Endoskopia

Uhakiki Kamili: Jan 2026 NaThe Manual's Editorial Staff
Iliyosasishwa mwisho: Jan 2026
v34376975_sw

Endoskopi ni nini?

Endoskopi ni kifaa ambacho madaktari hutumia kuangalia ndani ya mwili wako. Endoskopi pia inaweza kutumika kufanya vipimo na kutibu magonjwa.

Endoskopi ina bomba lenye mwanga na kamera ndogo ya video kwenye mwisho wake. Kipfaa ni tupu Madaktari wanaweza kupitisha vifaa kupitia endoskopi ili kufanya vipimo na kutibu matatizo.

Endoskopi inaweza kuwa:

  • Haipindiki, imetengenezwa na metali ambayo haikunjiki

  • Inanyumbulika, hivyo inaweza kuinama pembeni kama nyoka

Endoskopi za ukubwa tofauti zinatumiwa kwa aina tofauti za mwili. Ukubwa ambao daktari hutumia unalingana na ni sehemu gani ya mwili wako inahitaji kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa. Kwa mfano, zinaweza kuwa:

  • Fupi na nyembamba: Kwa pua na sehemu ya nyuma ya koo yako (nasofarenogolaringoskopi)

  • Ndefu na nyembamba: Kwa ajili ya njia za upumuaji (bronkoskopi)

  • Fupi na pana: Kwa sehemu ya chini ya utumbo wako mpana (sigmoidoskopia)

  • Ndefu na pana: Kwa ajili ya tumbo yako (endoskopia ya juu) na utumbo (kolonoskopia)

Endoskopia ni nini?

Endoskopia ni kipimo chochote ambapo madaktari wanatumia bomba ya kutazama ili kupata mwonekano wa karibu wa sehemu ya ndani ya mwili wako. Endoskopia mara nyingi humaanisha kipimo ambacho madaktari hutazama kwenye njia yako ya mmeng'enyo wa chakula (utumbo au njia ya GI) kwa kutumia endoskopi inayoweza kunyumbulika.

Madaktari wanafanya aina mbili kuu za endoskopia ya GI:

  • Endoskopia ya juu—bomba inayoingia mdomoni mwako na chini kwenye umio wako, kuangalia umio, tumbo na sehemu ya utumbo mdogo wako

  • Endoskopia ya chini (kolonoskopia)—bomba inayoingia kwenye tundu lako la haja kubwa ili kuangalia rektamu na utumbo mpana

Sigmoidoskopia ni aina ya endoskopia ya GI ya chini ambapo daktari hutumia bomba fupi na huangalia tu sehemu ya chini ya utumbo wako mpana.

Kutazama Njia ya Mmeng'enyo wa Chakula kwa Kutumia Endoskopia

Bomba inayopinda inayoitwa endoskopia inatumiwa ili kutazama sehemu tofauti za njia ya mmeng'enyo wa chakula. Inapopitishiwa mdomoni (kama inavyoonyeshwa kushoto), endoskopia inaweza kutumiwa kuchunguza umio, tumbo na baadhi ya utumbo mdogo. Inapopitishiwa kwenye tundu la haja kubwa (kulia), endoskopia inaweza kutumiwa kuchunguza rektamu na utumbo mpana wote.

Kwa nini madaktari hufanya endoskopia?

Madaktari hufanya endoskopia ya GI ili kupata na mara nyingi kutibu matatizo kwenye umio, tumbo, utumbo na rektamu yako. Hata kama huna dalili, madaktari wanaweza kufanya endoskopia kuchunguza matatizo makubwa kama saratani ya utumbo mpana, ambayo inaweza kutibiwa ikiwa itagunduliwa mapema.

