Visababishi vya Kawaida vya Enemia ya Upungufu wa Madini Chuma—na jinsi ya Kuitibu

Maoni06/05/25 Gloria F. Gerber, MD, Johns Hopkins School of Medicine, Division of Hematology

Karibu theluthi moja ya watu wazima wa Marekaniwanaweza kuwa na upungufu wa madini chuma. Tunahitaji madini chuma ili kutengeneza himoglobini, dutu iliyo kwenye seli nyekundu za damu ambazo hubeba oksijeni kote mwilini. Dalili za kawaida za upungufu wa madini chuma zinajumuisha kupata shida kumakinika na uchovu. Lakini watu ambao wanapata dalili hizi wanaweza kudhani zinatoka kwenye kisababishaji kingine na kutochukua hatua ili kushughulikia upungufu wa madini chuma uliopo. Usipodhibitiwa, upungufu wa madini chuma unaweza kusababisha enemia ya upungufu wa madini chuma. Dalili za enemia ya upungufu wa madini chuma zinaonekana hatua kwa hatua na zinafanana na dalili zinazosababishwa na aina zingine za anemia. Dalili kama hizo zinajumuisha uchovu, udhaifu, upungufu wa hewa na kusawajika. Wakiwa na kiwango cha chini cha madini chuma, baadhi ya watu wanaweza kupata dalili za pika (kutaka kula kitu ambacho si chakula, kama vile barafu, uchafu, rangi au chaki).

Kushughulikia enemia ya upungufu wa madini chuma huanza kwa kutambua na kushughulikia kisababishi cha upungufu wa madini chuma, kisha kwa kawaida kurejesha hifadhi ya madini chuma kwenye mwili. Huu ni mwonekano wa karibu wa baadhi ya visababishi vya kawaida zaidi vya enemia ya upungufu wa madini chuma na kile watu wanaweza kutarajia wakati hali hiyo inatibiwa.

Kisababishi #1 – Upungufu wa damu wa kawaida

Kwa watu wazima, upungufu wa madini chuma unasababishwa sana kwa kawaida na upungufu wa damu. Upungufu huu wa damu unaweza kutokana na vyanzo kadhaa. Kidonda au kiwewe kinaweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu kwa kipindi cha muda mfupi. Kwa wanawake ambao wapo kwenye hedhi, damu ya hedhi ndiyo kisababishi cha kawaida zaidi cha upungufu wa madini chuma. Wakati mwingine damu ya hedhi inaweza kukosekana kama kisababishi kwa vijana. Kwa wanaume na wanawake waliokoma hedhi, kwa kawaida upungufu wa madini chuma unaashiria kuvuja damu, mara nyingi kwenye njia ya mmeng'enyo wa chakula—kwa mfano, kutoka kwenye kidonda kinachovuja damu au polipu kwenye utumbo mpana. Kuvuja damu kali kwa sababu ya saratani ya utumbo mpana ni kisababishi madhubuti kwa watu wa umri wa kati na wazee.

Kisababishi #2 – Unyonyaji uliopungua

Unyonyaji madini chuma uliopungua kwenye njia ya mmeng'enyo wa chakula, unaojulikana kama hali ya kushindwa kunyonya virutubishi, inaweza kusababisha kutoka matatizo mbalimbali. Ugonjwa wa seliaki ni tatizo la kawaida linalosababisha hali ya kushindwa kunyonya virutubishi. Visababishi vingine vinajumuisha upasuaji wa bariatric na uondoaji wa utumbo na pia matatizo ya jeni yanayotokea kwa nadra.

 

Kisababishi #3 – Lishe isiyotosha / mahitaji yaliyoongezeka

Katika Marekani, kwa nadra anemia hutokana na kukula madini chuma kidogo zaidi kwa sababu madini chuma ya zaida yanaongezwa kwa vyakula vingi. Lakini kwa baadhi ya watu walio na ongezeko la mahitaji ya madini chuma, lishe yenye madini chuma kidogo inaweza kusababisha upungufu wa madini chuma na hata enemia ya upungufu wa madini chuma. Wanawake wajawazito, ambao mara nyingi huanza ujauzito wao kwa upunguaji mdogo wa hifadhi za madini chuma, wana ongezeko la mahitaji ya madini chuma. Vile ujauzito unaendelea, ongezeko la kiwango cha damu na mahitaji ya kijusi yanaweza kusababisha upungufu wa madini chuma--wakati mwingine wenye anemia, wakati mwingine bila anemia. Watoto wachanga na watoto wadogo wanaweza pia kuwa katika hatari ya upungufu wa madini chuma kwa sababu ya lishe zao, haswa ikiwa kwa sana ikiwa ni wanaochagua wanachokula au kula kiwango kikubwa cha bidhaa za maziwa.

