Tibakemikali

Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Nov 2025
v27370848_sw

Tibakemikali ni nini?

Tibakemikali ni dawa inayoharibu seli za saratani. Tibakemikali hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa seli. Lakini kwa kuwa seli zote mwilini hukua, tibakemikali pia huharibu baadhi ya seli za kawaida na kusababisha madhara. Si dawa zote zinazotibu saratani huchukuliwa kama tibakemikali, kwa mfano, tiba ya mfumo wa kinga ni tofauti.

  • Tibakemikali haifanyi kazi kwenye kansa zote

  • Kuna dawa nyingi tofauti za tibakemikali—ile utakayopata itategemea aina ya saratani uliyonayo

  • Dawa nyingi za tibakemikali hutolewa kupitia mshipa wako (IV)

  • Madaktari wanaweza kukupa dawa kadhaa za tibakemikali kwa wakati mmoja au wanaweza kuunganisha tibakemikali na aina nyinginezo za matibabu ya saratani, kama vile upasuaji au tiba ya mionzi

  • Madaktari wanaweza kukupa dawa nyinginezo ili kupunguza athari za tibakemikali

Wakati mwingine baada ya kutumia dawa za tibakemikali kwa muda, seli za saratani huwa kuwa kinzani kwa dawa hiyo. Tibakemikali huacha kuziua. Ikiwa hili litatokea, daktari wako anaweza kujaribu dawa tofauti.

Je, athari mbaya za tibakemikali ni zipi?

Tibakemikali ina sifa za kusababisha athari mbaya na wakati mwingine athari hatarishi. Dawa mpya za tibakemikali mara nyingi hazisumbui sana kuliko zile za zamani. Na madaktari sasa wana matibabu bora ya baadhi ya madhara yanayotokea.

Athari mbaya zinazotokea sana ni:

  • Kuhisi mgonjwa kwenye tumbo lako au kutapika

  • Kutohisi njaa kama kawaida

  • Kupungua uzani

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Kuharisha (kinyesi chepesi chenye umajimaji na kinachotoka mara kwa mara)

  • Kupoteza nywele zako

  • Vidonda kwenye kinywa au pua

Tibakemikali mara nyingi huathiri seli nzuri zinazotengeneza damu kwenye uboho. Hali hii inaweza kupunguza idadi ya seli zako za damu, jambo ambalo linaweza kusababisha:

  • Kiwango cha chini cha damu (anemia), iwapo idadi ya seli zako nyekundu za damu imepungua

  • Maambukizi mabaya, iwapo idadi ya seli zako nyeupe imepungua

  • Kuvuja damu, iwapo idadi ya chembe sahani imepungua

Anemia inaweza kusababisha:

  • Udhaifu

  • Kuhisi kizunguzungu

  • Kupumua kwa shida au maumivu ya kifua

Maambukizi kutokana na idadi iliiyopungua ya seli nyeupe yanaweza kusababisha:

  • Homa

Idadi iliyopungua ya chembe sahani inaweza kusababisha:

  • Kuvimba kwa urahisi

  • Kuvuja damu kutoka puani, fizi, au rektamu

Tibakemikali inaweza pia kuathiri ogani nyinginezo kando na uboho na kusababisha matatizo mengine ya kimatibabu:

  • Uharibifu kwenye mapafu, moyo, au ini

  • Ugumba (matatizo ya kupata ujauzito)

  • Wakati mwingine uwezekano mkubwa wa kupata kansa nyingine kama vile lukemia