katika hatari kubwa ya kupata endokadaitisi inayoambukizwa, unapaswa kuwa makini sana na vitu hivi. Zaidi ya hayo, watu waliyo katika hatari kubwa wanaweza pia kutakiwa:
Kumeza dawa za kuua bakteria kabla ya tiba fulani za meno au tiba kwa njia ya upasuaji ambazo zinaweza kuruhusu bakteria waingie kwenye mwili
Muulize daktari wako kama uko katika hatari kubwa.