Uti wa Mgongo

Uhakiki Kamili: Feb 2026 NaThe Manual's Editorial Staff
Iliyosasishwa mwisho: Feb 2026
v48796755_sw

Je, uti wa mgongo ni nini?

Jinsi Uti wa Mgongo Ulivyo

A column of bones called vertebrae make up the spine (spinal column). The vertebrae protect the spinal cord, a long, fragile structure contained in the spinal canal, which runs through the center of the spine. Between the vertebrae are disks composed of cartilage, which help cushion the spine and give it some flexibility.

Like the brain, the spinal cord is covered by 3 layers of tissue (meninges).

Spinal nerves: 31 pairs of spinal nerves emerge from the spinal cord between the vertebrae. Each nerve emerges in 2 short branches (roots):

  • Motor (or anterior) root at the front of the spinal cord

  • Sensory (or posterior) root at the back of the spinal cord

The motor roots carry commands from the brain and spinal cord primarily to skeletal muscles to control movement.

The sensory roots carry sensory information (about pain, temperature, vibration, limb position, and light touch) to the brain from other parts of the body.

Cauda equina: The spinal cord ends about three-fourths of the way down the spine, but a bundle of nerves extends beyond the cord. This bundle is called the cauda equina because it resembles a horse’s tail. The cauda equina carries nerve impulses, both motor and sensory, to and from the legs.

Uti wa mgongo ni bomba refu lililoundwa kwa neva ambalo huanzia kwenye ubongo na kushuka chini hadi kwenye mgongo wako ukipita kwenye uwazi wa kati wa mgongo wako.

  • Uti wa mgongo ni kama kebo ya umeme ambayo husafirisha ujumbe kwenda na kurudi baina ya ubongo na mwili wako.

  • Kama mabavyo fuvu hulinda ubongo wako, mgongo hulinda uti wa mgongo wako, ambao ni rahisi kudhurika

  • Uti wa mgongo husafirisha ishara kutoka kwenye ubongo zinazouambia mwili wako cha kufanya, kama vile kusogeza mikono au miguu yako

  • Pia uti wa mgongo husafirisha ishara hadi kwenye ubongo kutoka kwenye mwili wako kama vile umegusa nini au sehemu gani yenye maumivu

  • Matendohisia (kama vile kuvuta mkono wako kutoka kwenye jiko la moto) hutokea kwenye uti wako wa mgongo pasipo ubongo wako kuhusika

  • Ikiwa uti wa mgongo wako umeharibika, kwa kawaida unapoteza uwezo wa kusogea au kuhisi sehemu za mwili wako

Je, uti wa mgongo hufanyaje kazi?

Seli za neva katika ubongo hutuma ujumbe hadi kwenye uti wa mgongo wako. Neva zingine kwenye uti wa mgongo wako hupokea ujumbe huu na kuutuma kwa mwili wako kupitia mojawapo ya neva za uti wa mgongo.

Seli za neva kwenye uti wa mgongo wako zina nyuzi za neva zilizosambaa kwenye mwili wako ambazo zimeunganishwa kwenye vipokezi vya hisia. Kwa mfano, kuna vipokezi vya hisia kwenye ngozi yako kwa ajli ya mguso na maumivu. Kitu chochote kinachochochea hivyo vipokezi vya hisia, kama vile kuchomwa na sindano, hutuma ishara kupitia nyuzi za neva hadi kwenye uti wa mgongo wako. Seli zingine za neva kwenye uti wa mgongo wako husafirisha ishara hiyo ya sehemu unapohisi maumivu hadi kwa ubongo wako.

Je, neva za uti wa mgongo ni nini?

Neva za uti wa mgongo ni neva za ukubwa wa wastani zinazounganisha uti wa mgongo na neva ndogo zinazoelekea sehemu mbalimbali za mwili wako. Zipo jozi 31 za neva za uti wa mgongo zinazoingia na kutoka kwenye uti wa mgongo kwenye nafasi kati ya vatabrae yako.

Kila neva ya uti wa mgongo huanzia sehemu maalum ya uti wa mgongo na kuelekea sehemu maalum kwenye mwili wako. Hivyo, kwa mfano, ukigusa sehemu mahususi kwenye ngozi yako, unahisi sehemu hiyo kwa sababu ya ujumbe uliotumwa kwenye ubongo wako kupitia neva mahususi ya uti wa mgongo.

Muundo wa Kawaida wa Seli ya Neva

A nerve cell (neuron) consists of a large cell body and nerve fibers—one elongated extension (axon) for sending impulses and usually multiple branches (dendrites) for receiving impulses. Impulses from the axon of 1 nerve cell cross a synapse (the junction between 2 nerve cells) to the dendrite of another cell.

Each large axon is surrounded by oligodendrocytes in the brain and spinal cord and by Schwann cells in the peripheral nervous system. The membranes of these cells consist of a fat (lipoprotein) called myelin. The membranes are wrapped tightly around the axon, forming a multilayered sheath. This myelin sheath resembles insulation, such as that around an electrical wire. Nerve impulses travel much faster in nerves with a myelin sheath than in those without one.

Je, uti wa mgongo unaweza kupata matatizo gani?

Kuna matatizo mengi yanayoweza kuathiri uti wa mgongo wako, ikiwa ni pamoja na:

  • Majeraha

  • Saratani iliyoenea kwenye mgongo wako inaweza kuendelea hadi kwenye uti wa mgongo wako na kuuharibu

  • Kupoteza seli za neva za uti wa mgongo kutokana na magonjwa kama vile sklerosisi ya sehemu nyingi au kuzuiwa kwa usambazaji wa damu

Mara baada ya kufa kwa seli za neva katika uti wa mgongo, haziwezi kukua tena. Hivyo uharibifu wa uti wa mgongo kwa kawaida ni wa kudumu.

Ikiwa uti wa mgongo wako umeharibiwa, dalili zako hutegemea mahali ambapo uharibifu ulitokea. Kwa mfano, uti wa mgongo ukiharibika upande wa chini, huenda usiweze kusogeza au kuhisi chochote kwenye miguu yako lakini bado unaweza kutumia mikono yako. Lakini uti wa mgongo ukiharibiwa kwenye shingo, mikono na miguu yako yote huenda ikaathirika. Uti wa mgongo ukiharibika kwenye shingo yako, huenda usiweze kupumua. Huenda usiweze kudhibiti matumbo na kibofu cha mkojo, na huenda ukapoteza uwezo wa kushiriki ngono bila kujali sehemu ya uti wa mgongo wako uliyoharibiwa.