Uonevu ni nini?
Uonevu ni kumuumiza mtu mwingine kupitia vitendo (kama vile kumpiga mtu au kuvunja mali zake) au maneno (kutania, kusumbua, au kutishia). Mchokozi anaweza kuwa mkubwa, mwenye nguvu, au mwenye umaarufu zaidi kuliko mwathiriwa.
Uonevu unaweza kutokea katika maeneo mengi, kama vile nyumbani, shuleni, au kazini. Unaweza kufanyika mara moja au ujirudie mara nyingi.
Wavulana na wasichana kwa pamoja wanaweza kuwa waonevu
Uonevu unaweza kufanyika katika umri wowote, kutoka umri wa kabla ya shule hati utu uzima
Wanafunzi wengi huonewa kupitia barua pepe, ujumbe mfupi, na mitandao ya kijamii (hali hii inaitwa unyanyasaji wa mtandaoni)
Kuonewa au kuonea watu si sehemu ya kawaida ya maisha ya utotoni
Kutuma ujumbe wa ngono ni utumaji wa kidijitali wa ujumbe au picha za ngono kwa mtu mwingine. Utumaji wa ujumbe wa ngono unaweza kusababisha uonevu ikiwa mtu anataka kumuumiza au kumwaibisha mtu ambaye picha au ujumbe wake wa ngono ulitumwa.
Ninawezaje kujua iwapo mtu anaonewa?
Watu wanaonyanyaswa wanaweza kuwa na:
Huzuni
Kuwa na fedheha
Majeraha
Wasiwasi
Kutojiamini
Mwathiriwa wa uonevu mwenye umri mdogo anaweza kuona aibu kumwambia mtu mzima. Walimu na wazazi mara nyingi huwa hawagundui kuwa mtoto anaonewa. Waathiriwa wengi huathiriwa kimwili na/au kihisia kutokana na kuonewa.
Waonevu hujifunza tabia mbaya ambazo zisiporekebishwa, zinaweza kusababisha vurugu zaidi. Waonevu wana uwezekano mkubwa wa kushindwa kusalia shuleni, kuajiririwa, au kuwa na mahusiano thabiti wakiwa watu wazima, na wana uwezekano mkubwa wa kufungwa gerezani katika maisha yao ya baadaye.
Ninapaswa kufanya nini ikiwa ninaonewa?
Uonevu ni mbaya. Ikiwa mtu anakuonea, unapaswa:
Kumwambia mtu mzima
Kumwondokea
Kubadilisha shughuli zako za kila siku ili umwepuke anayekuonea
Kuzungumza na tabibu au mshauri wa kisaikolojia
Kujifanya kana kwamba unapuuza uonevu huo ili anayekuonea apoteze hamu ya kuendelea
Ikiwa uonevu unafanyika shuleni, wafahamishe viongozi wa shule.
Ninapaswa kufanya nini ikiwa mtu mwingine anaonewa?
Usipuuze uonaji huo. Kitu cha muhimu zaidi cha kufanya unapotambua kuwa mtu anaonewa ni kushughulikia hali hiyo mara moja.
Ikiwa mtoto wako anaonewa:
Pata ukweli kutoka kwa mtoto wako na uwaambie maafisa wa shule
Mkumbushe mtoto wako kwamba unonevu si kosa lake na si sawa kamwe
Mwambie mtoto wako ajaribu kumpuuza anayemwonea
Pata usaidizi wa polisi au matibabu ikihitajika
Mtafutie mtoto wako usaidizi wa ushauri nasaha ikihitajika