Mfua ya ndege ni maambukizi ya virusi yenye aina za virusi vya mafua ambavyo kwa kawaida hutokea kwa ndege wa porini na kuku wa kufugwa.
Ni nadra kwa virusi vya mafua ya ndege kuenea kutoka kwa wanyama hadi kwa watu (kuenea kwa watu kunaweza kutokea ikiwa nyenzo za jenetiki za virusi hubadilika).
Karibia watu wote ambao wameambukizwa mafua ya ndege wamewahi kutagusana kwa karibu na ndege aliyeambukizwa (haienei kamwe kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine).
Watu wanaweza kuwa na ugumu mkubwa wa kupumua na dalili kama za homa.
Ili kugundua mafua ya ndege, madaktari hupima sampuli ya majimaji kutoka puani au koo ya mtu huyo.
Mafua ya ndege hutibiwa kwa dawa za kuzuia virusi.
(Ona pia Homa ya mafua.)
Mafua ya ndege husababishwa na aina kadhaa za virusi vya mafua vya A ambavyo kwa kawaida huwaambukiza ndege wa porini. Maambukizi yanaweza kuenea kwa ndege wa kufugwa. Hata hivyo, mara chache huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa watu. Inaweza kuenea kutoka kwa ndege hadi kwa watu ikiwa nyenzo za jenetiki za virusi imebadilika (hubadilika), na hivyo basi kuwezesha virusi kushikamana na seli katika njia ya hewa za binadamu. Karibu watu wote walioambukizwa mafua ya ndege wametagusana kwa karibu na ndege aliyeambukizwa. Mafua ya ndege karibia haisambai kamwe kutoka mtu mmoja hadi mwingine.
Maambukizi ya binadamu na aina ya mafua ya ndege aina ya H5N1 (angalia aina na makundi za homa ya mafua) yalitokea kwa mara ya kwanza Hong Kong mwaka wa 1997 na kisha yakaenea hadi mataifa mengine. Visa viwili vya H5N1 vimeripotiwa kwa binadamu nchini Marekani. Kisa kimoja kilitokea huko Colorado mwaka wa 2022 ikiwezekana kutokana na kutagusana na ndege waliokuwa wameambukizwa. Kisa cha pili kilitokea kwa mfanyakazi wa shamba la ng'ombe wa maziwa huko Texas mwaka wa 2024. H5N1 iliripotiwa miongoni mwa ng'ombe wa maziwa katika majimbo kadhaa mwaka wa 2024. Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) na Idara ya Kilimo ya Marekani (USDA) vinaendelea kufuatilia hali hiyo (ona CDC: Taarifa kuhusu Mafua ya Ndege na Mafua ya Ndege ya H5N1: Muhtasari wa Hali ya Sasa; pia tazama USDA: Ugunduzi wa Mafua ya Ndege Yanayosababisha Virusi Vingi (HPAI) katika Mifugo).
Mwaka wa 2013, mlipuko wa aina ya mafua ya ndege aina ya H7N9 ulianza kusini mashariki mwa China. Wimbi jingine la maambukizi kwa binadamu nchini China lilifikia kilele chake mwaka 2016–2017 likiwa na visa karibia 800, na tangu wakati huo ni visa vichache tu vimeripotiwa. Kote duniani, zaidi ya visa 1500 vya binadamu na angalau vifo 615 vimeripotiwa kwa Shirika la Afya Duniani tangu mwaka wa 2013. Maambukizi hayo yametokea zaidi katika jamii zinazokula ndege kutoka masoko ya ndege hai.
Aina zingine za virusi vya mafua ya ndege pia zimesababisha milipuko ya mara kwa mara ya maambukizi kwa watu.
Dalili za Mafua ya Ndege
H5N1 na H7N9, aina za virusi vinavyosababisha visa vingi vya mafua ya ndege kwa watu, vina athari sawa.
Watu wanaweza kuwa na dalili kama za homa (kama vile homa, kikohozi, koo kuuma, na maumivu ya misuli). Baadhi ya watu wana ugonjwa wa konjunktivaitisi (kuvimba kwenye konjaktiva, ambayo ni sehemu ya jicho). Baadhi wana ugumu wa kupumua au nimonia.
Utambuzi wa Mafua ya Ndege
Upimaji wa sampuli iliyochukuliwa kutoka puani au koo
Watu wanapaswa kuwasiliana na daktari ili kupimwa ili kubaini kama wana mafua ya ndege ikiwa wana dalili kama za homa pamoja na mojawapo ya yafuatayo:
Wametagusana na ndege katika eneo ambalo ndege wanajulikana kubeba maambukizi.
Wamewahi kutagusana na mtu aliyeambukizwa mafua ya ndege.
Daktari anaweza kutuma sampuli iliyochukuliwa kwa kusugua pua au koo kutumia pamba ili kupimwa.
Matibabu ya Mafua ya Ndege
Dawa za kupambana na virusi
Watu walioambukizwa hupewa baloxavir, oseltamivir, au zanamivir (dawa za kuzuia virusi zinazotumika kutibu homa ya mafua). Dawa hizi kwa kawaida huboresha uwezekano wa kuishi (tazama CDC: Kinga na Matibabu ya Kuzuia Ukali wa Virusi vya Mafua ya Ndege kwa Watu).
Uzuiaji wa Mafua ya Ndege
Watu wanapaswa kuepuka kutagusana na wanyama wagonjwa au waliokufa, hasa ndege wa porini na wa kufugwa, kuku, na ng'ombe. Bidhaa za chakula ambazo hazipikwa au hazijaiva vizuri, kama vile maziwa na bidhaa za maziwa ambazo hazijachemshwa kwa moto ili kuua vijidudu, pia zinapaswa kuepukwa. Usambazaji wa maziwa ya kibiashara nchini Marekani unapimwa, na hakuna virusi hai vinavyoweza kuambukiza vimepatikana katika maziwa ambayo yamechemshwa kwa moto ili kuua vijidudu. Wauzaji wa maziwa wanatakiwa kufuata taratibu za usalama wa chakula, ikiwa ni pamoja na kutuma maziwa tu kutoka kwa wanyama wenye afya kwenye usindikaji kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na kuchemsha kwa moto ili kuua vijidudu ni sharti kwa maziwa yanayouzwa madukani.
China inachanja ndege wanaofugwa nyumbani ili kuzuia virusi vya mafua ya H5 na H7. Mpango huu wa chanjo unaweza kusaidia kuzuia virusi vya mafua ya ndege kusambaa kutoka kwa ndege wa porini hadi kwa ndege wa kufugwa. Ndege wa kufugwa wana uwezekano mkubwa wa kutagusana na watu na kuwasambazia virusi.
Kuenea hudhibitiwa kwa kutambua na kuharibu makundi ya ndege wa kufugwa walioambukizwa.
Nchini Marekani, chanjo ya watu dhidi ya mafua ya ndege ya H5N1 inapatikana kwa ajili ya kusambazwa ikiwa itaonekana kuwa ni muhimu na mamlaka za afya ya umma. Chanjo ya kawaida ya homa ya mafua haizuii mafua ya ndege.