Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes

NaNora E. Renthal, MD, PhD, Harvard Medical School
Imekaguliwa naMichael SD Agus, MD, Harvard Medical School
Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Sept 2025
v38720818_sw

Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes huhusisha kufa (nekrosisi) kwa kiungio cha nyonga kwa watoto.

  • Ugonjwa huu unasababishwa na usambazaji hafifu wa damu kwenye sehemu ya juu ya sahani ya ukuaji ya mfupa wa paja karibu na kiungio cha nyonga.

  • Dalii za kawaida zinajumuisha maumivu ya nyonga na kupata shida kutembea.

  • Utambuzi wa ugonjwa unajikita kwenye dalili na eksirei na wakati mwingine upigaji picha kwa mvumo wa sumaku.

  • Matibabu yanajumuisha kufunga nyonga na kupumzika kitandani.

Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes kwenye osteochondrosis. Osteochondrosis ni tatizo la viungo vya ndani maeneo ya ukuaji wa mifupa hilo hutokea wakati mtoto anakua kwa kasi.

Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes hutokea sana kwa wavulana walio na umri kati ya miaka 5 na 10. Ugonjwa huu kwa kawaida unaathiri mguu mmoja pekee. Karibu asilimia 10 ya watoto wna ndugu ambaye ana ugonjwa.

Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes unasababishwa na usambazaji hafifu wa damu kwenye sahani ya ukuaji ya juu ya mfupa wa paja karibu na kiungio cha nyonga. Usambazaji hafifu wa damu husababisha mwisho wa mfupa wa paja kufa na kuanguka (avascular necrosis osteonecrosis). Sababu ya usambazaji duni wa damu kwenye ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes haijulikani.

Usambazaji wa damu kwenye sahani za ukuaji kwenye mfupa wa paja unaweza kuathiriwa na sababu zingine. Sababu hizo hujumuisha ugonjwa wa selimundu na haja ya kutumia steroid (pia huitwa glucocorticoids au corticosteroids) kwa muda mrefu, ambayo huweza kusababisha hali inayoitwa avascular necrosis ya nyonga. Hata hivyo, kuharibika kwa nyonga kwa sababu ya avascular necrosis kutokana na sababu hizi na nyingine zinazojulikana haichukuliwi kuwa ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes.

Fupa la Paja: Sehemu ya Kiungo cha Nyonga

Dalili za Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes

Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes unaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa nyonga kabla ya dalili kuu kutokea. Hata hivyo, uharibifu mkubwa unaweza kusababisha ugonjwa wa baridi yabisi wa kudumu kwenye nyonga.

Dalili ya kwanza ya ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes mara nyingi ni maumivu kwenye kiungio cha nyonga na kupata shida kutembea. Maumivu huanza taratibu na kuendelea polepole. Maumivu huwa yanakuwa makali wakati wa kujongeza nyonga au kutembea. Baadhi ya watoto pia wana maumivu kwenye goti. Hali ya kuchechemea inaweza kutokea, wakati mwingine kabla mtoto hajawa na maumivu makubwa.

Hatimaye, kujongeza kiungio kunaweza kuwa shida na misuli ya paja inaweza kupotea (kusinyaa) kwa kutotumika.

Utambuzi wa Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes

  • Tathmini ya daktari

  • Kwa kawaida eksirei

  • Wakati mwingine upigaji picha kwa mwangwi wa sumaku (MRI)

Madaktari wanashuku ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes kwa watoto ambao wana dalili halisi.

Madaktari wanafanya eksirei na wakati mwingine MRI endapo eksirei ni za kawaida au wanahitaji taarifa zaidi kuhusu ukali. Baadaye eksrei zinaweza kuonyesha mabadiliko kwenye sahani ya ukuaji, kama vile kuharibika kwa mfupa.

Madaktari wanafanya eksirei ya ziada ya mifupa ya mtoto endapo tatizo hilo lipo kwenye familia ya mtoto au miguu yote miwili ya mtoto imeathiriwa. Eksirei hizi zinachukuliwa kubaini matatizo ya urithi ya mifupa.

Vipimo vya damu vinafanywa ili kubaini matatizo mengine. Madaktari pia wanajaribu kubaini iwapo dalili hizo zinatokana na jeraha.

Matibabu ya Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes

  • Kupumzika kitandani na kufunga nyonga

  • Wakati mwingine upasuaji

Matibabu ya ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes hujumusiha kupumzika kitandani kwa muda mrefu na kufunga nyonga (kwa mfano, kwa plasta au banzi). Uchaguzi wa matibabu unategemea umri wa mtoto na kiwango cha uharibifu wa mifupa. Wakati mwingine kutoweza kujongea kutokana na kupumzika kitandani kunatosha. Hata hivyo, wakati mwingine kuzuia kabisa mjongeo kwa kutumia kuvuta, tanzi, plasta na vibanzi ni lazima. Matibabu hayo hufanya miguu izunguke kuelekea nje.

Tiba ya viungo inatumika kufanya misuli isikaze na kupotea.

Ikiwa mtoto ana umri wa zaidi ya miaka 6 na ana uharibifu mbaya wa mifupa, upasuaji unaweza kusaidia.

Matibabu kwa kutumia bisphosphonates (dawa inayosaidia kuongeza uzito wa mifupa) imekuwa na ufanisi, lakini tafiti zaidi zinahitajika.

Ubashiri wa Ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes

Bila tiba, ugonjwa wa Legg-Calvé-Perthes kwa kawaida unapata unafuu, lakini inachukua muda mrefu, kwa kawaida miaka 2 hadi 3, na kuna ongezeko la hatari ya ugonjwa wa baridi yabisi kutokea baadaye maishani.

Kwa tiba, matatizo yanakuwa mabaya kidogo. Watoto wenye umri wa chini ya miaka 8 na watoto hawaathiriwi pakubwa wanapotambuliwa kuwa na ugonjwa wana matokeo bora.