Madaktari wanaweza kutumia endoskopia ili:

  • Kujua ni kwa nini unapata dalili fulani

  • Kukagua watu wa umri fulani kwa matatizo—kwa mfano, ikiwa uko zaidi ya miaka 45, madaktari wanaweza kufanya kolonoskopia ili kuchunguza kama una saratini ya utumbo mpana

  • Kutibu matatizo fulani kwa kutumia zana ndogo ambazo zinaweza kutoshea kwenye endoskopia

Baadhi ya taratibu ambazo madaktari wanaweza kufanya kupitia kwenye endoskopia zinajumuisha:

  • Kutoa kipande kidogo cha tishu ili kukipima (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)

  • Kutoa vinyama, kama vile polipu kwenye utumbo wako mpana

  • Kudunga dawa, kwa mfano, dawa inayositisha kuvuja damu kutoka kwenye kidonda

  • Kusitisha kuvuja damu kwa kutumia leza, joto au umeme

Je, nitawezaje kuwa tayari kwa ajili ya endoskopia ya juu?

  • Itakulazimu uache kula na kunywa kabla ya kipimo—daktari wako atakwambia ni lini haswa

  • Daktari wako atakueleza ikiwa unaweza kumeza dawa zako za kawaida asubuhi ya uchunguzi

Je, nitawezaje kuwa tayari kwa ajili ya endoskopia ya chini (kolonoskopia)?

  • Utakunywa viwevu pekee siku moja kabla ya kipimo, hakuna vyakula vigumu

  • Itakulazimu uache kula na kunywa usiku kabla ya kipimo—daktari wako atakwambia ni lini haswa

  • Daktari wako atakueleza ikiwa unaweza kumeza dawa zako za kawaida asubuhi ya uchunguzi

  • Utatumia dawa ili kutoa kinyesi chote kutoka kwenye utumbo wako siku moja kabla ya kipimo—dawa hiyo inaweza kuwa vidonge, vimiminika unavyokunywa, au kimiminika kinachowekwa kwenye tundu la haja kubwa (enema).

Ni nini hufanyika wakati nina endoskopia?

Wakati wa endoskopia ya juu au kolonoskopia, unalala chini na vifaa vinaambatishwa kwenye mwili wako ili kupima shinikizo la damu, mdundo wa moyo wako na kiwango cha oksijeni kwenye damu yako wakati wa kipimo.

  • Utawekwa IV kwenye mkono wako kwa ajili ya viowevu na dawa

  • Kwa endoskopia ya juu, madaktari watakuweka dawa ya kufanya ganzi kwenye koo yako

  • Utapewa dawa ya IV ili kufanya utulie na kuwa mtulivu au kukuweka usingizini

Daktari ataingiza bomba polepole kwenye mwili wako.

Daktari wako ataweza kuona matatizo kama vile:

  • Wekundu

  • Vidonda vilivyo wazi (vidonda)

  • Kuvimba

  • Vishikizo visivyo vya kawaida

Utando na tabaka za ndani zaidi za mfumo wako wa utumbo (isipokuwa sehemu ya chini ya tundu lako la haja kubwa) hazina neva ambazo zinahisi uchungu, kwa hivyo hautahisi uchungu kama hautakuwa usingizini wakati wa vipimo hivi.

Endoskopia ya juu huchukua takriban dakika 15 hadi 30. Kolonoskopia inaweza kuchukua muda mrefu zaidi. Baada ya kuamka na kuhisi kuwa kawaida, utaweza kwenda nyumbani na rafiki au mwanafamilia na kupumzika hadi siku inayofuata.

Endoskopia ni salama?

Endoskopia kwa kawaida ni salama sana. Matatizo ni ya nadra lakini yanaweza kujumuisha:

  • Kuhisi mchovu kutokana na dawa ya kutuliza

  • Kuhisi vibaya kwenye sehemu ya mwili ambayo ilichunguzwa

  • Kiwango kidogo cha kuvuja damu

  • Jeraha kwenye sehemu iliyochunguzwa

  • Kujikuna koo baada ya endoskopia ya juu

  • Kupitisha gesi nyingi sana baada ya endoskopia ya chini

Mpigie simu daktari wako mara moja ikiwa una yoyoye ya dalili hizi baada ya endoskopia:

  • Homa

  • Maumivu makali kwenye tumbo yako

  • Maumivu ya kifua au kukosa pumzi

  • Kutapika, haswa ikiwa yana ueusi au damu

  • Damu kwenye kinyesi au kinyesi cheusi