Biolojia ya Mishipa ya Damu

Uhakiki Kamili: Jan 2026 NaThe Manual's Editorial Staff
Iliyosasishwa mwisho: Jan 2026
v39747722_sw

Mishipa ya damu ni nini?

Mishipa ya damu ni bomba zinazofanana paipu zenye uwazi ambazo husafarisha damu kwenye mwili wako. Damu hufikisha oksijeni na virutubishi kwenye sehemu zote za mwili wako na kuondoa uchafu, kama vile kaboni dioksidi.

  • Kuna aina 2 kuu za mishipa ya damu—ateri na vena

  • Ateri husafirisha damu mpya kutoka kwenye moyo hadi kwenye viungo vyako

  • Vena husafirisha damu iliyojaa takataka na kuirudisha kweye moyo wako

  • Ateri na vena zimeunganishwa kwa mishipa midogo sana inayoitwa kapilari

Ateri zina kuta nene zilizofunikwa kwa misuli Ateri zinahitaji kuwa imara kwa sababu shinikizo la damu ni la juu zaidi kwenye ateri. Ateri za misuli yako wakati wote hubana na kuachia ili kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu.

Vena zina kuta nyembamba zenye misuli kidogo tu. Shinikizo la damu liko chini katika vena. Vena zinaweza kutanuka ili kukabili ongezeko la damu. Baadhi ya vena zina vali zinazozuia damu kurudi nyuma.

Mishipa yako ya damu na moyo wako ni sehemu za mfumo wa moyo na mishipa

Mishipa ya damu: Kuzungusha Damu

Damu husafiri kutoka kwenye moyo kwenye ateri, ambazo hugawanyika katika mishipa midogo midogo, mwishowe kuwa matawi ya ateri. Matawi ya ateri huungana na mishipa ya damu ambayo ni midogo zaidi inayoitwa kapilari. Kupitia kuta nyembamba za kapilari, oksijeni na virutibishi hupita kutoka kwenye damu na kuingia katika tishu, na takataka hutoka kwenye tishu na kuingia kwenye damu. Kutoka kwenye kapilari, damu hupita kwenye mishipa midogo/venali, kisha huingia kweye vena ili kurejea kwenye moyo.

Ateri na matawi ya ateri huwa na kuta za misuli nene kiasi kwa sababu shinikizo la damu ndani yake ni la juu na kwa sababu zinapaswa kurekebisha kipenyo chake ili kudumisha shinikizo la damu na kudhibiti mtiririko wa damu. Vena na mishipa midogo/venali zina kuta za misuli ambazo ni nyembamba na si nene sana kuliko ateri na matawi ya ateri, na sababu kubwa ni kwamba shinikizo lililo kwenye vena na mishipa midogo/venali ni la chini sana. Vena zinaweza kutanuka ili kuhimili uongezeko la ujazo wa damu.

Mishipa ya damu inaweza kupata hitilafu gani?

Ikiwa mshipa wa damu utakatwa au kuchanika, utavuja damu, kwa nje au kwa ndani katika viungo vyako. Matatizo mengine ya kawaida ya mishipa ya damu ni pamoja na:

  • Atherosklerosisi (ateri kuwa ngumu), ambapo mkusanyiko wa mafuta huziba ateri zako

  • Kuvimba kwa mshipa, ambapo ni viuvimbe kwenye sehemu dhaifu za kuta za ateri zako

  • Kuganda kwa damu kunaweza kutokea kwenye vena (huitwa mvilio wa damu kwenye mshipa wa ndani) au ateri zako, hivyo kusababisha kizuizi cha ghafla

  • Vaskulitisi, ambapo mishipa ya damu huvimba

  • Vena zilizovimba daima, ambapo vena zilizo karibu na tabaka la juu la ngozi yako hutanuka na kugeuzwa