Kisababishi #4 – Dialisisi

Watu walio kwenye dialisisi kwa sababu ya figo kushindwa kufanya kazi, haswa wale wanaotumia dawa ambazo zinasisimua mwili kutengeneza seli nyekundu za damu (bidhaa sinazosisimua erythropoiesis), wanaweza kuwa katika hatari ya upungufu wa madini chuma. Kwa kawaida, watu hawa wanafuatiliwa mara kwa mara kuhusu upungufu wa madini chuma.

Jinsi Enemia ya Upungufu wa Madini Chuma Inatambuliwa na Kutibiwa

Ni vyema zaidi kufikiria upungufu wa madini chuma kwa upana. Anemia inaweza kuwa matokeo mabaya zaidi, lakini upungufu wa madini chuma unapaswa kushughulikiwa hata kama bado mtu hana upungufu wa damu. Anemia inatambuliwa kwa uchunguzi wa mara kwa mara wa damu unaojulikana kama hesabu ya damu. Kutambua upungufu wa madini chuma kuna changamoto kubwa kidogo. Kipimo sahihi zaidi cha upungufu wa madini chuma ni kipimo cha kiwango cha damu cha ferritin (protini inayohifadhi madini chuma). Kiwango kidogo cha ferritin kinaashiria upungufu wa madini chuma. Hata hivyo, wakati mwingine viwango vya ferritin ni vya kupotosha kwa sababu vinaweza kuinuka kwa uongo (na hivyo kuonekana kuwa kawaida) kwa sababu ya uharibifu wa ini, kuvimba, maambukizi au saratani. Watu wanapaswa kuhakikisha kuwa madaktari wanafahamu kuhusu hali nyingine yoyote ya matibabu walio nayo kwa sababu baadhi zinaweza kuathiri matokeo ya kipimo.

Mara upungufu wa madini chuma unapobainishwa, matibabu yanajumuisha kushughulikia kisababishi kikuu cha upungufu huo, ikiwa ni pamoja na kusitisha kupungua kwa damu na kurekebisha madini chuma yaliyopungua mwilini. Kwa watu wengi, lishe yenye madini chuma mengi (ikiwa ni pamoja na vyakula kama vile nyama, shellfish, matunda yaliyokaushwa, nafaka, majani ya kijani na maharage) haitoshi kusheheneza hifadhi za madini chuma na uongezeaji kwa njia ya kinywa au mshipani unahitajika.  

Kile cha Kujua Kuhusu Virutubishi Madini Chuma kupitia Kinywani

Kusahihisha enemia ya upungufu wa madini chuma kwa kutumia virutubushi vya madini chuma kupitia kinywani kwa kawaida huchukua takriban wiki 6, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kujaza kikamilifu hifadhi za madini chuma hata baada ya kuvuja damu kuacha. Kwa kawaida virutubishi vya madini chuma vinatumiwa kupitia mdomo. Virutubishi vya madini chuma hufanya kinyesi kionekane kuwa cha kiza au cheusi na mara nyingi husababisha kufunga choo.

Virutubishi vya madini chuma vina uzoefu wa kusababisha matatizo ya kumeng'enya ikiwa ni pamoja na kuvimba, mikakamao na kufunga choo. Habari njema ni kuwa madaktari wengi watapendekeza kutumia virutubishi kila baada ya siku moja, jambo ambalo linaweza kusaidia unyonyaji na kupunguza athari mbaya. Watu ambao wako tayari kuanza kutumia virutubishi vya madini chuma, wanapaswa kuzungumza na daktari wao kuhusu mizio na athari mbaya kabla hawajaanza. Kuna fomula kadhaa za madini chuma ambazo daktari anaweza kutoa na wakati mwingine matibabu mengine kama vile vilainishi kinyesi au vitamini C zinaweza kupunguza dalili mbaya za kumeng'enya.

Hatimaye, ni muhimu kwa wagonjwa kujua kuwa upungufu wa madini chuma ni wa kawaida kiasi na ni muhimu kuwa na udhibiti, iwe unasababisha anemia au la. Ili kupata maelezo kuhusu enemia ya upungufu wa madini chuma, tembelea Ukurasa wa miongozo au Kweli za Haraka kuhusu mada hiyo.