Homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko ni ugonjwa wa rickettsial unaosababishwa na Rickettsia prowazekii na huenezwa na chawa wa mwilini na mara kwa mara kupitia kugusana na vichakuro wanaoruka.
Watu wenye kali iletwayo na chawa ya mlipuko hupata homa, maumivu makali ya kichwa, na uchovu uliokithiri, ikifuatiwa na upele baada ya siku 4 hadi 6..
Ili kutambua maambukizi, madaktari wanapima sampuli ya upele na wakati mwingine kufanya vipimo.
Homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko hutibiwa kwa dawa ya kiuavijasumu.
Kufua na kukausha nguo zilizoathiriwa kwenye joto la juu kunaweza kusaidia kuzuia kuenea kwa maambukizi.
Rickettsiae ni aina ya bakteria ambayo inaweza kuishi tu ndani ya seli za viumbe vingine. Rickettsiae zinazosababisha homa ya kali iletwayo na chawa ya mlipuko kwa kawaida huishi kwa watu (mwenyeji). Lakini Amerika Kaskazini, rickettsiae hawa wanaweza pia kuishi katika kindi wanaoruka.
Homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko hutokea kote ulimwenguni. Maambukizi kwa kawaida huenezwa na chawa wa mwilini wakati kinyesi chao kinapoingia mwilini kupitia mipasuko kwenye ngozi au wakati mwingine kupitia utando wa kamasi wa macho au mdomo. Nchini Marekani, watu mara kwa mara hupata homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko baada ya kugusana na vichakuro wanaoruka.
Maambukizi haya huitwa homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko kwa sababu hapo awali, yamesababisha milipuko mikubwa (magonjwa ya mlipuko) ambayo yaliua idadi kubwa ya watu. Milipuko kama hiyo sasa ni nadra, lakini milipuko midogo imetokea hivi karibuni barani Afrika. Homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko huenea kwa urahisi zaidi katika mazingira yenye msongamano na uchafu kama inavyotokea wakati wa vita au machafuko ya wenyewe kwa wenyewe au katika maeneo yenye umaskini uliokithiri.
Dalili za Janga la Homa Kali Iletwayo na Chawa
Dalili za homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko huanza ghafla takriban siku 7 hadi 14 baada ya bakteria kuingia mwilini. Watu wana homa na maumivu makali ya kichwa na huhisi uchovu sana. Upele huonekana siku 4 hadi 6 baadaye. Upele kwa kawaida huanza kifuani na kuenea hadi mikononi, na miguuni.
Wakati mwingine wengu huongezeka ukubwa. Ikiwa maambukizi ni makubwa, shinikizo la damu linaweza kuwa chini sana, figo zinaweza kushindwa kufanya kazi, na gangrini na/au nimonia zinaweza kutokea.
Bila kutibiwa, homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko inaweza kusababisha kifo; hatari ya kifo huongezeka kadri umri unavyoongezeka.
Utambuzi wa Janga la Homa Kali Iletwayo na Chawa
Tathmini ya daktari
Bayopsi na upimaji wa upele
Vipimo vya damu
Utambuzi wa homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko huashiria na dalili, hasa ikiwa mtu ana chawa mwilini au amekuwa katika eneo ambalo kulikuwa na mlipuko wa homa kali iletwayo na chawa.
Ili kuthibitisha utambuzi, madaktari wanaweza kufanya kipimo cha immunofluorescence, ambacho hutumia sampuli iliyochukuliwa kutoka kwenye upele (bayopsi). Au wanaweza kutumia mbinu ya mmenyuko wa mnyororo wa polima (PCR) ili kuwawezesha kugundua bakteria haraka zaidi.
Madaktari wanaweza kufanya vipimo vya damu ili kugundua kingamwili kwa bakteria. Hata hivyo, kufanya kipimo mara moja hakutoshi. Ni lazima kipimo kirudiwe wiki 1 hadi 3 baadaye ili kuangalia kama kuna ongezeko katika kiwango cha kingamwili. Hivyo, vipimo vya kingamwili haviwasaidii madaktari kugundua maambukizi mara tu baada ya mtu kuugua lakini vinaweza kusaidia kuthibitisha utambuzi baadaye.
Matibabu ya Janga la Homa Kali Iletwayo na Chawa
Dawa za kuua bakteria
Matibabu ya homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko kwa kawaida hujumuisha doxycycline (aina ya dawa ya kiuavijasumu inayoitwa tetracycline), inayotolewa kwa mdomo. Watu hutumia dawa za kuua bakteria hadi watakapopona na kutokuwa na homa kwa saa 24 hadi 48, lakini lazima watumie kwa angalau siku 7.
Ingawa baadhi ya tetracycline zinazotumiwa kwa zaidi ya siku 10 zinaweza kusababisha madoa ya meno kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 8, doxycycline inashauriwa kutolewa kwa kipindi kifupi (siku 5 hadi 10) kwa watoto wa rika zote na inaweza kutumika bila kusababisha madoa ya meno au kudhoofisha enameli ya jino (angalia pia Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC): Utafiti kuhusu doxycycline na madoa ya meno).
Kinga ya Janga la Homa Kali Iletwayo na Chawa
Hatua za kudhibiti chawa zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi kuenea. Kwa mfano, nguo na matandiko yaliyojaa chawa yanapaswa kuoshwa kwa maji ya moto na kukaushwa kwa joto kali au kusafishwa kwa kutumia dobi. Pia, watu wanapaswa kuepuka kugusana na vichakuro wanaoruka na viota vyao.
Watu walioathiriwa na chawa wanaweza kupewa lindane au malathion (ambazo ni dawa za kuagizwa na daktari) ili kupaka kwenye ngozi zao na kuondoa chawa. Hata hivyo, kwa sababu chawa wa mwilini huishi kwenye nguo na matandiko ya watu, badala ya kwenye ngozi yao (kama wanavyofanya chawa wa kichwani na wa sehemu za siri), kutibu nguo na matandiko kwa kawaida kunatosha. Matandiko na nguo zinapaswa kuoshwa angalau mara moja kwa wiki katika maji ya moto (> 130F (> 54 C) na kukaushwa kwenye joto kali. Nguo na vitu visivyoweza kuoshwa vinaweza kusafishwa kwa maji au kufungwa kwenye mfuko wa plastiki na kuhifadhiwa kwa wiki 2. Matandiko na nguo pia zinaweza kutibiwa kwa kutumia kiua-dudu kinachoitwa permethrin.
Ugonjwa wa Brill-Zinsser
Ugonjwa wa Brill-Zinsser huwa kutokea tena kwa homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko, wakati mwingine miaka mingi baada ya maambukizi ya kwanza.
Baadhi ya viumbe vinavyosababisha homa kali iletwayo na chawa ya mlipuko hubaki mwilini. Huenda zikaamilishwa tena ikiwa mfumo wa kinga wa mtu umedhoofika.
Dalili za ugonjwa wa Brill-Zinsser karibu kila mara huwa nyepesi na hufanana na ugonjwa wa homa kali ilitwayo na chawa ya mlipuko. Homa hudumu kwa takriban siku 7 hadi 10. Watu wanaweza wasiwe na vipele.
Utambuzi na matibabu ya ugonjwa wa Brill-Zinsser unafanana na ugonjwa wa homa kali ilitwayo na chawa ya mlipuko.