Ni nini maana ya jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa?
Mshtuko wa ubongo ni jeraha kwenye ubongo wako ambalo huathiri kwa muda mawazo na ufahamu wako.
Mfupa wa fuvu hulinda ubongo wako. Kiowevu kwenye fuvu lako pia hulinda ubongo wako. Hata hivyo, kichwa chako kikigongwa kwa kiasi cha kutosha, ubongo wako unaweza kusogea ndani ya fuvu la kichwa na kugongana na fuvu lako. Hii inaweza kuumiza ubongo wako na kubadilisha kwa muda jinsi ubongo wako unavyofanya kazi.
Huenda ukazimia (kupoteza fahamu) au huenda ukawa umechanganyikiwa tu
Madaktari wanaweza kufanya uchanganuzi wa tomografia ya kompyuta (CT) wa kichwa chako ili kuhakikisha ubongo wako huvuji damu au haujajeruhiwa.
Ukishapata jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa, kuna uwezekano kwamba unaweza kupata mishtuko ya ubongo katika siku za usoni, hususan ikiwa ubongo wako haujapona
Majeraha ya ubongo ya kujirudia yanayotokana na kupigwa/kugongwa yanaweza kuongeza uwezekano wako wa kupata uharibifu wa kudumu wa ubongo na kupoteza utambuzi
Ni nini husababisha jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa?
Jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa husababishwa na kitu kugonga kichwa chako kwa nguvu sana (majeraha ya kichwa). Hali hii inaweza kutokea wakati, kwa mfano:
Kuanguka na kugonga kichwa chako
Umejipata kwenye ajali ya gari au pikipiki
Umepigwa ngumi au kugongwa kwenye kichwa na kitu
Aina nyingi za spoti huweka watu katika hatari ya kupata jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa (tazama Sehemu ya Jeraha la Ubongo Linalohusiana na Spoti la Kupigwa/Kugongwa).
Zipi ni dalili za jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa?
Ikiwa una jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa, unaweza:
Maumivu ya kichwa na kuhisi kizunguzungu
Kutokuwa imara
Kuchanganyikiwa, ikiwemo kutunduwaa au kushtuka, kutokuwa na uhakika kuhusu alama au timu unayochezea, au kujibu maswali polepole
Kupoteza kumbukumbu, kama vile kutojua michezo ya timu au kutokumbuka kilichofanyika kabla na baada ya kujeruhiwa
Kuona vitu viwili viwili, au kuathiriwa na mwangaza
Mara chache, kupoteza fahamu kwa muda mfupi
Kuwa goigoi
Ni nini maana ya ugonjwa wa baada ya jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa?
Ugonjwa wa baada ya jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa ni wakati unapata dalili baada ya kuathiriwa na jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa. Unaweza kuwa na:
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu na wepesi wa kichwa
Kuwa na uchovu, kukasirika haraka, au kuathiriwa na mwangaza au kelele
Kutoweza kumakinika
Uwezo duni wa kukumbuka
Mfadhaiko na wasiwasi
Kwa kawaida dalili hizi hutoweka baada ya wiki moja au mbili. Kwa nadra, dalili hizi zinaweza kudumu kwa miezi kadhaa
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa?
Daktari wako anaweza kujua kuwa umepata jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa kulingana na dalili ulizonazo baada ya kupata jeraha la kichwa.
Ili kujua iwapo umepata majeraha yoyote ya ubongo, madaktari wakati mwingine hufanya yafuatayo:
Kufanya uchanganuzi wa tomografia ya kompyuta (CT) wa kichwa chako ili kuhakikisha ubongo wako huvuji damu au haujajeruhiwa.
Huenda usihitaji kipimo cha uchanganuzi wa CT ikiwa dalili zako zilitoweka ndani ya dakika chache baada ya kupata majeraha ya kichwa.
Je, madaktari wanatibu vipi jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa?
Daktari wako atakuelekeza:
Kupumzika
Umeze asetaminofeni ikiwa una maumivu ya kichwa
Usicheze michezo ya kugusana, inayokuweka katika hatari zaidi ya kupata jeraha la ubongo linalotokana na kupigwa/kugongwa, hadi daktari wako atakaposema kuwa majeraha yako ya kichwa yamepona kabisa na kwamba unaweza kurejea kucheza.