Kutengeneza upya Matiti

Kutengeneza upya Matiti

Baada ya daktari wa upasuaji wa jumla kuondoa uvimbe wa titi na tishu za titi zinazozunguka (upasuaji wa kuondoa matiti), daktari wa upasuaji wa plastiki anaweza kurekebisha umbo la titi. Kipandikizi cha silikoni au cha salini kinaweza kutumika. Au katika upasuaji mgumu zaidi, tishu zinaweza kuchukuliwa kutoka sehemu nyingine za mwili wa mwanamke, kama vile tumbo, matako, au mgongo.

Urekebishaji wa umbo la titi unaweza kufanywa wakati mmoja na upasuaji wa kuondoa matiti—chaguo linalohusisha kuwa chini ya athari ya dawa za ganzi kwa muda mrefu zaidi—au baadaye—chaguo linalohusisha kuwa chini ya athari ya dawa za ganzi kwa mara ya pili.

Urekebishaji wa chuchu na ngozi inayozunguka hufanywa baadaye, mara nyingi katika ofisi ya daktari. Dawa ya ganzi ya jumla haihitajiki.

Kwa wanawake wengi, titi lambalo umbo lake linarekebishwa linaonekana la asili zaidi kuliko lile lililotibiwa kwa tiba ya mionzi, hasa ikiwa uvimbe ulikuwa mkubwa.

Ikiwa kipandikizi cha silikoni au salini kitatumika na ngozi ya kutosha iliachwa kuifunika, hisia kwenye ngozi iliyo juu ya kipandikizi ni ya kawaida kwa kiasi fulani. Hata hivyo, hakuna aina yoyote ya kipandikizi kinachohisi kama tishu za matiti unapogusa. Ikiwa ngozi kutoka sehemu nyingine za mwili inatumika kufunika titi, hisia nyingi hupotea. Hata hivyo, tishu kutoka sehemu nyingine za mwili huhisi kama tishu za matiti kuliko kipandikizi cha silikoni au salini.

Silikoni wakati mwingine huvuja kutoka kwenye mfuko wake. Kwa sababu hiyo, kipandikizi kinaweza kuwa kigumu, kusababisha usumbufu, na kuonekana kisichovutia sana. Pia, silicone wakati mwingine huingia kwenye mkondo wa damu.

Baadhi ya wanawake wana wasiwasi iwapo silikoni inayovuja husababisha saratani katika sehemu nyingine za mwili au magonjwa adimu kama vile lupus erythematosus ya kimfumo (lupus). Hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba uvujaji wa silikoni una madhara haya makubwa, lakini kwa sababu huenda ikawa hivyo, matumizi ya vipandikizi vya silikoni yamepungua, hasa miongoni mwa wanawake ambao hawajapata saratani ya matiti.

Katika mada hizi