maumivu ya kifuu cha goti

(ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti)

Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Sept 2025
v41942943_sw

Je, ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti ni nini?

Ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti ni kulainika kwa gegedu lililopo chini ya kifuu cha goti (pia huitwa kibandiko cha goti). Gegedu ni tishu laini, thabiti ambayo hulinda mifupa pale inapokutana, kama vile kifuu cha goti au mifupa mingine katika kiungo cha goti.

  • Ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti huwapata zaidi vijana, hasa vijana wakimbiaji na wakimbiaji wanaofanya mazoezi ya viungo

  • Dalili kuu ni hafifu, maumivu ya kuuma kwenye goti

  • Inasababishwa na pia ya goti ambayo haipo mahali pake

  • Madaktari huitibu kwa mazoezi, barafu, dawa ya maumivu, na wakati mwignine upasuaji

Ndani ya Goti (Mwonekano wa Upande)

Je, nini husababisha ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti?

Chondromalacia patellae mara nyingi husababishwa na pia ya goti ambayo haipo mahali pake kwa hivyo haitelezi vizuri juu ya kiungo cha goti. Kukimbia au shuguli ambazo zinahusisha kupinda sana goti hufanya eneo la chini ya kifuu cha goti kujisugua kwenye mifupa ya goti. Hali hii inaweza kuharibu gegedu lililopo chini ya kufuu cha goti.

Je, dalili za ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti ni zipi?

Ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti husababisha:

  • Maumivu hafifu, yenye kuuma sehemu ya nyuma na ile inayozunguka goti

Hausababishi goti kuvimba

Maumivu kutoka kwa chondromalacia patellae mara nyingi hutokea wakati:

  • Ukipanda ngazi

  • Ukicheza mchezo fulani

  • Unapokaa kwa muda mrefu

  • Ukikimbia

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti?

Mara nyingi madaktari hujua kutokana na dalili za mtoto wako. Eksirei haziwezi kusaidia katika utambuzi wa ugonjwa, lakini madaktari wanaweza kupiga eksirei kutafuta matatizo mengine kwenye goti.

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti?

Madaktari hutibu ugonjwa wa maumivu ya kifuu cha goti kwa kumfanya mtoto wako:

  • Afanye mazoezi ya kuimarisha misuli minne (ile iliyo sehemu ya mbele ya paja) na kuongeza wepesi

  • Kuweka barafu kwenye goti

  • Meza dawa za kutibu uvimbe (NSAIDS) zisizo za steroidi, kama vile ibuprofen

Wakati mwingine, madaktari watafanya upasuaji ili kulainisha sehemu ya chini ya kifuu cha goti.